I think watanzania tunatumia asilimia mbili za ubongo miji yetu utafikiri hatuna ma town planner's nchi hii sehemu kuliko jengwa vizuri ni huko vijiji vya uchagani atleast nyumba Zina garden, miti ya kivuli na u nature wake Wala miti haijakatwa kabisa.Uzi Bora kabisa wa mwaka 2020
Sio kariakoo tu ndugu. Tanzania nzima ni uchafu mtupu. Ukienda nchi za wenzetu kitendo cha kushuka tu airport utagundua utofauti mkubwa sana na hapa kwetuSasa hivi kariakoo hapafai
Mwezi nilienda mabwe pande ni eneo zuri sana Ila nilivyoliangalia Roho iliniuma sababu linakuja kuwa squatter watu wanajijengea hovyo ni aibu sana alafu watu kutwa kumfia lukuviSio kariakoo tu ndugu. Tanzania nzima ni uchafu mtupu. Ukienda nchi za wenzetu kitendo cha kushuka tu airport utagundua utofauti mkubwa sana na hapa kwetu
Tatizo kubwa ni udhaifu katika usimamizi wa Sheria za mipango miji kutokana na udhaifu wa Serikali za Mitaa. Mimi naamini na Nina uhakika kabisa kwamba ramani zote za mipango miji ziko wazi zikionyesha matumizi ya kila eneo limepangiwa Shughuli na majengo ya aina gani ukiachana na yale maeneo ambayo yamevamiwa kutokana na udhaifu wa Serikali kutopima maeneo kwa Wakati.Watu hawawezi kufanya kazi nyinginezo hata za kuzalisha, Ni kuchuuza bidhaa za kichina tu?
labda kweli.Hii mada ni kubwa sana kwako ndugu. Kwa kifupi iko juu yako saaaana. Ni vizuri tu ukasoma na kupita kimyakimya ndugu
Sawa lakini msimamo upo palepale.Roho mbaya hiyo
Kwakweli kwa Dodoma CDA wote tangu ilipoanza hadi leo walipaswa wawe mahakamani kwa uhujumu uchumi! Maana hata maeneo ya city centre kama makulu na Mkalama eti yamejengwa kiholela! Miaka yote CDA walikuwa wanafanya nini?Mitaa yenyewe unayoitaja haijajengwa kwa utaratibu, ni mitaa ya hovyo hovyo tu ila ina nyumba nzuri nzuri.
Kinachotofautisha masaki na mbagala ni thamani ya nyumba lakini sio mpangilio wa mitaa na ubora wa nyumba zilizoko huko.
Kwa mpangilio wa mitaa masaki, Ada estate na obey haina tofauti na gongo la mboto au mbagala.
Hii nchi kwenye mipango miji na mitaa ni sifuri, hakuna mahala tumefanikiwa. Dodoma wale cda walipaswa kupewa kesi za uhujumu uchumi.
Sheria zipo mkuu, madhaifu yapo kwenye usimamizi. Sheria inayosimamiwa vizuri naona ni kipengele cha kutoza faini za usalama barabarani na sheria za kodi, zingine za usafi wa mazingira na mipango miji muda mwingi zipo likizo. Tatizo nadhani ni watendaji, ili waende saiti wanataka pawe na posho bila posho hawaendi hata kama gari lina mafuta. Maafisa mipango miji wanataka lazima wawe na GPS kupanga miji, lkn upangaji miji mzuri ulipaswa kuanza hata kabla hatuna gps kwa kuwatumia watendaji kuanzia kupanga vijiji, alama hata kupanda mkonge zingetumika.Serikali iingilie,mtu akitaka kununua na kujenga kitu lazima aombe permission na akionyesha hataleta madhara kwenye mipango mji ndio aruhusiwe...
Second, ni kuimpose stricter rules,kwa wanaodump uchafu iwe mtu mmoja au familia..walipishwe fines za kutosha
Kuwa na nyumba za zamani au nyumba za miti sio tatizo, tatizo ni mpangilio wa miji na mitaa. Nyumba itazamwe wapi na geti liwe wapi hata kama nyumba ni ya mitiSingida wanajitahidi kwa kuupanga mji,,tatizo wakazi wamekomaa na nyumba za 1947
Mimi hilo napinga, kwa maoni yangu kunatakiwa kuwe organized, ikiwezekana hata kila mtaa kuwa na eneo lililotengwa kwa biashara ambapo wafanyabishara ndogo ndogo watafanya. Hii ndivyo inatakiwa. Hata DSM ilipaswa kila mtaa kuwe na eneo la biasharaMtazamo wako ndo wenye changamoto, tunaishi vizuri tu. Mimi binafsi sikwaziki na kuwepo kwa vibanda kila mahali.
Kuna wengine wamepewa nafasi, tatizo ni ubunifu wa kufanya kazi hizo kwa gharama nafuu. Wanataka mpaka wapewe mabilioni ndio wafanye kaziKusema kweli nachukia nafasi za kisiasa. Ila kwa jinsi suala la makazi na mipango miji linavyoniumiza kuhusu Tanzania itanibidi tu nipokee iyo nafasi nitoe mchango wangu.
Asante Mkuu kwa kutambua mawazo yangu kama ni mazuri. Tanzania tuna watu wengi sana wenye mawazo mazuri, Tatizo lililopo ni kuwa wenye mawazo haya mazuri hawapewi nafasi wanaishia kupewa nafasi watu uchwara ambao walikuwa wanacrame tu darasani na wao kuifanyia makubwa nchi iwe nzuri, na ya kisasa sio ndoto yao kuu.
Hata interview ni za maswali ya darasani na sio maswali fikirishi kama " how will you solve the problems of ... In DSM using the minimum possible budget and local unskilled labour." Baadala yake unaulizwa maswali ya kukariri kama vile mention roles of central bank! Na sio how I'll you solve the problem of unequal distribution of wealth in the country.Ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] halafu ujue watu wanaofaulu kwenye hizi vyuo zetu mara nyingi sio watoto wa mjini. Ni wale walugaluga waliotoka vijijini huko ndani ndani hukoooo wanakuja mjini kusoma so wanakomaa na shule kama ibada.
Hawa ndio huwa wanafaulu maksi za juu sababu ya kuclamisha masomo muda mwingi. Na ndio serikali inawapick kama best candidate. Ila vichwa vyenyewe huwa vinapiga average tu.... Unakuta kichwa kina GPA ya 2.8 au 3.0 ila ndio kichwa kina idea za kuweka mambo sawa hadi basi......
Aiseee inabidi tuanze kujadili effectiveness ya hizi GPA zetu kuanzia leo hii.
Mkuu Dodoma pia kuna mtaa wa MLIMWA KUSINI kumepimwa vizuri tu lakini viwanja vimebanana utadhani slums, vipo vya 13 X 15 vingi sana, nyumba zimebanana hakuna hata maeneo ya wazi. Nimesikitika sana! Maeneo ya wazi hakuna kabisa, wakati ndo maeneo muhimu hutumika kwa michezo, assembly point wakati wa dharura, kuongeza mzunguko wa hewa, mikutano n.kInasikitisha Sana hyo Hali watu wanauziana 15 kwa 15 mbona vidogo nyumba zinabana kunakuwa hamna hata hewa Kati ya nyumba na nyumba, nadhani mipango Miji na halmashauri zimelala, nimependa jinsi Dodoma kunavojengeka wanajitahidi Kuna maeneo hauruhusiwi kujenga nyumba ya chini, ni ghorofa tu pia viwanja vina distance nzuri na kunapendeza.
Ila in short jiji la Dar ni slums kila corner sehemu zilizopimwa ka sinza watu wamejenga hovyo hovyo no space ni kuta kwa kuta tu.
Fact! Madhaifu ni usimamizi wa sheria.Tatizo kubwa ni udhaifu katika usimamizi wa Sheria za mipango miji kutokana na udhaifu wa Serikali za Mitaa. Mimi naamini na Nina uhakika kabisa kwamba ramani zote za mipango miji ziko wazi zikionyesha matumizi ya kila eneo limepangiwa Shughuli na majengo ya aina gani ukiachana na yale maeneo ambayo yamevamiwa kutokana na udhaifu wa Serikali kutopima maeneo kwa Wakati.
Aidha kuna sheria ya kutojenga mpaka upate building permit. Iwapo mtu anaekusudia kujenga nyumba ya biashara eneo la makazi sidhani kama mipango miji watakuwa wamempitishia. Vibanda vingi vya biashara vinavyojengwa katika nyumba ya makazi Ni maamuzi ya wajenzi wenyewe, tatizo Ni Serikali yenyewe kushindwa kusimamia sheria zake. Watu wanajenga vibanda vya biashara wakati hati ya kiwanja inasema wazi kwamba eneo hili zitajengwa nyumba za makazi.
Tatizo kubwa lililpo hapa ni hao viongozi wa Serikali wanatakiwa kusimamia sheria hizo ndio haohao wanao vunja sheria hizo. Wote tunajua kwamba nyumba za masaki waliuziwa viongozi wa juu wa Serikali ambao ndio watunga na wasimamizi wa Sera na sheria-wabunge, mawaziri, wakuu wa vyombo vya usalama n.k. Ni udhaifu wa kusimamia sera na sheria za nchi umesababisha watu wengi kuwa wachuuzi na sio wazalishaji.