Hivi Mungu wenu bado yupo au amekufa? Au zile zilikuwa hadithi tu za vitabuni?

Mungu hayupo mkuu.

Hizo habari za Mungu kuwapo ni stories walizotunga watu waliokuwa wanapambana na hali zao tu.

Mungu angekuwapo hata huu mjadala kama Mungu yupo au haupo usingewezakana kuwepo.
Kwanini?
 
Watu wakiacha mihemko watakujibu Maswali yako.

Kwamba mtu mfiraji. Mtesaji, muuaji na mwizi wa mali za umma anaiba kila siku na kufunga watu kwa kubambikia kesi.

Atakuja kusamehewa huku Mwizi wa Kuku wa jirani ataungua moto. Mtu mwovu anazidi kupanda vyeo na kutajirika kuliko Maskini Mwongofu?

Mungu mweza wa yote huku Njaa, vifo, maradhi na mauwaji vimetamalaki?

Mungu ni Neno, anashindwa kutamka neno Moja tu ili.
uharibifu duniani ukome? Au anafurahia tunayopitia? Kwa nini asiyazuia na kutoipa nafasi kabisa Dhambi? Kwani haiwezekani?

Au anafurahi tukiingia dhambini ili aje atuchome moto?
 
Kumbuka mungu katika biblia anaitwa amiri jeshi kuu na ni mungu wa vita na mungu anapenda vita kuliko kitu chochote wanachofanya israel zidi ya makafiri watu wasiomjua yesu wapo sawa mungu ni wavita naam..
 
Amekupa uhuru wa kuchangua, kufanya na kuamua lolote unalo taka.

Yeye yupo, anatizama na ukikwama ni mwepesi wa kukusaidia endapo utaomba msaada wake.
Kuna mbaya ambayo hayasababishwi na watu,

Mabaya kama matetemeko na mafuriko hayasababishwi na watu,

Inawezekana vipi Mungu huyu na sifa zake zote hizo zisimuliwavyo akaumba ulimwengu ambao unaruhusu mabaya!?
 
MOLA MLEZI YUPO HAI TOKEA ENZI NA HATA MILELE, HIKI KINACHO TOKEA LEO NA KESHO IMEANDIKWA KATIKA VITABU TUKUFU VYA QURAN NA BIBLIA, HIZI NI ZILE ISHARA YA NYAKATI ZA MWISHO,

MATAIFA KUPIGANA
FALME KWA FALME KUPIGANA
NDOA ZA JINSIA MOJA
MITUME, WACHUNGAJI, MANABII WAUONGO,
VITA KILA KONA YA DUNIA,
WATU KUUANA PASIPO SABABU YA MSINGI , NA KADHALIKA...
 
Hawa watu wanaoamini umasikini wao ni mpango wa Mungu kamwe hawatakuelewa, watakuja na majibu mepesi utasikia Mungu hapangiwi au wakati wa Mungu haujafika
 
Inafikirisha ukifikiri kwa wenye akiki kitamu
 
Hizo "sifa kede kede" unazosema zipo kwenye Qur'an, zipo wapi? Nukuu.
 
Kuna mbaya ambayo hayasababishwi na watu,

Mabaya kama matetemeko na mafuriko hayasababishwi na watu,

Inawezekana vipi Mungu huyu na sifa zake zote hizo zisimuliwavyo akaumba ulimwengu ambao unaruhusu mabaya!?
Matetemeko na vimbunga vikali, hizo zote ni ishara za uwepo wake, ishara za nguvu alizonazo. Pia Mungu anaweza kutumia matetemeko kama njia ya kutoa adhabu au kuonyesha kwamba anachukizwa na mabaya wafanyayo binadamu
 
Matetemeko na vimbunga vikali, hizo zote ni ishara za uwepo wake, ishara za nguvu alizonazo. Pia Mungu anaweza kutumia matetemeko kama njia ya kutoa adhabu au kuonyesha kwamba anachukizwa na mabaya wafanyayo binadamu
Kumbe hukumu ni hapa hapa duniani siyo!
 
Mungu ni jana leo nahata milele.. alikuepo yupo na atazidi kuwepo

Cc Smart911
Yeah. Safi mkuu; na Ieleweke kwamba kutokuamini au kuamini uwepo wake Mungu, hakumpunguzii chochote, Hakumuongezei chochote na wala hakumnufaishi kwa namna yeyote ile. i.e. YEYE yupo bila wewe kuwepo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…