Hivi ni kwanini tumeshindwa kujenga O'bey, Masaki, Ada Estate au Upanga nyingine?

Mimi nadhani watanzania wengi hata waafrika tuna alergy ya kufuata utaratibu.

Mtu hataki kufuata utaratibu uliowekwa lazima tu atafute njia ya mkato.

Tabia hii ndio imezaa Rushwa , Rushwa itaisha tabia hii ikiisha.
 
Unataka ccm yetu ikose kura,

Kikwete wanamsema alikuwa dhaifu lakini wakati wake Machinga hawakuzagaa kwenye barabara za Dsm.
 
Ustaarabu na utanashati ni tabia na asili, unless otherwise mamlaka ziamue kwa makusudi yaliyokamili kutekeleza kilichipangwa. Naam, KUTEKELEZA KILICHOPANGWA!!
 
Ni kweli kuna sehemu nilienda hadi nikajiuliza kama kuna viongozi wa serikali, yaani sisi waafrica tuna upumbafu mwingi sana sijui tupoje aisee

nenda mbagala ukaone namna jenga uza walivyo jenga nyumba za hovyo..
Sio mbagala tu ni almost Tanzania nzima. Kuna wazungu nilienda nao Mbeya mwaka fulani hadi niliona aibu jinsi Mbeya mjini ilivyojengwa hovyo. Nenda mwanza uone watu walivyojenga kwenye mawe milimani kama viota vya ndege.

CCM wameiharibu sana Tanzania. Hii nchi inabidi siku tukipata pesa viongozi wapya wavunje maeneo yote yaliyojengwa hovyo na wayajenge upya kwa mpangilio mzuri
 
Nchi hii viongozi wa CCM wanachojua ni kujinufaisha binafsi na familia zao ila walivyo wapumbavu wote wanaishia kuishi maeneo yaliyojengwa hovyo.

Kuna mda unaweza dhani Tanzania tuna watu wenye upungufu wa akili nchi nzima.
Narudia tena kwa maendeleo ya kweli ya watu na vitu nchini humu lazima tuitoe CCM madarakani kiingie Chama kipya chenye mrengo wa kisasa wa maendeleo sio hawa wenye akili za kijamaa zilizopitwa na wakati ambao kwao umasikini na unyonge ni sifa.
 
Suala la mipango miji nchi hii ni tatizo sugu kuliko hata Mr 2.
 
wewe bifu lako na wahamiaji toka mikoani ni nini?? kama unataka utulivu nunua shamba mkuranga ishi huko uone kama kuna atakuletea vurugu
 
National housing zote zilizojengwa, nyumba zilikuwa kwa mpangilio badaye wabongo wakaja wakaziba vichochoro vyote wakajenga
Sehemu za open space zote watu wamejengaaa
Ukweli sisi tuna matatizo makubwaaaa

Ova
 
Na sasa kuna kinachitwa kurasimisha maiazi, hapo ndiyo balaa

Mungu Ibariki Tz - MITz
 
Hili la ufugaji katika makazi ya watu ndo linanikera.. kuna mitaa ukienda kunanuka balaa, huyu kafuga ng'ombe, yule nguruwe, yule kuku wa kisasa.. yaani ni kero!
 
Ningekuwa raisi. Kwa mamlaka ambayo ningekuwa nayo kikatiba na kwa heshima na taadhima ningekuteuwa rasmi uchukue nafasi ya lukuvi wizara ya nyumba, makazi na nini sijui....... Ili uifanyie kazi maneno yako haya ambayo kiukweli yamenigusa sana na yapo kizalendo wazi wazi.
 
Hata huko Masaki kuko hovyo, obey kunatia aibu Bora hata bunju kwa Sasa kuko vizuri kidogo
Bunju ni ule upande wa bunju A tu. Na ni sehemu ndogo sana ukiwa unaelekea maeneo ilipo shule ya MOGA ile lami inayoelekea mbweni....

Ila huku upande wa chini waswahili wameshavamia kumekuwa kama mbagala.

Shida ni upigaji, kwa maana hela zilishatolewa kwa msaada wa benki ya dunia kujenga pilot project ya makazi. Ila jamaa wakapiga zile hela matokeo yake wamefanya vipimo sehemu ndogo sana.

Ila ukija huku upande mwingine wamepaacha kama palivyo na raia wa kiswahili wameshanya yao na vile viwanja vyao vya kipimo cha 15 kwa 15.

So kimsingi tunafelishwa na mipango ya serikali ambayo inasubiria mambo ya harabike ndipo wajue la kufanya ila sio kujenga mipango sahihi ya kuujenga mji.
 
Moderators hivi huu uzi unastahili kuwa kwenye jukwaa la hoja mchanganyiko??? Wakati unawagusa wanasiasa wa nchi hii ambao ni policy makers???

Embu urudisheni jukwaa la siasa!
Huu uzi sio wa kisiasa.... Huu uzi ni wa maendeleo
 
Kusema kweli nachukia nafasi za kisiasa. Ila kwa jinsi suala la makazi na mipango miji linavyoniumiza kuhusu Tanzania itanibidi tu nipokee iyo nafasi nitoe mchango wangu.

Asante Mkuu kwa kutambua mawazo yangu kama ni mazuri. Tanzania tuna watu wengi sana wenye mawazo mazuri, Tatizo lililopo ni kuwa wenye mawazo haya mazuri hawapewi nafasi wanaishia kupewa nafasi watu uchwara ambao walikuwa wanacrame tu darasani na wao kuifanyia makubwa nchi iwe nzuri, na ya kisasa sio ndoto yao kuu.
 
Watabuni na kujenga Masaki na O’bay kwa mtaji gani wa uzoefu?
Mtu katoka bush, halafu ndio mkurugenzi wa mipango miji, unategemea nini hapo.
Hata huko Masaki, O’bay anakusikia tu, hajawahi kuishi huko, naye anakaa Bonyokwa!
Ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] halafu ujue watu wanaofaulu kwenye hizi vyuo zetu mara nyingi sio watoto wa mjini. Ni wale walugaluga waliotoka vijijini huko ndani ndani hukoooo wanakuja mjini kusoma so wanakomaa na shule kama ibada.

Hawa ndio huwa wanafaulu maksi za juu sababu ya kuclamisha masomo muda mwingi. Na ndio serikali inawapick kama best candidate. Ila vichwa vyenyewe huwa vinapiga average tu.... Unakuta kichwa kina GPA ya 2.8 au 3.0 ila ndio kichwa kina idea za kuweka mambo sawa hadi basi......

Aiseee inabidi tuanze kujadili effectiveness ya hizi GPA zetu kuanzia leo hii.
 
ndo maisha na uwezo wetu ulipoishia hapo usifos tufanane na watu wengine.

tatizo lenu mlio wengi ndo Hilo mnajidharau Sana na kijipima kwa wazungu.

sisi hata tukila mavi, tukaishi mapangoni ama kulala kwenye miti sawa tu maana ndo sisi.

yaani SISI.

Sent from my Infinix X5515 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…