Uchaguzi 2020 Hivi ni haki kweli kwa akina Robert Amsterdam kuingilia uchaguzi mkuu wa nchi yetu? Je, tunaweza kuwashitaki kwenye mahakama za kimataifa?

Yote ni ubatili tu, hapa duniani kuna sheria tu, haki iko mbinguni kwa Mwenyezi Mungu.
 
Amsterdam ni mwanasheria kitu Cha msingi labda uchunguze mipaka ya kufanya kazi yake Ni ipi ndio uje hapa kulalamika.Kama amevuka hiyo mipaka ama la!
 
Lisu = Kigogo (chahali)= amsterdam hiyo ni project moja ya mabeberu kujaribu kutu destabilize.
Wewe Kweli ni "Stroke". Mabeberu ilikuwa ni "slogan" za kina Nyerere Kipindi Cha Vita baridi.Sasa hivi Dunia nzima Wana mfumo mmoja wa kibepari(capitalism).Ujamaa kama haujafa basi uko hoi bin taabani hapa duniani.Hata huko China,Urusi kuna mabilionea .Kwa mantiki hiyo ukitumia slogan ya "Mabeberu" hata wao ni "Mabeberu".
Wewe tu na Jiwe naona ndio mnatumia slogan za kizamani!
 
kumbuka anasimamia haki ya mteja wake na siyo kuingilia ndo maana nchi zilizoendelea unakuta unakamatwa unakataa kuongea chochote mpk mwanasheria wako aje so yule kwa maana nyingine ni Lissu
 
Wewe Kweli ni "Stroke". Mabeberu ilikuwa ni "slogan" za kina Nyerere Kipindi Cha Vita baridi.Sasa hivi Dunia nzima mfumo mmoja wa kibepari.Hata huko China,Urusi kuna mabilionea .Kwa mantiki hiyo ukitumia slogan ya "Mabeberu" hata wao ni "Mabeberu".
Usipotoshe issues hapa....Kama hujui nyamaza...maana ya ubeberu kwa kiingereza ni imperialism...na imperialism bado ipo..Imperialism tendencies bado zipo...unachozungumza kuhusu mfumo ni globalization au utandawazi ambapo capitalism ndiyo engine yake.,
 
Tatizo lako bogus wewe nilishakwambia awali ufuatilii kitu kingine chochote zaidi ya siasa za JF, ndio maana sishangai kuona unatetea kila ya aina ya upuuzi wa Lissu.
Ningeshangaa kama usingepanick.
 
Ningeshangaa kama usingepanick.
Nenda ukamwambie Lissu asijifananishe na Magu sio size yake.

Yeye kazoea kuiga anachofanya Magufuli ila mwenzake ajali anachofanya mara sijui ohoo mimi kigulu nazunguka nchi nzima who cares Magu na team yake nzima ya makamu na PM awawezi .

Nani kamwambia strategy ya CDM na CCM kwenye campaign zilikuwa sawa aache kujilinganisha na raisi wa nchi.
 
Amsterdam ni tapeli mpiga debe tu, wala usiwe na wasiwasi naye kabisa. Ubaya kwake ni kuwa anapambana na mtu mwenye msimamo. Wewe focus kwenye uchaguzi tu usihangaike na Amsterdam hata siku moja; atalala usingizi muda wowote kuanzia sasa.
Sawasawa kama tapeli basi endeleeni kufanya ujinga wenu muone matokeo, dadekiiii
 
Hizo ni siasa za kizamani.Ukiwa mjamaa huwezi kuwa bilionea.Nyerere ni mjamaa halisi.Mpaka anaondoka madarakani hakuwa na mali.Alipoona Ujamaa umefeli duniani aliamua kuondoka.Hizo globalization,free trade,free economy,they are just "terminologies".Zote Zina akisi mifumo ya kibepari na kibeberu!
 
Kamwambie magufuli hamuwezi Lissu, alishindwa kumuua na hatamuweza pia kwenye Sanduku la kura
 
Ccm vilaza ndugu wavumilie tu
 
Nani anataka kujifananisha na rais wa Tanzania? Au unamuona rais wa Tanzania ni mtu superior sana mpaka itokee mtu anataka kujifananisha naye? Ingekuwa rais wa US ingekuwaje? Ww kwakuwa ni limbukeni ndio unamuona rais wa Tanzania ni mtu wa maana sana.
 
Kamwambie magufuli hamuwezi Lissu, alishindwa kumuua na hatamuweza pia kwenye Sanduku la kura
Ijumaa sio mbali ‘hayawi hayawi,.....’ Magufuli anashinda asubuhi na mapema. Tuone Lissu na Amsterdam watafanya nini.
 
Lisu = Kigogo (chahali)= amsterdam hiyo ni project moja ya mabeberu kujaribu kutu destabilize.
Waku destabilize una nini wewe?? Ndo propaganda mnazolishana huko lumumba😂😂

Nani aliwaambia mpige watu risasi, mteke na kuwaua??? Pambaneni na hali zenu sasa
 
Hayo sasa kamwambie Lissu kutwa kujifananisha nae, kama nilivyokwambia wewe uwa ufuatilii chochote nje ya JF.

Wakati Lissu kila siku majukwaani anatamka chochote anachofanya Magufuli na yeye atafanya mpaka kaanza kucheza na yeye mziki majukwaani kisa Magufuli anacheza.
 
Jiwe nje ya mifumo ya dola(polisi+tiss),idara za serikali pamoja na tume ya uchaguzi,ambazo zinambeba ni mwepesi kuliko unyoya wa kuku.
Akitaka aone anashindwa uchaguzi saa 4 asubuhi ya tarehe 28,ajitoe huko.Kumlinganisha Lissu na Jiwe kwenye ulingo wa siasa ni sawa na kumfananisha ,"Tysoni"Lissu na "Matumla"Jiwe
 
We uliona wapi Mabeberu wanaangaika na nchi ambayo haina natural resources wanazozitaka. Rwanda haina natural resources ndo maana Mabeberu hawakuingilia Kati. Nchi zenye raslimali ndo Mabeberu hukimbilia kuiba na kupora kwa mgongo wa haki za binadamu na Demokrasia. Mfano hai angalia Kilichotokea Libya,(Mafuta) Congo(Madini) DRC, Venezuela (Mafuta) n.k hutakaa usikie Beberu ameingilia mambo ya ndani ya nchi isiyo na raslimali
 
Wewe mtu unayo 'akili' nzuri?
Mahakama ya nani, aliyojimilikishia Magufuli kama alivyomilikisha CCM.
Tume ya uchaguzi ipi, ile anayomiliki Magufuli?

Na hapa wewe mwenyewe unaonyesha umemilikiwa na huyo huyo Magufuli!

Sisi tunakataa kumilikiwa kama mifugo na mtu mmoja.

Sasa kwa vile akili yako ni fupi hutaweza kuyaelewa haya niliyoandika.

Hao akina Amsterdam hawapo hapa na wala hawahusiki na lolote linalotuhusu waTanzania.

Unawasikia kwa sababu Magufuli ndiye anayewakaribisha kwa haya anayoyafanya ya kuminya HAKI za wananchi wake.

Mwambie aachane na tabia hiyo, na hutasikia cha Amsterdam au nani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…