Hivi mnawezaje kuwapeleka watoto wenu wa kike wakafanye kazi za ulinzi?

Hivi mnawezaje kuwapeleka watoto wenu wa kike wakafanye kazi za ulinzi?

Binafsi siamini katika 50/50 na sijawahi kuamini kuwa mwanamke anaweza kuwa sawa na mwanaume

Inatokea mzazi unampeleka mtoto wako jkt aje awe mlinzi wa makampuni anakesha akiwa lindo ni ajabu hii kuwa hakuna kazi nyingine?

Tumeona vita nyingi duniani kama kule middle east na Ukraine Frontline haina soldiers wa kike hii ni dhahili kuwa mtoto wa kike sio wa tasnia ya ulinzi, wako soft sana na siku zote ni wa kupambaniwa na wanaume

Tofauti na vigogo ambao hata watoto wao wakiwa wanajeshi na askari huwa katika vitengo maalum ambavyo kwa namna moja au nyingine wanakuwa hawahusiki na mission ngumu ngumu na lindo, kwa masikini mwenzangu kumpeleka mtoto wako akafanye kazi za ulinzi ni ukosefu wa uwajibikaji kwa mtoto wa kike ni hayo tu.

Kwanza usifananishe kampuni za ulinzi na jeshi, jeshi ni different levels , different roles.
Hivi ni vitu viwili tofauti

Naona unajichanganya sana, front line ina watoto wa kike, mostly ni field medics, snipers (japo wachache) , wengi ni field hospital front line, wengine wako MI wana conduct recon, wengine ni marubani waki conduct flight sorties
 
Kwan. Kazi ya Ulinzi ni dhambi au ni kosa kisheria Kwenda Lindo au Kumlinda Rais zote ni kazi za Ulinzi
Umekunywa chai lakini ?
Unadhani kumlinda rais anapata hiyo nafasi chapalikanchuri wa isimikinyi huko? Jidanganye
 
Kwanza usifananishe kampuni za ulinzi na jeshi, jeshi ni different levels , different roles.
Hivi ni vitu viwili tofauti

Naona unajichanganya sana, front line ina watoto wa kike, mostly ni field medics, snipers (japo wachache) , wengi ni field hospital front line, wengine wako MI wana conduct recon, wengine ni marubani waki conduct flight sorties
Hoja yangu ni kuwa hivyo vitengo vya kuwa medical doctors na vingine havipati chapalikanchuri na mbugila mbugila kwa nchi zetu hizi za kujuana

Hivyo ni vitengo maalum ndani ya jeshi kwa masikini utashika Sr na kwenda lindo tu
 
Kwanza mi huwa nashangaa sana hata wale wanaoruhusu watoto wao wa kike kupitia jeshi baada ya form six,.....hamna cha ukakamavu wanaoupata huko zaidi ya kwenda kuwa MBOGA za watu tu,......🚮🚮
 
Binafsi siamini katika 50/50 na sijawahi kuamini kuwa mwanamke anaweza kuwa sawa na mwanaume

Inatokea mzazi unampeleka mtoto wako jkt aje awe mlinzi wa makampuni anakesha akiwa lindo ni ajabu hii kuwa hakuna kazi nyingine?

Tumeona vita nyingi duniani kama kule middle east na Ukraine Frontline haina soldiers wa kike hii ni dhahili kuwa mtoto wa kike sio wa tasnia ya ulinzi, wako soft sana na siku zote ni wa kupambaniwa na wanaume

Tofauti na vigogo ambao hata watoto wao wakiwa wanajeshi na askari huwa katika vitengo maalum ambavyo kwa namna moja au nyingine wanakuwa hawahusiki na mission ngumu ngumu na lindo, kwa masikini mwenzangu kumpeleka mtoto wako akafanye kazi za ulinzi ni ukosefu wa uwajibikaji kwa mtoto wa kike ni hayo tu.
Ulichoandika ni sahihi kabisa lakini kwa hali hii ya maisha tutafanyaje!? Maisha ya huku mtaani ni zaidi ya ulinzi. Acha wakajipambanie.
 
Kwanza mi huwa nashangaa sana hata wale wanaoruhusu watoto wao wa kike kupitia jeshi baada ya form six,.....hamna cha ukakamavu wanaoupata huko zaidi ya kwenda kuwa MBOGA za watu tu,......🚮🚮
Umesema kweli mkuu nimepita huko nimeona mengi nawashauri wazazi wakatae hii kitu kwa watoto wao wa kike
 
Sijajua ulitaka kumaanisha nini?

Kwanza kwenda JKT hasa ya kujitolea muhusika mara nyingi ndo anakuwa na msukumo wa ndani...... akiamini anaenda kuwa labda askari kwenye jeshi au taasisi nyinginezo za ulinzi...

Kwenda JKT pia kulitokana na mazingira pengine Hana option nyingine zaidi ya kwenda JKT akiamini huko atatimiza lengo lake.....

Kwenda JKT inaaminika ni njia ya kwenda kukuza vipaji na ubunifu plus kujifunza stadi kazi za maisha mfano kilimo, ufugaji, music, upishi, ufundi, udereva wapo waliotoka majumbani mwao hawana skills yoyote kufika kule wakajikuta wanaongeza ujuzi kwa namna moja ama nyingne....

Kwenda JKT na kuajiriwa makampuni ya ulinzi ni vitu viwili tofauti.....

Nijuavyo JKT ni shule mama ya kuwaandaa vijana tayari kulitumikia Taifa kupitia uzalendo...... Ambapo badae zikitoka ajira za jeshini ama taasisi nyinginezo za ulinzi km police, uhamiaji inakuwa rahisi kwa mtu aliyefuzu kutoka JKT kama mafunzo ya awali.....

Kutokana na changamoto za ajira majeshini inawalazimu watafute mbadala wa kazi wakisubiri hizo ajira jeshini ndo utakuta wameajiriwa maybe makampuni ya ulinzi......

Yapo makampuni ya ulinzi ambayo hata la saba au form four anaenda ili mradi ujue kusoma na kuandika......

Vijana maua...... Popote huchanua

Twendeni Tukalijenge Taifa.....

Mamaa walilee, mamaaa walileee

Mama walileee mamaa walilee

Iyoo mamaah iyoooh....

Iyoo mamaah iyoooh

Iyoo mamaah iyoooh.... Maah...

822kj
 
Back
Top Bottom