Kuhusu kujiimarisha kiuchumi, kijeshi, kitechnology . Hayo hayawezi kufanyika ikiwa kila wakati proxies wa wa Iran wanavamia na kufanya vita.
Japo mimi siamini katika mambo ya dini lakini bila shaka yoyote wewe ndio uliekaririshwa kuhusu haya uliyoandika hapa JF.
Nasema umekaririshwa kwa sababu ulichoandika ni upuuzi mtupu, na hakina ushahidi wowote wa maana.
IPO HIVI ....
Acha nikufungue macho, akili na fikra zilizofungwa upande mmoja na watengeneza propaganda wa Netanyahu na Israel, kwa lengo la kutaka uendelee kuwaona kina Netanyahu na genge lake ni miungu yako isiyoweza kukosea chochote hapa duniani 🤣, na kwamba eti ukiongea kinyume na wanachotaka wao uamini, basi utakuwa umejikosesha wewe mwenyewe ticket ya kwenda mbinguni na hautobarikiwa na mungu wao 🤣🤣🤣.
Kwa aina ya majirani alionao Israel. Kiongozi kama Netanyahu anahitajika pamoja na kumuona ana mapungufu. Israel imezungukwa na majirani walioapa kufanya nao vita vya milele. Nayo ni kwa sababu ya kukaririshwa imani potofu dhidi ya waYahudi.
Ukweli ni kwamba katika hao majirani wote unaosema hapa, hakuna jirani yoyote anaewachukia wayahudi. Na ndiomaana hizo nchi zote zipo na raia wengi tu wenye asili na imani ya kiyahudi. Kuanzia Jordan, Egypt, Syria na Lebanon kote huko kuna wayahudi wengi tu wanaishi huko bila shida yoyote na hatusikia wanashambuliwa wala kuuwawa.
Iran ambayo umedanganywa eti inachukia wayahudi, ndio nchi ya tatu duniani kuwa na wayahudi wengi baada ya Israel, Marekani. Ukitaka ushahidi wa hili hebu nenda kwenye Google ambayo inamilikiwa na wazungu wakiwemo wayahudi wenyewe utaona imethibitisha hivyo kwamba Iran inashika nafasi ya tatu kuwa na wayahudi wengi duniani.
Sasa kama Iran haiwataki wayahudi kwanini haikuanza kuwachinja kwanza wale wayahudi waliopo Iran?
Tukiachana na Hamas huko Gaza, ni kawaida kusikia walowezi wa kiyahudi wamevamia makazi ya wapalestina kimabavu, kuwapiga na wengine kuwaua bila sababu. Lakini kamwe hauwezi kusikia myahudi wa Iran amevamiwa nchini Iran na kuuwawa kwa sababu ya dini, au asili yake. Myahudi wa Iran ana haki sawa na zile walizonazo raia wengine ndomaana hauwezi kuona wananyanyaswa au kuteswa hata siku 1.
Tukija kwa kina Netanyahu hawa wanachukiwa kwa sababu kwanza wengi wao ni wazungu waliotokea Ulaya na Marekani kuja kutawala na kunyanganya ardhi za watu wengine waliowakuta katika eneo hilo. Iran imekuwa ikitumia makundi ya wapambanaji kuwasaidia wapalestina kupigania haki zao kama Israel inavyosaidiwa na Marekani, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani kukandamiza haki za wapalestina.
Hayo mambo ya sijui Iran au majiran wanawachukia wayahudi ni ya uongo kwa sababu hizo nchi zote ikiwemo palestina zina raia wengi tu wa kiyahudi na hakuna mwenye muda au mawazo ya kuwaua.
Netanyahu na genge lake wakikubali kuwaacha wapalestina waishi kwa amani basi hakuna mtu atakaekuwa na shida nao kwani wayahudi hapo wapo wengi miaka na miaka toka enzi za waajemi, wagiriki, waroma na Othman empire, kabla hata hao wazungu hawajaja miaka ya 1947 kuanzisha taifa hilo.
So ni wewe ndio uliemezeshwa matango pori kuhusu nchi hizo kuchukua wayahudi. Sio kweli na ni uongo wa zamani kabla mambo ya sim za kiganjani ambayo mtu unapakua na kujua ukweli hayajaja.
Jana raisi wa Ufaransa Emanuel Macron kwenye speech yake katika bunge la Uingereza aliwaambia wabunge wa Uingereza kwamba ili amani ya kweli ipatikane pale Israel au Mashariki ya kati basi ni lazima Israel na nchi za Magharibi zikubali kulitambua taifa la Palestina na kuwatoa walowezi wote waliovamia ardhi na makazi ya wapalestina.
Sasa unaweza kujiuliza kati ya waliokulisha matango pori na raisi wa Ufaransa Macron nani anaefahamu haswa kinachoendelea huko Israel na Palestina?
Umepewa kichwa chenye akili ili kufikiri, sio kufugia nywele na kamasi tu ndugu yangu. Amka!