Hivi mtoto kumaliza darasa la Saba ni kitu cha kuandalia sherehe?

Hivi mtoto kumaliza darasa la Saba ni kitu cha kuandalia sherehe?

Kusini kunachekesha Sana yaani siku ya mahafali ya shule ya msingi mzazi anakwenda kukopa hela kabisa ili afanye shughuli nyumbani karibia mziki wa kukodi laki tatu chakula laki mbili eti kusherehekea mtoto kamaliza la Saba kweli jamani elimu ya msingi ni kitu cha kujivunia hivyo?
Ingawa inashangaza lakini hupaswi kushangaa kwa tulipofikia Sasa; watu (hususani kina mama) wanafikiria 'kupali' tu muda wote hivyo wanahitaji kasababu hata kama kana uzito mdogo kama wa sisimizi. Kama inawekwa sherehe kubwa kisa tu Kuna katoto kanatoboa masikio, tutashangaa nini' ikiwekwa kwa kumaliza la saba?!!!!!🤣🤣🤣
 
Tatizo ni mtu kukopa (Living beyond ones means) na tatizo kubwa kabisa ni ulimbukeni Huu ukishakuwa utamaduni na utaratibu kwa mtoto mdogo ambaye hajapevuka na kuweza kuelewa anaweza kuona wewe humpendi kwanini wenzake wanafanyiwa party (Hapa ndio linakuja suala hata la kuhakikisha hata hizo shule anakwenda kwenye shule za watu anaoendana nao unless anaweza akawa a very very tiny fish in a very very big Pond) hivyo maisha yake yasiwe ya furaha na kujishitukia...

All in all kama wanajamii tumezidi sana kuishi fake lives na kusujudu vitu materialistic hivyo kuwa watumwa wa maisha badala ya kufurahia maisha - Ingawa nina-feel wazazi wanachokipata sababu ni kama emotional blackmail na kwa mzazi kusema no kwa mtoto inakuwa ngumu (Ndio maana kuna kipindi Ulaya walitaka kupiga marufuku matangazo yanayowalenga directly watoto ili kuwa-blackmail wazazi)

It's the sad world that we currently live in.... It's a Rat Race chasing an Illusion.
 
Kusini kunachekesha Sana yaani siku ya mahafali ya shule ya msingi mzazi anakwenda kukopa hela kabisa ili afanye shughuli nyumbani karibia mziki wa kukodi laki tatu chakula laki mbili eti kusherehekea mtoto kamaliza la Saba kweli jamani elimu ya msingi ni kitu cha kujivunia hivyo?
Mkuu acha asherehekee milestone ya mwanae. Ukipata nafasi ya kufurahi furahia maana mateso ni mengi
 
Chanzo cha hizo sherehe ni vikundi vya huku mtaani hasa wakina mama wanachangiana katika sherehe.

Unakuta mtu kachangia sana katika sherehe za wenzake mixer kutoa zawadi hivi unadhani na yeye akipata sababu kwanini asifanye sherehe kurudisha pesa zake.

Tena bora hao wa sherehe za kumaliza darasa la saba nowdays huku uswazi wanachangishana hadi arobaini ya kumtoa mtoto, birthday, ubatizo na vipaimara wakati zamani ilikuwa ni sherehe ndogo za kifamilia zaidi.
 
Kusini kunachekesha Sana yaani siku ya mahafali ya shule ya msingi mzazi anakwenda kukopa hela kabisa ili afanye shughuli nyumbani karibia mziki wa kukodi laki tatu chakula laki mbili eti kusherehekea mtoto kamaliza la Saba kweli jamani elimu ya msingi ni kitu cha kujivunia hivyo?
Ndio watu wanafanya kipaimara, komunio, birthday 🎈

Sembuse kwenye darasa la Saba kaka huwezi pangia watu vya kufanya period!!
 
Kusini kunachekesha Sana yaani siku ya mahafali ya shule ya msingi mzazi anakwenda kukopa hela kabisa ili afanye shughuli nyumbani karibia mziki wa kukodi laki tatu chakula laki mbili eti kusherehekea mtoto kamaliza la Saba kweli jamani elimu ya msingi ni kitu cha kujivunia hivyo?

Naomba kufahamu umuhimu wa pre form one kozi zinatozwa laki 4 kwa miezi 2. Au ni loop_hole ya kupiga pesa?
 
Ni ujinga na hufanywa na watu wajinga hata hizo sherehe sijui ubatizo,kipaimara, arobaini na hizi za shule kuitoa shule kuja kuifanyia nyumbani ni ujinga haijarishi wewe ni tajiri au ni maskini ni ujinga wala siwezi kuhudhuria kwenye ujinga wa namna hii
Mkuu jitahidi kufurahia maisha. Ukifa mali zako zote na mkeo zitaliwa na wajanja na hamna kitu utafanya
 
Ni maisha yao ila kwangu mimi binafsi hapana. Nilikataa kufanya mahafali ya chuo familia nzima iliniona wa ajabu wakisema kama ni gharama si wanagharamia wao.

Niliwaambia hiyo gharama ya kutoka mkoa watu zaidi ya 10, chakula, malazi, usafiri na bado gharama za sherehe ni bora wanipe nifanye mtaji au wanunue kuku wafuge huko nyumbani kwa sababu n wastage of money ambazo kiuhalisia hazipo.
 
Mkuu jitahidi kufurahia maisha. Ukifa mali zako zote na mkeo zitaliwa na wajanja na hamna kitu utafanya
Issue ni kwenye malezi hao watoto unao wafanyia party za kila aina siku ukiishiwa watajua huwapendi milladayo ameripoti matukio ya watoto kujinyonga na kunytwa sumu kisa hawajafanyiwa sherehe za ubatizo na za kuzaliwa.

Elewa kabisa mtoto umleavyo ndivyo akuavyo unapofanya hivyo mtoto anaweka kama sheria kuwa kwa kila tukio zuri lazima umfanyie sherehe ukiacha anajenga chuki huku akinishinikizwa na mama yake hasa hawa wa 2000.

Ujue kufurahia maisha siyo lazima nifanye sherehe kwa kila tukio la hasha!

Mimi hapa ninaposema kuna mtoto wa dada alimwambia mama (bibi yake) mimi Anko p namchukia sana akaulizwa kwa nini eti sijawahi mpa zawadi siku ya Happybirthday yake wala kumtakia heri!! Je hii ni sawa mtoto kujenga chuki kisa tu hujampa zawadi?
 
Kusini kunachekesha Sana yaani siku ya mahafali ya shule ya msingi mzazi anakwenda kukopa hela kabisa ili afanye shughuli nyumbani karibia mziki wa kukodi laki tatu chakula laki mbili eti kusherehekea mtoto kamaliza la Saba kweli jamani elimu ya msingi ni kitu cha kujivunia hivyo?
Sasa si afadhali huyo wa drs la saba? Haujakutana na grand graduation ya baby class. Mtu anatumia hata milioni kufanya sherehe ya baby class.

Wakati mimi kwenye mahafari ya kidato cha nne nilitumia chini ya laki 2 hapo nimejumuisha mavazi hadi cameraman
 
Kusini kunachekesha Sana yaani siku ya mahafali ya shule ya msingi mzazi anakwenda kukopa hela kabisa ili afanye shughuli nyumbani karibia mziki wa kukodi laki tatu chakula laki mbili eti kusherehekea mtoto kamaliza la Saba kweli jamani elimu ya msingi ni kitu cha kujivunia hivyo?
Maisha yao, kukopa wanakopa wao, mtoto wao.

Tatizo lako ni nini?

Mfano mtu hata akiamua kusheherekea kila mwaka mtoto wake anavyotoka darasa moja kwenda lingine, kuanzia chekechea, tatizo liko wapi?

Kuna sheria kavunja?

Katumia pesa yako?

Katumia pesa ya umma?

Kwa nini unapata tabu sana mtu baki akiamua kufurahia maisha kwa njia anayojua yeye?

Kitu gani kinachokushughulisha hapa?
 
Back
Top Bottom