Hivi ni kwanini tumeshindwa kujenga O'bey, Masaki, Ada Estate au Upanga nyingine?

siku hizi oysterbsy haina tofauti na mbagala. ilianza kuharibika mara tu baada ya ile project ya viongozi kuamua kuuziana nyumba za serikali.

juzijuzi tu hapa nilienda kumtembelea kiongozi fulani mstaafu, nikakuta uwani kwake kaotesha migomba, pia anafuga kuku, nguruwe na ng'ombe wa maziwa.

harufu kali ya kinyesi cha mifugo yake inaleta usumbufu mkubwa kwa jirani zake.
 
Inawezekana walikaa na mabeberu kwa muda mrefu
Botswana population ya wazungu Ni wengi ndio maana ipo vile,
Botswana, Namibia, South Africa na Zimbabwe kabla Mugabe hajaharibu, population za Wazungu waliobaki baada ya Uhuru Ni wengi na ndio wamesaidia kuzipandisha nchi zao
 
Simple Serikalini pawe na ajira za mikataba.
 
Botswana population ya wazungu Ni wengi ndio maana ipo vile, Botswana, Namibia, South Africa na Zimbabwe kabla Mugabe hajaharibu, population za Wazungu waliobaki baada ya Uhuru Ni wengi na ndio wamesaidia kuzipandisha nchi zao
Botswana haikukaliwa na wazungu, lilikuwa jangwa kabla ya kugundua almasi na dhahabu.

Nimetoa mfano wa nchi za kiafrika zenye weusi wengi
 
Botswana haikukaliwa na wazungu, lilikuwa jangwa kabla ya kugundua almasi na dhahabu.

Nimetoa mfano wa nchi za kiafrika zenye weusi wengi
Ilikutawaliwa na Waingereza ikiitwa Bechuanaland, Uhuru ilipata mwaka 1966

Mzee hayo madini ya Almasi na Dhahabu unadhani waligundua watu gani? Na yanachimbwa na watu gani? Ni Wahindi na Wazungu
 
Mambo ya Dathramu mnapenda sana kuyafanya ya kitaifa, jengeni basi Dodoma kwa mpango ili tuone... sisi huku mikoani huwa mnatuchukuliaje?
 

Mbweni JKT,Malindi na Mpiji ndio Next Obay Miaka ijayo!!
 
Ilikutawaliwa na Waingereza ikiitwa Bechuanaland, Uhuru ilipata mwaka 1966

Mzee hayo madini ya Almasi na Dhahabu unadhani waligundua watu gani? Na yanachimbwa na watu gani? Ni Wahindi na Wazungu
Dhahabu na almasi zinachimbwa na wawekezaji kwa ubia wa 49-51 percent. Hao wawekezaji hata hapa kwetu wapo.

Wazungu ni wengi Tanzania kuliko Botswana.
 
Dhahabu na almasi zinachimbwa na wawekezaji kwa ubia wa 49-51 percent. Hao wawekezaji hata hapa kwetu wapo.

Wazungu ni wengi Tanzania kuliko Botswana.
Ni asilimia 3 ya Population ya Botswana, Ni wachache kwa absolute numbers Ila Ni wengi relatively ukilinganisha na nchi nyingine Africa,
Population ya Botswana Ni milioni 2.5 tu, Ina mbuga za wanyama zinazoingiza fedha za Kigeni, ambayo Ni nyingi
ukilinganisha na population yao ndogo

Mabeberu wamewekeza vizuri kwenye utalii pia, na kule poaching sio kubwa
 
Waulize watu wa halmashauri. Watu hawana upeo wala maono. Ni moja ya sababu naunga mkono MAGU kutowaongezea mishahara wafanyakazi wa serikali -tena ikiwezekana wapunguziwe- hawa watu hawafanyi kazi zao.
😂😂😂 Dah mkuu!
 
Serikali gani sasa Becky? Ya huyu ambaye huwa anasema “waacheni machinga wafanye biashara zao popote kwa uhuru”!!! Tz ili uishi sehemu nzuri ni lazima uwe na pesa sanaaaa, na hata hizo sehemu nzuri si nzuri kivileeee, very shame!
 
Ilikutawaliwa na Waingereza ikiitwa Bechuanaland, Uhuru ilipata mwaka 1966

Mzee hayo madini ya Almasi na Dhahabu unadhani waligundua watu gani? Na yanachimbwa na watu gani? Ni Wahindi na Wazungu
Maendeleo ya wa Botswana yameletwa na wenyewe hasa sera za madini ambazo zimenufaisha wa Botswana,hapa mipango yao kimaendeleo, nilisoma na wa Botswana aisee walikuwa sanatunanga sana, kw Africa Botswana imefika level ya developmental state
 
Kiukweli miundo mbinu ilikwishawekwa kwa maeneo ya Magomeni, Ilala, Mwananyamala na Kinondoni na Kariakoo.

Kilichohitajika ni muendelezo na uboreshaji.

Unaweka tu maneno haya ni Phaee 1 na haya ni Phase two na unayaendeleza.

Hata Temeke, Tandika, Kurasini Kilwa road sehemu hizi zinaweza kabisa kugeuzwa kuwa maeneo ya kuvutia kutokana na mipango miji madhubuti.

Maeneo mengine kama Buguruni, Tabata na Ubungo yote yanaweza kufanyiwa kitu chaitwa urban regeneration.

Sidhani kama tunao watanzania walosemea hii kitu.

Kwa kifupi ni kwamba ufisadi ndo ulosababisha haya yote ya kutoendeleza miji na makazi kwa ustadi unotakiwa.

Badala yake fedha zilikuwa zatumika kwa mambo mengine yasokuwa na maana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…