Hivi mnawezaje kuishi Dodoma?

Dodoma ni mahali pazuri kuishi, nimeishi maeneo mengi lakini kwa Dodoma nimefika, hali hii ya hewa ni nzuri sana kwa afya, usafiri hauna changamoto, nyumbani za kupanga ni za kutosha, hakuna foleni, unaweza kujenga nyumba katika eneo kubwa tu la kiwanja nk

Zingine ni changamoto za ugeni tu, Arusha kuna maeneo ya hovyo, Dar, Mbeya, Morogoro nk lakini naheshimu mahali ambapo wengine wanabarikiwa kuishi
 
Huwa nawashangaa sana wanaoichukia Dom eti kuna joto😀😀.Huku Dar ukienda kazini lazima ubebe kitambaa cha kujifutia majasho.Hatukatai Dom kuna joto(moderate) kipindi cha mchana ila usiku kuna ubaridi na kuanzia mwezi wa 6 hadi wa 9 Dom kuna baridi kama vile ya Mbeya
 
Dodoma ni sehemu ya kuishi mtu mwenye ramani na pesa. ni sehemu nzuri sana kibiashara pia.
 
Kwa kawaida dodoma mvua tunategemea kuanzia December na April mwishoni mvua zinaacha kabisa mpaka mwakani.
Kuhusu nyumba ulizosema mbaya na hazina rangi, hizo kila mkoa zipo inategemea wewe umefikia wapi.
Kuhusu nauli za daladala, sumatra wa dar ndo hao hao wa mikoa yote ndio waoregulate nauli. Achaga kauongo !
 
Bei ya nyumba umesahau ,nyumba ni ghali sana dodoma
 
Kwa kawaida dodoma mvua tunategemea kuanzia December na April mwishoni mvua zinaacha kabisa mpaka mwakani.
huyo jamaa ni walewale "hater" nina wasiwasi kama kweli amewahi kufika Dom manake anajichanganya mwenyewe anasema eti anakaribia mwakamzima hajaona mvua wakati msimu wa masika mwakahuu Dom mvua ilinyesha ya kutosha hadi kuvunja rekodi😀😀
 
Hauna kiwanja ulichonunia uniuzie maana aisee Dodoma hapafai?
 
Sijawahi shindwa kuishi Mkoa wowote ila extremely joto kama Dar hapana na extremely baridi kama Njombe sitaki.
 
Ndio kinachoendelea hapa.

Sasa hao wa Dar wavumilie tuu kwamba Dom hakuna uswazi na Wala haitakuja kuwa na uswazi Wala Msongamano wa kisenge kisenge kama huko Dar kunakonuka.
 
Ebu tuachie jiji letu, ukipashindwa kuishi wapo wengine wataweza.

Sio kila mahala ni pa kila mtu.
 
Kiufupi ukifika Dom Jiji lote ni jipya sio sawa na huko Mikoani Dar au kwingine kukikojaa uswazi na uswahili.

Binafsi napenda kuishi Dom sema ndio Sina fursa Kwa Sasa
 
Watu wanaishi Khartoum hakuna miti na joto 40°C ndio ushindwe kuishi Dodoma?

Usipoishi Dodoma kwenye pesa utaishia wapi pengine? Acha uzushi wa kijinga
Ishi popote unapotaka mimi sijakupangia.
Sijawahi shindwa kuishi Mkoa wowote ila extremely joto kama Dar hapana na extremely baridi kama Njombe sitaki.
Kama ambavyo hupataki Dar na Njombe. Nami ndivyo sipataki Dodoma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…