Kw
Ili agundue nini kwa huo mlo mmoja?
Ukweli ambao mfumo wa Leo hautaki uujue ni Huu, šmwili wa mwanadamu haukuundwa kuwa kiwanda Cha kusaga chakula saa 24 kwa siku. Dhana kwamba lazima ule Milo mitatu au minne kila siku ni tabia tuliyofundishwa na mfumo wala sio hitaji la mwili wako, umejiendekeza tu
Unapokaa masaa 20 hadi 23 bila kuingiza chakula, mwili unaingia kwenye hatua ya kibiolojia inayoitwa Autophagy.
Huu ni mchakato ambapo mwili wako unajisafisha wenyewe: unakamata seli zilizochakaa, sumu, na mafuta yaliyozidi, kisha unayaharibu na kuyabadilisha kuwa nishati safi. Ni matengenezo ya ndani yanayotokea pale tu unapoiwezesha tumbo kupumzika.
Unapofunga, mwili unachochea homoni zinazoongeza umakini na ustahimilivu wa akili. Matokeo yake? Akili inakuwa sharp, unakuwa na umakini wa hali ya juu kazini, na unamaliza kabisa ule usinziaji mzito wa baada ya mlo wa mchana.
Zaidi ya hapo, unarejesha nidhamu ya nafsi (self-control). Unaacha kuongozwa na njaa za kisaikolojia na utumwa wa kila chakula unachokiona mtaani.
Mbali na manufaa yote ya kiafya na kisaikolojia, kula mlo mmoja kwa siku kunakuokolea pesa nyingi sana ambazo ungezipoteza kwenye mlo wa mchana, snacks, na vinywaji vya njiani! Katika uchumi wa leo, huu sio tu mfumo wa afya tu hii ni mbinu ya kiufundi ya kuinusuru wallet yako isipate mshtuko wa moyo!
Angalizo: kama unaanza leo, Fanya mabadiliko taratibu na hakikisha mlo wako mmoja unakuwa na virutubisho kamili na vilivyoboewshwa.