Hivi Mungu wenu bado yupo au amekufa? Au zile zilikuwa hadithi tu za vitabuni?

Hivi Mungu wenu bado yupo au amekufa? Au zile zilikuwa hadithi tu za vitabuni?

Mto Songwe

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2023
Posts
6,683
Reaction score
14,060
Ujue siwaelewi.

Nashindwa kuelewa mpaka sasa huyo Mungu anayepata sifa kede kede katika hivyo vitabu vyenu Biblia na Quran mpaka sasa hizo sifa zake ameshindwa kuzionesha kwa wafuasi wake.

Angalia wafuasi wake pale Palestine wapo tayari kwa nguvu zao kulinda ule msikiti usitwaliwe na waisrael lakini Mungu wao mpaka sasa kashindwa kabisa kuwalinda wao dhidi ya makombora ya waisrael.

Hivi umewahi kuona video za watoto wa kipalestine wanao kufa kila siku tuchukulie mfano video za juzi juzi tu hapa ambazo kambi ya wakimbizi imeripuliwa huko Rafah na watoto wa kipalestine wamechomwa moto inasikitisha sana lakini huyo Mungu wao ambao wao wapalestine mpaka huwa wanapigana na askari wa waisrael kuhusu msikiti wa Al Aqsa wanapo zuiliwa kusali na wapo tayari kuulinda huo msikiti dhidi ya Israel lakini huyo Mungu hata kuwalinda wao dhidi ya uharamia wa Israel kashindwa kabisa.

Zile sifa kede kede mnazompa kwenye Quran ni hadithi tu za kijifurahisha za uongo ? Au huyo Mungu kafa ? Hayupo ? Au amewachoka hataki kuwasikiliza wafuasi wake ?

Tuje hapo Sudan, tuende somalia hali ni ile ile ni kushindwa kwa huyo Mungu anaye abuduiwa na kupewa sifa kede kede mara oooh ni muweza wa yote mpaka sasa kuwalinda watu wake dhidi ya uharamia kashindwa kabisa.

Sasa huyo Mungu kazi yake nini ? Kama tu zile zinazo elezewa kwenye hivyo vitabu mpaka leo hakuna anacho thibitisha kama anaweza kufanya au kuna mahali naye kajificha kazidiwa nguvu na watu wa duniani wa sasa tofauti na hao wa kale ambapo aliweza ?

Hawa wayahudi nao Mungu wao anapewa rundo la sifa mara ooh Samson pekee aliua wafilisti kwa uwezo wa Mungu, mara oooh Mussa alipasua bahari kwa uwezo wa Mungu sifa nyingi lakini huyo Mungu alishindwa kabisa kuwaokoa dhidi ya uharamia wa Hitler mpaka unajiuliza wakati Hitler anafanya anayo yafanya huyo Mungu alikuwa amelala miaka yote ?

Leo hii wanajilinda kwa mamifumo ya ulinzi ya kutisha na makombora ya kutisha sioni yule Mungu wao akiwalinda kwa miujiza yake kama anavyopewa sifa kwenye vitabu vyao.

Juzi tu hapo walipigwa ambush na Hamas huyo Mungu wao kuwalinda alikuwa wapi ?

Tuje Congo hawa wakatoliki wa Congo nao wanachinjana na kuchinjwa kila siku, wacongo huwezi waambia kitu kuhusu Mungu wao kupitia katoliki lakini mpaka leo wanategemea askari toka Tanzania waende wakawalinde kwa nini huyo Mungu wao asioneshe miujiza yake sasa ? Anasubiri nini na lini ?

Huko Ukraine wale wa orthodox nao Mungu wao kashindwa kuwalinda kabisa hata kuwapatanisha na wa orthodox wenzao warusi hakuna muujiza wowote alio fanya zaidi tu ya waukraine kuendelea kufa kila siku na kufanyiwa uharamia na Warusi.

Tunaambiwa huyo Mungu kupitia jiwe tu Daudi alimuua Goliath lakini leo hii mawe yameshindwa kuwalinda wapalestine kuzuia vifaru vya waisrael vinavyo waangamiza na kupora maeneo yao kila siku.

"Mungu wa upendo na huruma" inafikirisha sana.

HUYO MUNGU TUNAEAMBIWA WA HURUMA NA UPENDO YUPO WAPI ?

MBONA KIMYA WAFUASI WAKE WANAZIDI KUANGAMIZWA KILA SIKU AU MIUJIZA IMEISHA ?
 
20240408_180045.jpg
 
Kwenye Biblia ukisoma Agano Jipya na Agano la Kale kuna maangamizi ya kufa MTU kwa HIO sio Jambo Jipya hata KIDOGO
Kwa hiyo yeye anafurahia watoto kuendelea kuuawa hovyo hovyo ?
 
Kwa hiyo una maanisha sio muweza wa yote ?
Amekupa uhuru wa kuchangua, kufanya na kuamua lolote unalo taka.

Yeye yupo, anatizama na ukikwama ni mwepesi wa kukusaidia endapo utaomba msaada wake.
 
acheni kumsimanga Mungu wetu,,mbona nyie hivyo mnavyoviamini kua vipo hatuvisimangi!?Mungu yupo na ataendelea kuwepo.
 
Hata firauni aliua sana lakini wakati wa Mungu ulipofika hakutoboa kabisa aliangamia na utawala wake. Mungu anafanya kazi zake kwa Wakati hakurupuki kama wewe. Sifa ya binadamu ni pupa Allah ameshakadiria kila kitu na idadi ya watakao poteza usiwe na haraka ndugu yangu
 
Uzi mzuri fikirishi, ndio maana kundi la "atheists " likaibuka ulimwenguni. Kulingana na akili yangu japo wafia dini wataniita mpumbavu, kama Mungu yupo, amejigawa sehemu mbili, ushetani na umungu. Maafa ndiye anaeruhusu, akiona vipi analeta neema.
 
Yupo kwenye nini ? Wafuasi wake wanaendelea kushughulikiwa au naye anafurahia wanayotendewa ?
watu wake wanashughulikiwa na watu kama wewe apo,,na wala hafurahii ila subirini zamu yenu.
 
Hata firauni aliua sana lakini wakati wa Mungu ulipofika hakutoboa kabisa aliangamia na utawala wake. Mungu anafanya kazi zake kwa Wakati hakurupuki kama wewe. Sifa ya binadamu ni pupa Allah ameshakadiria kila kitu na idadi ya watakao poteza usiwe na haraka ndugu yangu
Hakurupuki kama mimi sawa.

Kwa hiyo anatoa kafara watoto anao waumba kila siku kwa faida ya nini sasa ?
 
Sisi tunaoamini na kujua kwamba Mungu yupo tunajua pia kwamba ana hekima na njia na sababu katika kila jambo limtokealo mwanadamu.

Kwa sababu hawezi kuwa Mungu bila kuwa na maelezo mantikifu ya kila kitu, au siyo?

Mungu huyaelekeza mambo yote ili yawafaidie wale wampendao (Warumi 8:28).

Tatizo linaanzia tu pale mwanadamu anapotaka kucheza kwenye nafasi ya Mungu.

Nadhani kila mmoja acheze kwenye nafasi husika kadiri ya uwezo na hekima aliyo nayo.

Imani yangu thabiti kwamba Mungu yupo ni jawabu la majawabu ya maswali yote magumu na mepesi.

Ukiamini kwamba Mungu yupo, maisha yanakuwa rahisi mno na yenye maana sana.
 
Back
Top Bottom