Hivi Mungu aliwaza nini mpaka akaamua kututupia Ibilisi duniani!

Tatizo lako hujui hata unacho simamia nilisha kwambia mara kadhaa ikiwa huamini uwepo wa Mungu sio tatizo langu, kwa nini kuamini kwangu liwe tatizo lako?

Whether ni hadithi za kutungwa nitashukuru sana ukileta ushahidi usiotia shaka.... kuliko assumption zako za kila siku
... ambazo ni za kufikirika... ukishindwa kuthibitisha utungwaji wa hizo hadithi heshimu imani yangu.

Ujinga wa watu aina yako wanaamini wanachowaza lakini hawaji na uthibitisho wa dhahania zao...

Maisha ya wote waliongelewa kwenye bible na matendo waliyofanya ni uthibitisho tosha kwangu kwa uwepo wa Mungu wangu.
 

We
We
Jamaa
Yaani
Bible ya kina Constantine Ndio chanzo Cha uthibitisho juu ya Mungu Elohim ambaye unadai ndie Mungu wako wakati ndie Moja wa miungu wa Sumerians?
 
Kwanza kabisa, sijadili imani, najadili ukweli.

Natambua haki yako ya kuamini chochote unachotaka, cha uongo au ukweli.

Mimi sijadili imani, natafuta ukweli uko wapi.

Imani si kitu muhimu kwangu, kwa sababu kila mtu anaweza kuamini anavyotaka. Wengi wanaamini tofauti, vitu vinavyopingana.Hivyo kwangu sioni kama imani tu ni njia nzuri ya kunipeleka kwenye ukweli.

Ukweli ni kitu kinachosimama vilevile bila kujali imani yako.

Umeandika wewe hujali mimi kutoamini, sasa kwa nini unajibizana nami?
 
Alieanza kuhoji kati yetu kwa mwenzie ni yupi? Ndio maana nakwambia kama imani kwako sio muhimu hilo limatosha kutohoji chochote kuhusu imani yangu... imani ni kusadiki hata bila kushudia kwako hilo si muhimu.
 
Mmasai [emoji16][emoji16][emoji23][emoji23]
 
Kunyoa kipara ni mtindo wa kusuka nywele[emoji1787][emoji1787][emoji16][emoji16][emoji23][emoji16][emoji16][emoji1787]
 
Namzungumzia anayeitwa Mungu na watu wengi yule aliyemtoa mwanae wa pekee ili wewe ukombolewe
 
Namzungumzia anayeitwa Mungu na watu wengi yule aliyemtoa mwanae wa pekee ili wewe ukombolewe
Hapana mkuu ninae mjua mimi hawezi kumtoa kafara mtoto wake pekee kwa maana hata huyo mtoto hana na kama unamzungumzia huyo mwenye mtoto bado unazungumzia wa movie tu.
Zungumzia Mungu ambaye anasifa ya Mungu na sio mungu mmoja kati ya miungu.
 
Ibilisi na Mungu ni mambo ya imani. Imani ni hakika ya mambo yasiyoonekana. Sasa kutaka mtu athibitishe mambo yasiyoonekana sidhani kama ni sahihi na kama akiweza basi hiyo siyo imani tena
Ahsante kwa jibu ndugu, mimi huo ujumbe ulioni-quote nilikuwa natania tu, ndo maana nimeandika naomba nipuuzwe
 
mung mungu hampi mja mitihan nje ya uwezo wake
 
alafu siku ya kiama unapigwa moto na uyo ibilisi,wengine hatumjui hata anafananaje.kwa kweli hao kina adam angemalizana nao uko eden sio kutuuzia kesi yao ambao hatukuepo
Hamna kiama wala nini maana mimi kama mimi unipambanishe na Ibilisi kama sio uonezi ni nini?kifupi kila nikifikiria naona kabisa hiyo adhabu ya moto ni sound hakuna binadamu wa kumshinda hyu mbwa ibilisi ni noma
 
Kwani hii story kuna anayeamini ni ya kweli? Tuanzie hapo.
 
Alieanza kuhoji kati yetu kwa mwenzie ni yupi? Ndio maana nakwambia kama imani kwako sio muhimu hilo limatosha kutohoji chochote kuhusu imani yangu... imani ni kusadiki hata bila kushudia kwako hilo si muhimu.
Sihoji imani, nahoji ukweli uko wapi.

Kimantiki, Mungu hayupo.

Kwa sababu, dhana ya kuwepo kwake ina contradiction inayoonesha Mungu hayupo.

Huo ndiyo ukweli.

Kwenye imani sitaki kukuingilia kwenye imani yako.

Imani si lazima ifuate ukweli.

Unaruhusiwa kuamini hata uongo.
 
Watu wanafurahisha sana mida mingine, mtu kakurupuka huko kaja na mifano isiyo na kichwa wala miguu; “kunyoa kipara ni moja ya mtindo wa kusuka nywele? “ hii ni nini sasa lmfao? kipara huwa kinanyolewa? pia, kipara na kusuka wapi na wapi?. Hii ndo changamoto ya kukurupuka kwenye kufikiri, kwa hicho kibonzo kwa upeo wake aliona ni hoja, pia kwa asiyekuwa na uelewa wa kuchanganua mambo katika dimension zote anaweza akaona jamaa ameweka jiwe pale, lakini kwa wanaouelewa mchezo wangeuliza kwa nini asingeandika “kipara ni moja ya mtindo wa kunyoa nywele?”, hivyo tu imejitosheleza. Najua shabaha yake ilikuwa kuandika swali lenye mkinzano wa kimaana, kama ni hivyo alitakiwa aandike “kipara ni moja ya mtindo wa kusuka nywele?” na si hivyo alivyoandika – huo ni ufahamu mbovu. I NEVER ABANDON MY WEAK STUDENT

Hakuishia hapo akatoa na mfano wa pili wa “MAMA wa miaka 30 na MTOTO wa miezi 6” akieleza kwamba ukiambiwa “mtoto wa miezi 6 ndiye aliyemzaa mama wa miaka 30”, huu mfano kwenye LOGIC ni ABSURDITY - ni uongo, haiwezekani, sababu unapingana na BASIC LAW OF LOGIC ambayo ni LAW OF CONTRADICTION au NON CONTRADICTION, Hilo ni sahihi na mimi naunga hoja

Cha ajabu, huo huo mfano kwa mujibu wa nadharia ambayo yeye anaisadikisha - anaiamini ya CAUSALITY IN QUANTUM PHYSICS hilo jambo lipo - ni sahihi, nadharia inalazimisha kulielezea hivyo. CAUSALITY IN QUANTUM PHYSICS inasema “effect precipitates the cause in loop or cycles” au “effect happen before the cause in infinite quantum loop or cycles”. Tafsiri yake kwa lugha ya kiswahili ni kwamba “MATOKEO hujiri/huwepo/hutokea kabla ya (V/K)ISABABISHI kwenye tabaka la mzunguko lisilo na mwanzo wala mwisho”. Kwa maana hiyo ni kwamba kwenye infinite quantum loop “MTOTO hutokea kabla ya MZAZI”, mimi nauliza je ni sawa? ni sahihi? inawezekanaje?. Yaani “uwepo wako “mtoto” utangulie uwepo wa wazazi wako?” = “mtoto uzaliwe kabla ya wazazi wako” huo ni uongo, haiwezekani, ni lazima visababishi viwepo/vitangulie kabla ya matokeo, au walau basi wangeleta “assumption” kwamba cause ‘visabanishi' viwe simultaneous na matokeo ‘effect' lakini visababishi ‘cause' viwe superior/greater/faster kuliko matokeo ‘effect', la sivyo wazazi na mtoto watakuwa na umri mmoja hahahaha

NB: Wanaosoma huu uzi naomba watafute uzi wenye mada: wanaopinga uwepo wa MUNGU ni wakaidi 2 ndo utanielewa vizuri

Uzi wa wasioamini uwepo wa MUNGU ni wakaidi 2 nilimwambia kwa kuwa anaamini uwepo wa “INFINITE QUANTUM LOOP” basi atuthibitishie, hakufanya hivyo – na nina confidence interval 100% kwamba hawezi kuthibitisha hilo na cha ajabu anaamini uwepo wake, lakini likija suala la uwepo wa MUNGU hata akithibitishiwa convincingly kwa inference – empiricism – rationale – noumenal – phenomenal hataki kuamini, Sasa hii ni nini?[/B]
 
Imani inahusu mambo yaliyo nje ya uwezo wa akili za binadamu kuyaelewa au ku "comprehend"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…