Hivi Ndivyo Rais Samia Alivyopamba na Kutawala Magazeti Yote ya Leo

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Ndugu zangu Watanzania,

Baada ya hapo jana Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan kutema cheche na kutoa hotuba nzito ya karne na kihistoria na kuteka anga la kitaifa na kimataifa na kupongezwa kila kona ya Nchi yetu.

Hii leo Magazeti yamepambwa na kutawala na habari za Mheshimiwa Rais na hotuba yake nzito na ya kihistoria aliyoitoa hapo jana


Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Naona hata jamii forum ameipamba
 

Haya magazeti ni ya machawa wake ambayo kazi take kubwa ni 'kusifu na kuabudu.' Rais awe mwangalifu na sifa anazopewa kutoka kwa chawa wake.

Aidha, Nafikiri Rais awe mwangalifu sana katika kuchagua maneno au lugha ya kuongea mbele za hadhara za Watu, asiwe anaamini kila kitu anachoambiwa na wale Watu wanaomzunguka. Sometimes anadanganywa au amekuwa akiambiwa Habari ambazo zimetiwa chumvi Sana. Awe anachuja maneno ya kuongea hadharani.
 
Weka gazeti lako hapo.Rais Samia ni kipenzi cha mamillioni ya watanzania.Ndio Maana habari zake hazikauki midomoni Mwa watu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…