Hivi mchina ana technolojia gani ya kumsinda Mmarekani?

Free market economy etii 😀 ni vizuri kuota
 
Ukianza wewe si mbaya
 
Kwamba yakijadiliwa mambo ya nchi kipi hasa kitabadilika au badilishwa.

Jukwaa la siasa limejaa hayo mambo so far mpaka sasa umeshuhudia mabadiliko gani ? Tumekuwa kama U.S ?, tumekuwa kama China ? , tumekuwa kama Russia ?, Tumekuwa kama Singapore ? Tumekuwa kama SK ? , tumekuwa kama France ?, Tumekuwa kama Canada ?
Kipi kimebadilika au tuna endelea kuwa wapumbavu tu.

Bila kuchukua hatua za dhati hata kupigana unafikiri kuna kitu kita badilika hapa nchini kwa michango ya JF ?

Acha Watanzania wajifariji hata kwa hiki kidogo.

Kama ufurahishwi organize vijana na Watanzania yapatikane mabadiliko ya jasho na damu kama unaweza sio kuponda watu humu walioamua kujifariji.
 
Wewe hayo mambo ya nchi umeyajua , umechukua hatua gani baada ya kujua? , Pathetic[emoji706]
 
Mkuu uijadili bongo unaijadili nini!?
Tanzania nchi ambayo wasomi hawapewi kipaumbele!?
 
Kivipi embu nieleweshe?
Maana kuna mataifa yapo na mapigano na wanatumia Chinese made weapons.
Biashara ni Vita mkuu , mfano;unadhani alieifungia Huawei Marekani ni wanasiasa pekee na watu wa usalama ? pale kulikuwa na mkono wa matajiri wakubwa , Huawei ilikuwa kampuni inayokuwa kwa kasi ya upepo wa kisulisuli na kuwa tishio kwa kampuni za Kimarekani na kilichofanyika ni kuikata miguu ianze upya, hizi ni figisu ambazo popote pale utazikuta kwenye vita ya maendeleo.
Mmarekani hawezi igusa Sumsung pale Korea kwasababu ushirikiano wa S.Korea na Marekani ni mkubwa zaidi kuliko Korea na China.
Kwenye swala la China kuuza Siraha hawezi mpiku Mmarekani japo anauza, Ndio kashikilia mtandao wa Black Market karibia dunia nzima ,Marekani haijaanza Vigisu jana yaani anazijua China anajifunza... Rejea namna USSR Ilivyo collapse
 
Tofauti kubwa ni Wamarekani wavumbuzi wote ni wageni.

Wenye asili ya Marekani wamevumbua vitu vichache sana.
 
Tofauti kubwa ni Wamarekani wavumbuzi wote ni wageni.

Wenye asili ya Marekani wamevumbua vitu vichache sana.
Mfano wa wenye asili ya Marekani waliovumbua hivyo vichache ni wakina nani na vitu gani kwa Mfano?
 
Jiulize hao ma Dr wa aina gani na wamepitaje!?
Na hata kama wamepita je wanasikilizwa na kupewa uhuru wa mawazo!?
Watu kama kina prof Kabudi una mashaka na elimu yao? Ukiwa msomi kama uko huko na husikilizwi basi ni vizuri uondoke.
 
Ni wale wale. Hata kuandika maneno ya kiswahili hujui, sitegemei uelewe point yangu. Elimu yetu imezaa ma-graduate hovyo kabisa.
 
Ni wale wale. Hata kuandika maneno ya kiswahili hujui, sitegemei uelewe point yangu. Elimu yetu imezaa ma-graduate hovyo kabisa.
Hongera kwako upo vizuri.

Tukomboe masihi na umasikini huu ongoza njia sisi wanafunzi wako twasubiri muongozo wako.
 
Watu kama kina prof Kabudi una mashaka na elimu yao? Ukiwa msomi kama uko huko na husikilizwi basi ni vizuri uondoke.
Tuseme nipo katikati.
Ila uhalisia tunaujua mkuu Tanzania wasomi stahiki hawasikilizwi maoni yao.
Kama wangekua wanasikilizwa Tanzania isingekua hapa tulipo.
 
Kwenye pharmaceuticals mchina ana company gani inayoweza kupambana na high tech giant multinational pharmaceuticals za US kama johnson and jonson? na zingine nyingi tu mchina ana kampuni gani? ya madawa ambayo ipo even kwenye tano bora duniani? huyo mchina ambaye utafiti wa MUHAS ulionyesha wazi dawa zake nyingi za kichina zinaua figo ndo ampite US?
 
Kuna dawa isio na madhara ? Tuanze na chanjo za Covid19 za U.S
 
Lete ushahidi hapa wa dawa za China zinazoleta madhara ya figo.
Ila hiyo kampuni uliyoisemea kuna dawa zake nyingi zimepigwa marufuku Tanzania na vipodozi vyake maana huleta vimelea vya carcinoma.
Mitandao ipo bro nenda kagoogle uone jinsi China walivyoendelea kwa kuleta herbal medicine katika uwanda wa pharmaceuticals science.
Na dawa zao zime prove kwa kiasi kikubwa,na dawa za herbs za kichina zimeonekana kuwa too active kwa early stage of carcinoma.
Field yangu hiyo nimesoma na nimepita nyanja za wote wawili hao mkuu.
We kama unabisha kafuatilie.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…