Mimi huwa nakula hivi na kusurvive siku nzima.
View attachment 3696705
Kula kunatakiwa kuendane na shughuli.
Mtu anayelima na kutembea sana anatakiwa kula zaidi ya mtu anayekaa ndani tu hata kutembea hatembei sana.
Kwa hiyo ukituonesha unavyokula bila ya sisi kujua unavyotumia hicho chakula, how you burn the calories, umetuonesha upande mmoja tu wa mlinganyo.
Waafrika kiutamaduni wamekuwa wakifanya kazi za kuunguza sana calories, kama ukulima na ufugaji. Kazi hizi zinahitaji kula sana.
Mkulima anayelima siku nzima anatakiwa kula vizuri kuhakikisha ana caloroc balance. Mchungaji anayetembea sanankwa siku naye pia.
Tatizo moja kubwa ni kwamba watu wengi wanapobadili maisha na kufanya kazi za kisasa za maofisini, ambazo hazitumii nguvu sana, wanapokuwa wanasafiri kwa magari zaidi kuliko kutembea, badala ya kupunguza kula, wanaendelea kula sana, na pengine hata kuongeza kula kutokana na kipato kuongezeka.
Jambo hili, hususan likendana na kukosa mazoezi, kutojua kupangilia mlo, kupenda kula nyama, vitu vya wanga na vitu vya mafuta, na kunywa pombe, linapelekea unene wa kupita kiasi, obesity, na matatizo ya kiafya kama ugonjwa wa moyo.