Hivi ni kwanini tumeshindwa kujenga O'bey, Masaki, Ada Estate au Upanga nyingine?

Wewe hebu nenda kaendelee kuunga mkono juhudi za mwenyekiti tuache sisi tusio na mashiko na biashara yenu ya kisiasa...... Tuache tunajadili mambo ya msingi hapa na watanzania wenzangu tukiwaandalia a better tomorrow watoto na wajukuu wetu.....
 
Hii mada ni kubwa sana kwako ndugu. Kwa kifupi iko juu yako saaaana. Ni vizuri tu ukasoma na kupita kimyakimya ndugu
 
Inasikitisha Sana hyo Hali watu wanauziana 15 kwa 15 mbona vidogo nyumba zinabana kunakuwa hamna hata hewa Kati ya nyumba na nyumba, nadhani mipango Miji na halmashauri zimelala, nimependa jinsi Dodoma kunavojengeka wanajitahidi Kuna maeneo hauruhusiwi kujenga nyumba ya chini, ni ghorofa tu pia viwanja vina distance nzuri na kunapendeza.
Ila in short jiji la Dar ni slums kila corner sehemu zilizopimwa ka sinza watu wamejenga hovyo hovyo no space ni kuta kwa kuta tu.
 
Dodoma kuna watendaji wana akili kidogo kama yule Mkurugenzi wa Jiji. Wameanza vizuri kwa kweli ila ninavyoona siasa zimeanza kuingia na pameshaanza kuharibika. Bora waamke saivi.

Juzi tu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Magufuli ametangaza ni ruksa mama ntulie, bodaboda na wachuuzi kuingia na kufanya kazi stand ya Dodoma na wasizuiwe. Huyu ndo raisi wa nchi alafu anahamasisha haya.

Nakwambia si tu Dar es Salaam , Tanzania karibu asilimia 90 ya makazi na maeneo ni slums zinapotofautiana ni kuwa kuna slums zilizojaribu kupangwa na zingine ambazo hazijapangwa kabisa. Kiufupi ni kuwa asilimia 90 ya miji na maeneo ya Tanzania ni takataka.

Tunaitaji watu watakaopanga upya miji yetu na kuweka miongozo ya jinsi ya kujenga nchi nzima na kusimamia iyo miongozo.

Hakuna lisilowezekana maana kama Dubai waliweza Kwa nini sisi tushindwe?? Kama wazungu wameweza kwa nini sisi tushindwe??? Mataifa ya hapahapa Afrika Mf Botswana wameweza pale Gaborone kwa nini sisi tushindwe???? Senegal wameanza pale Diamniadio na wanafanya vizuri sana, sie tunashindwa nini????
 
Mzungu pamoja na kuwa simpendi, lakini ana uwezo wa kutumia akili yake kuyaweka maisha yake na yale ya wananchi wenzake yakawa rahisi na ya kupendeza.

Katika hili ninakubali kuwa sisi watu weusi ni manyani. Hatujitambui kuwa sisi pia ni binadam na tunatakiwa ili tuweze ishi katika mazingira mazuri, tunahitaji kuweka utaratibu wa mipango yetu.

Rais Magufuli amejenga magorofa ya Magomeni Quarters, sina uhakika kama wapangaji miji wetu walichukua taratibu zote zinazo paswa katika ujenzi wa hayo magorofa.

Nasema hivi kwa sababu sisi watanzania tukiambiwa tujenge yumba basi tuko mbio mbio sana katika kutekeleza hayo badala ya kuanangalia vitu muhimu vinavyotakiwa kuangaliwa katika ujenzi huo.

Serikali za kizungu ziko hivi, kabla ya kujenga makazi ya watu wake wanaangalia idadi ya wakazi, watapitisha au kuweka miundo mbinu muhimu kama; mabomba ya maji safi, mabomba ya maji taka, mitaro ya maji ya mvua kutoka majumbani na barabarani, barabara za mitaa, nyaya za umeme na taa za barabarani, nyaya za simu, TV na Radio, na internet.

Pia wanaangalia ni nyumba za aina gani zijengwe na kama za gorofa ni mpaka gorofa ngapi. Vilevile wanagarantii mobility ya wakazi kwa kuweka public transport, sehemu za michezo za vijana na watoto na sehemu za mahitaji muhimu ya vyakula kama soko na maduka.

Kwa kifupi wanazingatia mambo yote ya umuhimu ya wakazi katika eneo na sio majengo tu. Wanafanya vitu kwa system.
 
Umesema vyema kabisa ndugu. Mtu mweusi anatakiwa kuwekewa taratibu na zaidi asimamiwe katika kufuata huo utaratibu.

Tatizo la Tanzania kwanza ni sera za Chama ambazo zimekuwa zikituongoza na pili ni aina ya watu wa Chama hicho ambao wanapewa uongozi katika nafasi mbalimbali hapa nchini. Wengi kama wana exposure basi wanakuwa wajinga na wengine ndo hawana exposure kabisa. Ndo mana sasa nchi hii imeharibiwa vibaya tena sana.
 
Hiki ni kigezo kimoja kikubwa cha ngazi ya uchumi ya nchi. Majuzi tumejipongeza kwa kufikia “uchumi wa kati”. Sidhani kama kiuhalisia ina maana kubwa kwetu. Kiwango cha umasikini ni kikubwa kiasi kwamba chama tawala kinajikuta kikitegemea kura za wamachinga na mama lishe na hivyo kuruhusu sekta hiyo kugeuza miji kuwa majalala (slums).

Aidha, karibia nyumba zote za kuishi (residential) zinazojengwa siku hizi zina “fremu” za maduka, mama lishe, “grosari” bila kusahau “car wash” za kila sampuli. Si rahisi kuwa na O’bay, Upanga, Ada na Regent Estate za zamani. Tunazidi kurudi nyuma.
 
Huo ndo ukweli. Hakuna maendeleo hapa kwetu kiuhalisia. Tunarudi nyuma mara 1000 kila siku.
Ujenzi wetu ni wa hovyo kabisa na mamlaka wala hazishtuki.

Mfano Dar Viongozi wangekuwa serious maeneo mapya yanayoendelea kama Kigamboni, Kinyerezi, Mbezi , Goba na Bunju ndo Viongozi wangetakiwa kuonesha ubunifu wao kwa kuweka na kusimamia miongozo ya ujenzi wa makazi.

Ila kote nako huko yanayofanyika ni uchafu mtupu. Nenda Mikoani kote ni uchafu mtupu
 
Masaki na osterbay imehabika karibuni baada ya watu kuuziwa Nyumba za serikari na kutokuwa na utaratibu maalumu wa kusimamia uendelezaji wake. Ni aibu kwa maeneo hayo kongwe yaanze kulingànishwa na miji ya juzi tu kama Bunju beach na Mbweni
 
Waulize watu wa halmashauri. Watu hawana upeo wala maono. Ni moja ya sababu naunga mkono MAGU kutowaongezea mishahara wafanyakazi wa serikali -tena ikiwezekana wapunguziwe- hawa watu hawafanyi kazi zao.
Roho mbaya hiyo
 
Uzi Bora kabisa wa mwaka 2020
 
Mbona bahari beach pazuri
 
Mipango miji watu hawako na.weledi njaa tupu
 
Sasa hivi kariakoo hapafai
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…