Hivi mtoto kumaliza darasa la Saba ni kitu cha kuandalia sherehe?

Yeah hakuna tatizo kabisa 1 mpaka 7 ni safari ndefu sana , hivyo wakisheherekea hakuna tatizo kabisa.
Kakah sawa ni muhimu kufanya sherehe kama kumfariji mtoto ikiwa tu mna pesa ya kutosha.
Kama mbaka ukope pesa ndiyo ufanye sherehe umuhimu unapotea na kuwa matatizo ya kujitakia.
Then subiria wakati wa kulipa hizo pesa ndiyo utakuja kuona huo ubaya, mara kitanda kimeuzwa ili kurejesha mkopo.
Ni hvy tu mkuu.
 
Kaka usome Tena huu Uzi.
Mtuma Uzi amesema vyengine kabisa.
 
Umaskini una effects kubwa sana, usipokuwa makini unaweza chukia kuona mtu mwingine anavyotumia pesa zake ambazo wewe hazikuhusu hata kwa bahati mbaya.
 
Waache wajivunie wengine ndio mwisho wao wa safari ya elimu mkuu πŸ˜… wakitoka hapo ni kitaa
 
Haya ni maamuzi yao wafanye wanacho ona ni sahihi kwao
 
 
Huo ujinga ushakuwa kote sasa hivi.
 
Kumbe kusomesha mtoto imekuwa adhabu sasaπŸ˜‚
 
Kitu ambacho wengi hatukielewi ni kwamba times has changed.

Sahizi wanawake wengi ambao ndio wamekuwa wazazi wa hao watoto ni wale millenials i.e watoto waliozaliwa 2000's. During their childhood wamepitia same treatments. Ubatizo sherehe, Kipaimara sherehe, Graduations sherehe, Birthday sherehe.

How do you expect such kind of women raised in that manner to behave differently?
 
Kitu ambacho wengi hatukielewi ni kwamba times has changed.

Sahizi wanawake wengi ambao ndio wamekuwa wazazi wa hao watoto ni wale millenials i.e watoto waliozaliwa 2000's. During their childhood wamepitia same treatments. Ubatizo sherehe, Kipaimara sherehe, Graduations sherehe, Birthday sherehe.

How do you expect such kind of women raised in that manner to behave differently?
 
Wanawake millenials wamekuwa wabunifu sana wa sherehe na michango 😁!

Kabla hajazaa kuna "Bebi shawa" michango ipo.

Akishazaa "Birthday" kila mwaka na michango juu.

Akimaliza Chekechea, Primary, O-level, A-Level, Chuo kikuu "Graduation" nayo inaelekea kuwekewa michango.

Akitaka kuoa au kuolewa, michango na sherehe πŸ˜‚
 
Hahahah mkuu ata kindergarten wengine wanafanya.Huonagi kina mama Junior wanavyolia kwenye sherehe za kindergarten.
 
Yeah watu wa mjini wanasukuma siku kwa staili hiyo
 
Haya ndio maisha halisi sasa.
Yale mengine ni maisha ya maigizo ya kujifananisha na wazungu ila wanachosahau ni kwamba wazungu wanafanya kila kitu kwa mahesabu yaani kila kitu kipo kwenye bajeti. Wakati Bongo mtu anafosi kufanya sherehe na akaunti yake haina kitu na hata kodi ya nyumba anadaiwa halafu anaalika watu nje ya nyumba waje kuselebuka hii ni akili au matope.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…