Hivi mtoto kumaliza darasa la Saba ni kitu cha kuandalia sherehe?

Hivi mtoto kumaliza darasa la Saba ni kitu cha kuandalia sherehe?

Ni maisha yao ila kwangu mimi binafsi hapana. Nilikataa kufanya mahafali ya chuo familia nzima iliniona wa ajabu wakisema kama ni gharama si wanagharamia wao.

Niliwaambia hiyo gharama ya kutoka mkoa watu zaidi ya 10, chakula, malazi, usafiri na bado gharama za sherehe ni bora wanipe nifanye mtaji au wanunue kuku wafuge huko nyumbani kwa sababu n wastage of money ambazo kiuhalisia hazipo.
Hongera sana. Mimi nilifanyiwa party ya HBD na dada yangu akaalikana marafiki zake zawadi nikapata kama 800k japo alini suprise ila nilimwambia dada Ahsantye sana ila mimi sipendi sherehe hizi sioni umuhimu wake
 
Fimbo mbili tu zilitosha kufanya nikatae shule.
I'll baridi ya Njombe, Sasa piga kwa miaka Saba

Acheni washerekee
 
Hongera sana. Mimi nilifanyiwa party ya HBD na dada yangu akaalikana marafiki zake zawadi nikapata kama 800k japo alini suprise ila nilimwambia dada Ahsantye sana ila mimi sipendi sherehe hizi sioni umuhimu wake
Binafsi huwa sipendi sherehe, nakumbuka anko wangu alinipa kitambaa kikubwa sana cha kushona suti nilivyomaliza form 4, hadi leo kipo na nakumbuka sana ila yale makadi waliyotoa wadau sikumbuki hata rangi yake.
 
Issue ni kwenye malezi hao watoto unao wafanyia party za kila aina siku ukiishiwa watajua huwapendi milladayo ameripoti matukio ya watoto kujinyonga na kunytwa sumu kisa hawajafanyiwa sherehe za ubatizo na za kuzaliwa.

Elewa kabisa mtoto umleavyo ndivyo akuavyo unapofanya hivyo mtoto anaweka kama sheria kuwa kwa kila tukio zuri lazima umfanyie sherehe ukiacha anajenga chuki huku akinishinikizwa na mama yake hasa hawa wa 2000.

Ujue kufurahia maisha siyo lazima nifanye sherehe kwa kila tukio la hasha!

Mimi hapa ninaposema kuna mtoto wa dada alimwambia mama (bibi yake) mimi Anko p namchukia sana akaulizwa kwa nini eti sijawahi mpa zawadi siku ya Happybirthday yake wala kumtakia heri!! Je hii ni sawa mtoto kujenga chuki kisa tu hujampa zawadi?
Uko sahihi
Mtoto asilelelewe kama kidonda ila akikosea mpe adhabu akifanya vizuri mpongeze
 
Siyo Kusini. Waafrika wengi tunapenda sherehe
Uzi ufungwe,hiyo mtoto kumaliza la 7 ni sababu tu au kisingizio tu ila wana sababu nyingi sana kwa mfano mtu akizaa mtoto baada ya siku 40 wanaweka sherehe hata kama huyo mtoto hana baba wa kueleweka wao wanasheherekea tu bila kuwaza huyo mtoto mbeleni ataishi maisha gani
 
Uko sahihi
Mtoto asilelelewe kama kidonda ila akikosea mpe adhabu akifanya vizuri mpongeze
Malezi tuliyo lelewa sisi ni mazuri sana. Yaani sioni kama nisipofanya party yoyote nitapungukiwa leo hii unaweza kuachwa na girl friend wako kisa hujampa hela ya kufanyia party yake kama huna wewe kakope tu au uza simu yako ndo akuelewe.

Mimi nimesoma la kwanza hadi form4 sikuwahi kuona wala kusikia leo kuna birthday ya fulani. Baada ya kwenda chuo sasa daaah nikajiona kumbe sisi ni watu wa zama za kati kabisa huko
 
Malezi tuliyo lelewa sisi ni mazuri sana. Yaani sioni kama nisipofanya party yoyote nitapungukiwa leo hii unaweza kuachwa na girl friend wako kisa hujampa hela ya kufanyia party yake kama huna wewe kakope tu au uza simu yako ndo akuelewe.

Mimi nimesoma la kwanza hadi form4 sikuwahi kuona wala kusikia leo kuna birthday ya fulani. Baada ya kwenda chuo sasa daaah nikajiona kumbe sisi ni watu wa zama za kati kabisa huko
Hatari sana

Ila kama girlfriend wako anakufanyia party hakuna ubaya kumfanyia pia.
Tofauti na hivyo ni uzwazwa
 
Chanzo cha hizo sherehe ni vikundi vya huku mtaani hasa wakina mama wanachangiana katika sherehe.

Unakuta mtu kachangia sana katika sherehe za wenzake mixer kutoa zawadi hivi unadhani na yeye akipata sababu kwanini asifanye sherehe kurudisha pesa zake.

Tena bora hao wa sherehe za kumaliza darasa la saba nowdays huku uswazi wanachangishana hadi arobaini ya kumtoa mtoto, birthday, ubatizo na vipaimara wakati zamani ilikuwa ni sherehe ndogo za kifamilia zaidi.
Wewe ndio unaelewa mkuu. Hizo sherehe zinazoitwa shughuli nyingi ni biashara tu

Unakuta shangazu anachangia za wenzie sana kwa hiyo yupo radhi hata akasimamie shughuli ya mtu kwa kujifanya "mama wa hiyari" Ili mitunzo yake irudi. Sasa akipata darasa la saba, birthday, kipaimara anapata gap

Wengine wakikosakosa wanaandaa usiku wa chai, siku ya vyombo, sherehe ya taraka etc 😁😁😁😁 uswazi 🙌🏾🙌🏾🙌🏾🙌🏾🙌🏾
 
Yeah hakuna tatizo kabisa 1 mpaka 7 ni safari ndefu sana , hivyo wakisheherekea hakuna tatizo kabisa.
...Halafu anafeli !...Kumalizia STD VII iwe Jambo la Kawaida TU Sio la Kufanyia Sherehe ya kukodi Muziki'.
Tusubiri Akimaliza Form Iv, angalau anajua kinachoendelea ...tofauti na Sasa ambapo darasa la Saba anamilza na Miaka 12 !!! 🤔
 
Sioni shida kama familia ikifanya sherehe kwa mtoto wao kumaliza darasa la saba kwa sababu sio haramu, haimdhuru mtu. In fact watu wanaenjoy so hamna cha kuchekesha wala sio tatizo hata kidogo kusherehekea mtu kumaliza darasa la saba

Duh ndo Ukope sasa kumfanyia sherehe mtoto?
 
...Halafu anafeli !...Kumalizia STD VII iwe Jambo la Kawaida TU Sio la Kufanyia Sherehe ya kukodi Muziki'.
Tusubiri Akimaliza Form Iv, angalau anajua kinachoendelea ...tofauti na Sasa ambapo darasa la Saba anamilza na Miaka 12 !!! 🤔
Hiyo fanya kwako mkuu, tuheshimu maamuzi ya wengine.
 
Bora afanye hiyo Sherehe kwa kutumia ela zake. Unakuta mtu anataka mchango kabisa.
Mimi kuna ndugu yangu aliniomba nimchangie sherehe ya mwanae anamaliza la saba nkamwambia sikupi ela ya Sherehe hata cent ila ntamnunulia mwanao vitu vya shule akianza form1.
 
Unachangia sherehe za wenzako mpaka unakua mzee unastaafu unasema watakuja kukuchangia kwenye harusi za wanao. Watoto wanakua unakuta kuoa shida kuolewa shida. Watu wanagonga miaka 40 hawajaoa wala kuolewa kawaida nowdays ile michango yako inakua imeenda bure mzazi inamuuma balaa hasa wakinamama. Bora mnaenda mnamalizana na visherehe vidogo vidogo Kipaimara, Birthday, Graduation la7 form 4 na chuo akifanikiwa na Ndoa amen..
 
Kusini kunachekesha Sana yaani siku ya mahafali ya shule ya msingi mzazi anakwenda kukopa hela kabisa ili afanye shughuli nyumbani karibia mziki wa kukodi laki tatu chakula laki mbili eti kusherehekea mtoto kamaliza la Saba kweli jamani elimu ya msingi ni kitu cha kujivunia hivyo?
Kama kujenga barabara serekali inaweka sherehe kulipa wasaanii unadhani raia wakè inawaandaa je ?
 
Ndo mpaka ukodi mziki mkubwa?kwanini isiwe ya kifamilia tu
Wazaramooo mpa mtu anamaliza DRIVING SCHOOL COURSE.

Wana changisha fedha za kufanya sherehe ya kuhitimu driving school course 🤣🤣😂😂🤣

Ukisikia kuwa uyaonee sio maghorofa ndio hii...
 
Kwa miaka ya leo kuna vikundi vya kusaidiana kwenye maafa na sherehe, ukijifanya darasa la saba kwako unazingua wenzako wanawafanyia watoto wao hadi chekechea na wewe kama mwanakikundi unaambiwa ukachangie ni lazima
Kitendo cha mtu kujiunga tu na kikundi ambacho wanajadili michango ya sherehe ya chekechea inaonyesha uduni wa maisha waliyonayo mpaka wanajadili vitu petty.
 
Back
Top Bottom