Upo sahihi, sasa,
Kule kijijini kwetu watoto wawili wa familia moja, mapacha wa kiume, walipo maliza la saba, wazazi wao wakafariki! Mi naenda form one, wao ikashindikana, inabidi wasote kijijini, wauze mkaa, wapike gongo,nipo form two, wao wakaanza form one, wakapata mfadhili wakamaliza form 4,pesa ya kuendelea hakuna, wakauweka kijijini, waendelee na msisha mengine,elimu ikawa imeishia hapo, kule kijijini, kaya ni maskini Sana, hata majani ya chai ya dukani ni hanasa, mi nikaenda chuo, baada ya mwaka nikarudi kusalimia kijijini, nilivyowaona washikaji, nilisononeka Sana, wamechakaa, wameishaoa, wamekuwa wazee wa kijijini, asubuh kilimo, mchana kunywa gongo kidogo, deal ya kuingiza pesa, ama uchome mkaa, uvue samaki!
Namalizia shahada yangu, washikaji ndio kabisaa,wameishakubali matokeo, ni kufa maskini tu, wana vitoto,makalio yapo nje, wakati huo Mimi, Nina CPA yangu, salary six figure!
Sasa kijana kama huyo, akiendesha boda kutafuta fedha, usimdharau, you have know idea what people go through!
Unaowaona mjini, wanapiga boda, kuuza umachinga, sio kwamba unawazidi akili, au ni wajinga, ni maisha tu, wengine tupo tulipo,sio kwa akili zetu, akili zilichsngia, Ila nature/Mungu Ali manipulate circumstances, tukaweza kufika hapa.