Hivi ni kwanini wanaume mnaongelea sana maovu ya wanawake na kuyaacha ya kwenu?

Sawa Mkuu
Sijasoma wote ila i get your point, ipo hivi kwa ufupi sana tunaishi kwa kutegemeana hasa kwenye kitu ambacho umekizungumzia ndio husababisha lawama nyingi kwenye jamii dhidi ya Jinsia KE, me naamini tupo 50/50.
 
Huyu haujamkuta kwenye nyuzi nyingine huwa anatumia lugha za matusi balaa sema naona tu leo kaamka vizuri
Best comment in this thread!
Umeiweka point yako vizuri, umeargue kisomi kabisaaa.
Ahsante, sio wengine wanatumia matusi, kejeli, fedheha na udhalilishaji.
mbarika chukua maarifa haya kwa Jokajeusi
 
hauhisi dunia ilianza kupotea pale mmoja alipojitokeza na kusema hii aya haiko sawa? sku hizi hadi ndoa za same sex zinafungwa kwa kutumia biblia hio hio inayokataza same sex, sababu tu kuna mtu amepingana na hiko kipengele. na waumini nao wanaitikia Aameen!!
Tatizo lipo ukishindwa kujua kipi unapaswa kufanya na kipi uache kufanya, ukifanya tu kwa sababu imeandikwa hvyo utapotea.
 
Ni kweli mkuu, lakini haya mambo yanaongelewa hata mitaani na siyo mitandaoni tu yaani inaonekana wanaume wako serious kabisa kulalamikia maovu ya wanawake utadhani wao ni watakatifu au labda wenzetu maovu yao yamepitishwa
Dada mbona unayachukulia serious sana maisha ya jf? Mengi yanayoletwa humu ni kuchangamsha jukwaa tuu.

Dont take it seriously to point of giving you depression.

Unforgetable
 
Asante mkuu kwa kuukubali ukweli barikiwa
 
Kupinga sio vibaya, me kupinga haimaanishi ndio ntakuwa muovu, Hapana nasimamia ukweli na uhalisia, kama hakuna wema duniani jaribu kuwa mwema and vice versa is true usituaminishe maandiko kwenye kila kitu.
 
Na ni biblia gani hiyo iliyomruhusu mwanaume kufanya uzinzi na uasherati??

Watu wa JF ndiyo hawa hawa wa mitaani na haya mambo yanaongelewa hadi mitaani!!
 
Machungu yatabaki kwa watawaliwa..
 
Ni kweli kabisa.
Wanyama wote wenye akili ya karibu
Binadamu ni mfano wa Mungu na siyo wanyama na wala hatukuagizwa tufuate maisha ya wanyama bali tumewekewa sheria zetu sisi kama binadamu hivyo usijilinganishe na wanyama hata siku moja binadamu tuna maisha baada ya kifo ila wanyama hawana sasa kama hadi hapo bado haujaona tofauti kubwa kati ya wanyama na binadamu basi utakuwa na tatizo mahali
 
Kupinga sio vibaya, me kupinga haimaanishi ndio ntakuwa muovu, Hapana nasimamia ukweli na uhalisia, kama hakuna wema duniani jaribu kuwa mwema and vice versa is true usituaminishe maandiko kwenye kila kitu.
Chief huwezi ukatreat maandiko kama nguo, inayokufaa unachukua, isiyokufaa unatupa kule. EITHER YOU ARE ALL IN OR YOU ARE ALL OUT.
 
Naona uzi umejijadili wenyewe , naona sina cha kuchangia , namaliza kwa kusema "Funguo inayofungua milango yote ina thamani kubwa sana , inamilikiwa na wenye pesa nyingi, ila kufuli inayofunguliwa na kila funguo ni useless utaikuta jalalani"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…