Hivi Mungu wenu bado yupo au amekufa? Au zile zilikuwa hadithi tu za vitabuni?

Mungu hayupo mkuu.

Hizo habari za Mungu kuwapo ni stories walizotunga watu waliokuwa wanapambana na hali zao tu.

Mungu angekuwapo hata huu mjadala kama Mungu yupo au haupo usingewezakana kuwepo.
 
Thibitisha hayo uliyo andika
Mungu hayupo mkuu.

Hizo habari za Mungu kuwapo ni stories walizotunga watu waliokuwa wanapambana na hali zao tu.

Mungu angekuwapo hata huu mjadala kama Mungu yupo au haupo usingewezakana kuwepo.
 
Suala ni kwanini anashindwa kulinda wafuasi wake licha ya sifa kede kede anazopewa na hao wafuasi wake
 
Hayupo kiongozi kwa nani alisema yupo?kumbuka unaelezwa hivi ..your ways aren't my ways.. says the Lord

Kila jambo hutokea kwa sababu kuwa na subra utajua.Atakama ni nature lazima kuna kitu kama cause-effect relationship.So kabla ya kupata majibu sahihi jiulize nini chanzo cha haya yote uliyosema hapa afu ndio utajua who is to intervene
 
Thibitisha hayo uliyo andika

Kwanza kabisa.

Kimantiki.

Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote kuumba ulimwengu unaowezekana kuwa na mabaya ni contradiction.

Mungu huyo, kwa sifa zake hizo, hawi pamoja na ulimwengu unaoruhusu mabaya.

The two are mutually exclusive.

Ama Mungu huyo yupo na ulimwengu unaoruhusu mabaya haupo.

Ama, ulimwengu unaoruhusu mabaya upo, na Mungu huyo hayupo.

Ulimwengu unaoruhusu mabaya upo.

Hivyo.

Mungu huyo hayupo.
 
Suala ni kwanini anashindwa kulinda wafuasi wake licha ya sifa kede kede anazopewa na hao wafuasi wake
Mkuu, define ^kushindwa!^

Utagundua mwenyewe kwamba hiyo ni istilahi sahabi na tushisi (relative and subjective term).

Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote kuumba ulimwengu unaowezekana kuwa na mabaya ni contradiction.

Mungu huyo, kwa sifa zake hizo, hawi pamoja na ulimwengu unaoruhusu mabaya.
Hizi sifa za Mungu umezipata wapi? Ningependa sana kujua chanzo cha taarifa zako hizi.

Nikijua chanzo chako ulikopata hizo habari, bila shaka nitakusaidia utoke kwenye mkwamo wako wa kifikra.
 
Huwezi kumpangia Mungu ratiba yake

Wakati wake bado

Maisha ya hapa duniani ni kama movie, sasa hivi kubwa la maadui Shetani anatamba ndio maana unaona mambo ya hovyo mengi sio vita tu hata maadili

Movie inapoelekea mwishoni wakati wa Mungu wa kumuua kubwa la maadui utafika na hapo ndiyo itakuwa mwisho wa yote uliyosema
 
Tunaambiwa yeye ndie mjuzi wa hatma ya kila alie muumba. Anajua utakufa vipi toka unazaliwa. Sasa kama alishapanga utakufa vipi inakuwaje anae kuua apate dhambi? Kama anajua kwa mfano Palestinians watakufa kwa kupigwa makombora na Israelis how come Israelis waandikiwe dhambi kwa kutekeleza kila ambacha muumba alishakipanga kwa Palestinians? Au kama tayari alijua some Jews watakufa kwa kuangamizwa kwa sumu na Hitler, iweje Hitler aandikiwe dhambi kwa kutelekeza kitu ambacho tayari yeye muumba alishakipanga.
 
Kila kitu kipo katika mlolongo......
Usiache kufanya haqi kisa kuna batwili. Mungu wetu ni mmoja na akilihukumia jambo uliambia "kua kisha linakua"
 
Imani za kidini zimebaki kwa watu wenye mioyo miepesi ya kudanganyika ila sisi tuliojua ukweli kuwa DINI ni mifumo tu ya maisha ya kundi fulani TUMESHA LEFT GROUP kitambo.AASAAANTEEEE
 
Siwezi kuwasemea hao wenzangu ila Mungu wetu ambae ni Mungu wa Israel anayo nguvu sana na ndio maana wewe mwenyewe unaona kazi zake mchana na usiku.

Angalia Israel yenyewe utaelewe ninachosema,

Jina na Yesu linatenda kazi kulingana na imani uliyonayo sio historia.
 
Hakunaga kiumbe kinachoitwa mungu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…