Hivi ndivyo Hayati Magufuli aliharibu Uchumi wa Tanzania. Takwimu huwa hazidanganyi

Haikuteteleka kwa muktadha wa Covid 19 kama ni kufanya citing ya alichokizungumza Mama lakini in aggregate mtoa mada anatuambia ni horrible sasa leta nondo hapa kumpinga mleta mada kwa facts na sio farts.
Aje apinge kwa 'facts na si kwa farts'[emoji1], noted.
 
ni kweli ni mkapa pekee ndiye aliyeweza kukuza uchumi wa nchi hii hata kama watu walimlaumu vipi kwangu mimi mkapa ndo aliyekuwa mchapa kazi.Magufuli aliletwa na Mungu kuwanyoosha mafisadi sababu aliyaona mambo yote ya kishenzi yaliyofanyika huko nyuma wakati akiwa waziri.nchi ilikuwa ya wenye pesa,sheria zilikuwa hazifanyi kazi,uonevu ulipitiliza,wenye pesa walikuwa na uweza wa kufanya lolote na watoto wao ndo hao walioko humu JF wanaotukana au wanaomtukana JPM baada ya wazazi wao kunyooshwa kisawasawa na upuuzi huu unataka kuendelea ktk awamu hii.
 
Alianzisha miradi, na si lazima amalize yeye anayefuata anamaliza, siyo kwamba anayeanza na miradi lazima amalize, Magufuli alifanya kazi kipindi kimoja, na umona ongezeko la GDP, hilo ni muda mfupi sana Vs Kikwete na Mkapa. Kwenye percent kunaonyesha kuwa Vianzo vingi ambavyo vilikuza uchumi kipindi cha Kikwete (miaka kumi) na kipindi cha Pili (miaka 5) vingi vilianzhishwa na Mkapa. Vyazo vingi vilibaki vile vile hadi akaja Magu. Bomba la gesi la Mtwara Dar viliongeza GDP kwa kiasi kikubwa ingawa na miundo mbinu mingi ilisaidia kuongeza GDP ambayo ni routine.

Bwawa umeme utauzwa, maji yatauzwa, viwanda vikubwa itaanzishwa, wakekesaji wakubwa watakuja, efficiency itakua. Meli, Ndege, Train - mizigo itasafarishwa, watu watatumia kusafiri that is how GDB grows. Ukarabati wa Meli Vitctoria, Tanganyika, Nyasa ilikuwa siyo kazi ndogo. Makao makuu Dodoma yaliongeza ukuzaji wa uchum indirect kwa viwanda vya cememt na infrastructure, hata kama Samia ataongeza hizo 30% lakini hivyo ni vitu vinavyohitajika. Huwezi kuita investors wakati huna umeme, ndege, train au Barabara; waste of time.

Sukari unayongea itafikaje kwa mlaji bila ya umeme, Barabara, train, au ndege? Hapa siongei ushabiki kwa siasa; bali uchumi. Sukari, Mbolea, mafuta ya kula vyote hivyo bila ya umeme na infrastructure zingine ni bure, hakuna service.
 
Pole kwa kutambua hivyo. Naheshimu madai yako

Kuzindua na Kutokuwa na Senti wapi na wapi.

Unasomeka
 
Kuegemea kule Kwa hayati kwenye ishu gani?

Mengine uliyoandika ni hadithi,hoja ilikuwa ni Magufuli kufifisha Kasi ya ukuaji wa uchumi Kwa 32% tuu,hiyo effects ya Miradi ya awamu ya 5 itaonekana baada ya Kukamilika kwenye awamu ya Samia lakini inasakia kuwa ni juhudi za Rais maana amepokea miradi karibu yote Iko chini ya 30% na by 2025 yote itakuwa imekamilika labda itasalia Sgr tuu ..

Mwisho Kwa miaka 2 tuu ya Rais Samia kuifungua uchumi rekodi zifuatazo zimewekwa..

TPA imevunja rekodi ya kuhudia makasha na mapato Kwa 1Tilioni

Banks Kwa mara ya kwanza zimefikia faida ya 1T

Kampuni za Bima mara ya kwanza zimefikia faida ya 1T

Tanzania Kwa mara ya kwanza imeizidi Kenya na EAC yote kwenye mauzo ya Nje yaani tuna exports zaidi ya tunavyo import,

TRA Kwa mara ya kwanza inakusanya wastani wa til.2 Kwa mwezi kutoka 1.2 Til.

Kwa mara ya kwanza tumeanza kuzalisha mbolea yetu wenyewe,mwaka huu Tume import Kwa sababu kiwanda kimeanza mwezi wa 7 ila.mwakani hakuna mfuko hata mmja utatoka Nje na infact Kunyaland wameanza ku import kutoka Tanzania,Tunajenga kiwanda kingine Pwani na kampuni ya Morocco..

In facts tuna vingi vya kuonesha mambo ni mengi mda ni mchanche,
 
Eti Hayati Magufuli, shujaa wako au siyo
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Stupidity at it's highest level, yaani Denmark kuweka fedha za sherehe kwenye mifuko ya maendeleo 'wamemkopi' Jiwe. What exactly are you smoking? Hivi yule mwehu aliwarogo au ndiyo akili zenu zilivyo, unadhani civilized countries huwa yanatoka tu maamuzi ya kiongozi. Tanzania or rather uongozi wa Tanzania kwa '1st world' countries ni kama wewe hapo unavyoziona nchi za Tonga au Tuvalu au Fiji. Literally we don't exist in the world of politics, labda tukiwa kwenye vita ndiyo kwao inaweza kuwa habari kwao. Zaidi ya wasomi walio-specialize kwenye mambo ya Afrika hakuna watu wenye muda wala interests za mambo yenu huko third world.
 
Jiwe aliua kila kitu, napendekeza kaburi lake lichomwe moto
 
Mtu hayupo alishafariki lakini bado mna msakama,mnalipwa kiasi gani kutukana maiti?
 
Wala usijali hakuna mtu amesema lazima amalizie yeye ila Kasi ya ujenzi awamu ya 5 ilikuwa ndogo sababu serikali haikuwa na pesa tofauti na Sasa..

Sasa boss unaposema hakuna umeme nk uwe unaongea vitu vinavyoeleweka,Kila mtu Moja ya matatizo yaliyosababisha matatizo ya umeme mwaka Jana ni kukosa akili Kwa awamu ya 5,huwezi kuweka Nguvu kubwa kwenye mradi mmja ambao haujui utakamilika lini matokeo yake ukame ulivyopiga umeme ukasumbua..

Saizi mvua zimenyesha tumepata nafuu na imetoa nafasi Kwa Serikali kuongeza mitambo ya gas,Kwa Sasa hata ukame utokee hutosikia mgao maana wameingiza megawatt 200 Mpya za gas na nimemsikia Byabato akisema installed capacity Kwa Sasa ni megawatt 1900 na Kati ya hizo 70% ni gas.By 2024 Tanesco inasema itakuwa ni megawatt 6,000.

Kuhusu Barabara Hilo achana nalo Mzee,Barabara zinatandikwa Kila sehemu ya Nchi hii siwezi Anza kukupa orodha hapa wewe angalia Mkoa wako Kuna miradi au hakuna,Mimi Mkoa wangu Kuna miradi 2 ya Barabara kuu achilia mbali za Tarura.

Trains hazina impacts yeyete ya maana kwenye uchumi,tuna Tazara Iko vizuri kabisa Kuna nini Cha maana inasafirisha? Hivyo hivyo hata Sgr kwangu naita ni tembo mweupe ikikamilika serikali itachukua Kodi za watu kuiendesha kama inavyofanya kwenye mandege, upuuzi mtupu.
 
Mtu hayupo alishafariki lakini bado mna msakama,mnalipwa kiasi gani kutukana maiti?
Kufariki sio excuses,mlitaka tuache kumsakama muache kumuita shujaa wakati hakuwa na huo ushujaa na ndio maana tunawaonyesha
 
Vipi wale walioporwa mali/biashara zao, waliodhulumiwa, waliotekwa na kuteswa, walioshambuliwa kwa risasi na kujeruhiwa, waliobomolewa nyumba zao bila ya compensations, waliotukanwa na kukashifiwa baada ya kupata madhara na hasara kutokana na natural disasters na ndugu wa wale waliouawa au 'kupotezwa' hao hawapo humu janvini?
 
Na wakati bila ya Mwinyi kuwatengeneza raia kiuchumi toka kuvaa magunia,kula mlo mmoja hadi kufikia kumiliki biashara zao wenyewe,Mkapa angekusanya kodi toka wapi?.
 

Rais SSH amekiri mwenyewe, bila maamuzi magumu ya Hayat Raisi hapa tulipofika palikiwa kana ndoto!
Hayo yote yalikuwepo na ndio maana Hayat alikuwa akirudia rudia" nchi hii tunachezewa" alioana Uhalisia na yale yanayoripotiwa nje ni tofauti....mifano ni kama hiyo uliyotoa....alikuwa anjiuliza inakuwaje sisi ndie tuna Tanzanite alafu kenya ndie irepoti ndio expota wa kwanza?

Kubali tu mirija aliyofunga imeleta tija, ufanisi, unaonekana ingawaje upo uwezekano kuwa tunaweza hata kuwa maradufu ya hapo...."We are a Donor Country" sasa we chagua tafsiri yako mwenyewe, mie nachagua Joshua 24:15 tuna uwezo wa Kulisha Dunia nzima, hamtaki kukubali na mntaja kejeli hatuwezi, ila kubeza yake Hayati Raisi mtafanya kwa sababu huo uchumi mnaodai nyinyi ni wa wale waliofinywa. Period. Nenda Manzese uwaulize
 
Mpaka leo tuanze kuorodhesha miradi ya DR Samia ambayo itakwenda kwa wananchi moja kwa moja
1. Umeme kubadilisha waya wa umeme kwa trilion 4.1 kati ya huzo tunaanza tril 1.9

2.Gesi asilia kwa wawekezaji wa tril 70
3. Mradi wa kujengewa barabara na wawejezaji chalinze to Morogoro na haujaanza bado.
4.mradi wa kupeleka kivuko kenya kwa 7.5 bil kwa kuzinduliwa na sherehe ya mkataba
5.
Tarura kujenga barabara mpaka uwe na mheshimiwa mtaa huo.
6. Barabara kuu za mikoa kazi nzuri zinaendelea .
Ile tril 1.3 ya IMF Tuliona ilivyoiendesha nchi na kuchangamsha ujenzi wa mashule ,vituo vya afya,mabwenu,nyumba za waalimu ila huu mradi wa tril 70 sioni watu wakikimbilia ajira huko au ni wageni tu?
Tunapenda miradi ya wananchi wapate ajira sio miradi ya wananchi kubakia watazamaji.
Mwendo kasi nchi nzima vijana wamepata kazi.any way mimi sio mchumi lakini tunapenda miradi ambayo sio ya kiini macho.
 
Ripoti ya BOT ya October 2019 ilionesha jinsi anguko la mauzo ya korosho lilivyopunguza mapato Tanzania.

Na Magufuli ndiye aliyesababisha anguko hilo.
 
Mtu hayupo alishafariki lakini bado mna msakama,mnalipwa kiasi gani kutukana maiti?
Anasemwa na ataendelea kusemwa kwa maovu aliyofanya, anavuna alichopanda. Kama Hitler, Mussolini, John Vosta, Idd Amin and so many other dictators waliokufa miaka iliyopita bado wanasemwa na pia wametungiwa vitabu sasa kwa nini dictator Jiwe asisemwe eti kwa kuwa hayupo alishafariki. What's the difference kati yake na hao dictators wengine? Hili liwe fundisho kwa marais wengine wataokuja wawe wakijua ya kuwa matendo yao ndiyo yatawahukumu na ndiyo yatayo-determine jinsi watakavyokumbukwa.
 
Madai yangu na simama nayo one thousand percent

Usijitoe ufahamu, hizo kejeli zako hazinipunguzii taarifa wa maarifa niliyokuwa nayo. Jifunze kukubali....Usinilazimishe kukubali propaganda zenu hizo. Jibu hapa Denmark wamefanya hivyo au hawakufanya?

Kweli mna huzuni...Ungependa kuhudhuria mikutano ya kupunguza kero, yaani una lalalm kana kwamba hakuna cha kujifunza kutoka Afrika?

Aisee una hasira. Duh Basi jibu tu Denmark walifanya hivyo au hawakufanya?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…