Hivi mwanaume anapata nini kwenye ndoa kiasi kwamba ajutie kutokuwa na ndoa. Je, ndoa kwa Dunia hii ni muhimu kuliko pesa

Hivi mwanaume anapata nini kwenye ndoa kiasi kwamba ajutie kutokuwa na ndoa. Je, ndoa kwa Dunia hii ni muhimu kuliko pesa

Nimekuwa nikijiuliza Nini cha maana mwanaume anapata kwenye ndoa, kiasi kwamba ajutie anapokuwa hana ndoa. Siungani na wale wa kataa ndoa, ila najiuliza tu Nini kinapotea kama haupo kwenye ndoa. Kwa wanaume, una pesa, una watoto.

Mwanamke akiwa kwenye ndoa anapata faida hizi .
1. Usalama wa kijamii na kifedha.
2. Furaha nk ,

Najiuliza Sana sababu wanaume wenye pesa na hawana ndoa naona kama wapo happy Sana na afya zao zipo SAWA sana .............

Kuna watu maarufu mitaani wenye pesa na hawana ndoa, mfano mchukue Mbowe, Aliko Dangote, Diamond Platnum, Myika Nk na wengine wengi wenye pesa na hawana ndoa, vipi wenye wanonekana kutetereka kwa kuikosa ndoa.

Mchukulie Sugu ameoa akiwa na almost 40 hivi kuna kitu anaweza kuwa anajutia sawa na Gerald Amos yule mwimba kwanya pale kanisani kwenu aliyeoa akiwa na miaka 20 na anaishi kwenye nyumba ya kupanga, hawezi panga mlo wa wiki, watoto wapo Kayumba school, ada, nguo vinamtesa
Faaaaact
 
Ndoa inaleta heshima, furaha, malezi mazuri ya watoto, uhakika wa papuchi, usaidizi katika maendeleo nk


NB
Hayo yote Kwa sasa yanakosekana Kwa asilimia kubwa na ndio maana watu wanaona ndoa hazina maana na ndio sababu hadi imekimufanya uulize Hilo swali
Umenena vyema mkuu, mwanaume ukipata heshima, uhakika wa tendo, furaha, amani n.k utakuwa na furaha ktk maisha yako yote.

Sasa siku hizi ktk mahitaji 7 ya ndoa kwa mwanaume, basi utapata uhakika 2 au 3 tu.
 
Ni lini pesa imekuwa muhimu kuliko chochote ? Pesa ni kiwezeshi na Furaha ni State of Mind hata ukiwa na Pesa mlima kama haujapata your Heart Desires huwezi kuwa na Furaha....

Na ndoa ni utamaduni / way of life ambayo jamii imejiwekea huenda ndoa za kipindi kile sio kama ndoo za leo n.k. ila mtu anachohitaji ni intimacy, love and belonging, (na hayo anaweza kuyapata hata asipokuwa kwenye ndoa....

Kwahio furaha ya mtu ni mtu mwenyewe (kipi anakitaka na kama amekipata au hajakipata)... Na kuhusu needs nakupa Hierarchy of Needs ambazo ukizipata zote utakuwa na Peace of mind...

1712927787162.png
 
Kero ya ubachela hata kama una pesa ni;
1. kufua nguo (nguo alizofua mke tamu kuzivaa)
2. Kupika (chakula unashiba ukiwa unakula na mke,raha yake asikuambie mtu)
3. Tendo la ndoa (raha sana kungonoka na mke kuliko kuiba mke wa mtu au mpenzi wa kushare na wasaidizi wa matumizi)
4. Ushauri kutoka kwa mwenza wa ndoa (mpenzi atahitaji balance yako mtaitumia vipi kwenye bata lijalo)
5. Usaidizi kiuchumi (hawala ngumu sana kupambania ongezeko la mzunguko wa fedha katika ukoo wa Mwafilombe,anawaza muda wote akutoeje upepo )
Na mke wa hivi kumpata ni mtihani
 
Kuoa ni ukomavu wa akili kwa mwanaume.
Ni kweli wanawake ni pasua kichwa ila tambua sio kila tatizo hukimbiwa hasa tatizo ambalo ni wajibu. Kutatua tatizo ni sehem ya kujifunza.

Kuishi na watoto pekee haitoshi kwako na kwa watoto pia, wototo hujifunza mambo mengi kwa wazazi sasa kuwanyima upande mwingine wa somo uiue unawaanda kwa maisha ya upande mmoja (usiloliweza mwingine analiweza). Kama wewe umeshindwa Watoto wako kama ni wa kiume usifikiri na usiwaandae kushindwa
uliloshindwa, umeamua kuwanyima haki yao.

Jamii zetu nyingi za kiafrika kuoa ni jambo la heshima kubwa na kuaminika zaidi. Kama la familia litakushinda hata mengine yataweza kukushinda, japo si yote!
Hakuna asiyependa heshima labda mpumbavu tu, HESHIMA NI ZAIDI UMAARUFU.
Kuoa ni wajibu wa kila mwanaume anayejitambua.
Lakini ujue hao watoto ni wapitaji hapo hutakaanao maisha yako yote na usiwategemee kabisa. Kwa sasa wanakufariji ila kuna muda utafika utajutia maamuzi ya sasa na kutamani bora ungekuwa na mwenzi wa maisha, kwangu mimi maisha ya mume na mke ni matam sana pamoja na kero za wanawake ila hilo siwezi likimbia nitalikabili. OA.
Heshima gani hiyo ya mtu aliyeoa
 
Back
Top Bottom