King Mbappe
JF-Expert Member
- Jul 26, 2018
- 1,195
- 2,053
Wewe ndo umetumia mihemko hicho kitabu gani unachotumia sie wengine tusio kitumia, kujificha Kwa maandiko ni udhaufu ili kufanya justification yako uonevu. Kwanza hvo vtabu viliandikwa na wanaume ulitaka wasijipendelee wao, ni sawa na Mimi niandike kuhusu mambo ya usawa wa kijinsia kati ya wanaume na wanawake, lazima niipe favor jinsia yangu. Acheni kutafsiri maandiko vibaya mfyuuuuuu
Watu wanafanya uovu alafu wanakimbilia kujitetea na maandiko huu ni ujinga wa kupitiliza, umeshapewa uwezo wa kutambua baya na jema ni lipi lakini bado unakubali kuendeshwa eti kisa maandiko yanasema na mbaya zaidi wameelimika, sasa elimu ya kazi gani kama unashindwa kuyatumia maarifa kwenye maisha halisi kwa kufanya yanayostahili kwa haki? Nmekua nashuhudia baadhi ya wanawake wakinyanyasika wengine kwa kujua na wengine kwa kutokujua, imagine unaona mama yako akinyanyasika inauma sana kwakweli ni kitu ambacho huwa sikipendi milele yote.
Mke wa mjomba alimwambia baby nataka kwenda kusoma walau niwe na degree diploma haitoshi
Anko akajibu inatosha sana na ajira unayo hukuolewa kwangu kusoma siku utakayoamua kwenda masomoni beba kila kilichochako usirudi hapa. Mjadala ukafungwa
Mpaka Leo bibie yupo anatumikia taifa kupitia ualimu na ndoa pia
Mimi nafata data za kiuchunguzi wanaume mumezidiwa vingi na wanawake Kwa sasa angalia idadi hata ya vijana wakiume hovyo hovyo tu hawana mbele wala nyuma.
What a brave commentMarianah huu ndio Ulimwengu.
Ulimwengu wa pande mbili.
Giza na Nuru. Nuru inatawala giza.
Muumba na muumbaji.
Mtawala na mtawaliwa.
Masikini na Tajiri.
Mungu na Shetani.
Mwanaume na Mwanamke.
Mweupe na Mweusi. N.k.
Mwanamke yupo kundi la kutawaliwa. Hata afanye jambo gani zuri mtawaliwa ni mtawaliwa tuu. Atabaki kuwa mtumwa wa Mwanaume.
Utahangaika sana Kupambana na Nature.
Hilo lipo wazi hata kwa Viumbe wengine waliowengi.
Mwanamke akienda porini akikutana na Nyani au Sokwe hawezi kumtisha kwa lolote. Sokwe atamchukulia kama mwanamke tuu. Nyani atakuchukulia kama mwanamke tuu. Na ndivyo ilivyo. Wewe ni mwanamke utabaki kama mwanamke na utachukuliwa kama mwanamke.
Yaani tunaweza kusema. Mwanamke yupo upande dhaifu wakati Mwanaume yupo upande mkuu.
Hata Mungu pamoja ya kuwa hana Jinsia lakini Bado anaitwa Baba. Yaani mwenye nguvu, Mamlaka, Asiyekosea, Mtawala.
Mungu hawezi itwa Mama wala mwanamke kwa kuwa Mwanamke anasifa ya Kutawaliwa, Hana nguvu, anayekosea mara kwa mara, Anayeenda kila mwezi katika unajisi wake n.k.
Mwanamke pamoja na umuhimu wake lakini mpaka dunia inaisha atabaki kuonekana mkosaji siku zote.
Hata huko Ulaya wanapojitahidi kutetea haki zao lakini bado Mwanamke anachukuliwa kama kiumbe duni tuu.
Kuhusu Uovu. Dhambi ni dhambi haijalishi ni nani anaifanya.
Lakini Biblia inamtambua mwanamke kwa namna kadhaa. Moja ya namna hizo ni kuwa mwanamke ni kiumbe dhaifu sana.
Pia biblia uisemayo inamchukulia Mwanamke kama daraja la chini kabisa.
Moja, Biblia inamtaka mwanamke asihubiri mbele ya wanaume hasa wanaume halisi. Hii ni kutokana na kuwa Mwanaume hapaswi kuisikiliza sauti ya mwanamke bali mwanamke ndiye anapaswa kusikiliza sauti ya mwanaume.
Pili, Mwanamke maumbile yake yanamfinya na kumdunisha awapo kwenye makutano. mfano Biblia inamkataza Mwanamke aliyekatika siku zake kuingia mahali pa ibada. Yaani kanisani au msikitini.
Tatu, Mwanamke mchawi anatakiwa kuuawa. Lakini Biblia imenyamaza kuhusu mwanaume mchawi. Je haikujua kama kuna wanaume wachawi. Jibu ni hapana. Ilijua.
Lakini kwa vile Mwanamke yupo tabaka la chini kwa habari za jinsia ndio maana kawekewa sheria nyingi kuliko mtawala.
Wanaume ndio watawala ndio maana wanaweka sheria wazitakazo na zinazowanufaisha.
Hata Mungu kwa vile ndiye mtawala ndio maana akatuwekea sheria.
Wewe utabaki kulia lia humu lakini huna utakapofika. Ukirudi nyumbani utaosha vyombo, utapika, utafua kama sio zako ni za watoto. Utapangiwa muda wa Kurudi nyumbani. Yaani wewe umetawaliwa.
Kama hujanielewa hutanielewa tena.
kwa hio kama kitabu kimeandikwa na mwanaume manake si cha Mungu. na kwa maana hio wewe haukiamini.
Je, wewe humuabudu tena Mungu?
Napenda watu wa Data. Mkuu naomba hizo Data.
Tena hata ulete za Ulaya nitashukuru zaidi. Data zinazoonyesha kuwa Wanawake wamewazidi wanaume kwa mambo mengi.
Nikurahisishie dondoo utakazojikita.
●Kiuchumi
●Kijamii
● Kisiasa
● Kiulinzi na usalama
● Kiutamaduni.
Nakuruhusu hata nchi za Ulaya utumie kama Case Study.
Nakusubiri.
Dada mbona unayachukulia serious sana maisha ya jf? Mengi yanayoletwa humu ni kuchangamsha jukwaa tuu.
Dont take it seriously to point of giving you depression.
Unforgetable
Maandiko yapo very clear, hayajamruhusu binadamu yeyote kutenda dhambi (si mwanaume wala mwanamke)
Maandiko hayo hayo unayosema wanaume "wameyatumia vibaya" yapo straight forward mwenye kustawisha familia ni mwanamke (mithali inasema:mwanamke mpumbavu ataivunja nyumba yake kwa mikono yake)
Kama Mungu angetaka tuwe sawa sawa,tungeona katika maandiko wanawake wakiishi na wanaume zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja kama ilivyo kwa wanaume,(kwa imani zote unakuta mwanaume mmoja ana wanawake watatu wanne na kuendelea,na wote wanaishi pamoja pasipo tatizo kabisa)
Sasa fanya utafiti wako wako kwa kadri unavyoweza,ulete marejeo yanayokupa usawa katika mahusiano?HAKUNA!
Na ndiyo maana muoaji analazimika kuleta mahari kwa mwanamke,unajua ni kwa nini? Umewahi kujiuliza utamaduni huu una msingi gani?
Mwanamke anapokuwa cheap sana,thamani yake inashuka sana,na wanaume wakimtaka mwanamke kingono bila mafanikio,wengi wao humuheshimu zaidi mwanamke huyo na kuanza kumpigania ili wamuoe (thamani ya mwanamke iko mikononi mwake mwenyewe)
Hahaaa ungenitafta tu aisee
Mkuu mimi wala sipingi utofauti uliopo wa kiutawala kati ya mwanaume na mwanamke. Hoja yangu ni usahihi wa njia zilizotumiwa kuusimamisha huo utawala( maandiko matakatifu ).Vyovyote iwavyo. Asili inaonyesha Mwanaume ndiye mtawala.
Jamii karibu zote duniani mwanaume ndiye mtawala.
Hivyo yeye ndiye hubuni sheria kulingana na vile atakavyoona yeye.
Hata mwanamke kupewa haki ni matokeo ya baadhi ya wanaume kuona ipo haja ya kuwapa haki hao wanawake.
Wanawake hawana uwezo wa kukaa pamoja na kuamua kupigania haki zao bila msaada wa mwanaume. Hiyo ni nature mkuu.
Huyo Marianah anajaribu kufanya jaribio lililofeli pale Edeni lililofanywa na Mama yetu Hawa au Eva.
Eva alitaka kumpindua Adamu kisiri ili afanane na Mungu. Kumbuka Adamu aliumbwa kwa mfano wa Mungu wakati Eva au Hawa akiumbwa kwa Mfano wa Adamu.
Kama jinsi Wanadamu wanavyohangaika kuwa sawa na Mungu lakini inashindikana ndivyo wanawake wanavyojitahidi kuwa sawa na Mwanaume na inashindikana.
mwanamke atabaki kutawaliwa siku zote mpaka aingie kaburini kwenye huo usawa.
sijakataa usemacho, nauliza wewe unamwabudu Mungu humuabudu?Achana na Ku abudu na kumwamini Mungu vitabu hivo kuandikwa na mwanadamu hasa mwanaume vina bias, zamani wanawake walikuwa hawahesabiwi kuwa ni watu hata kwenye sensa ilikuwa ni wanaume. Unataka kusema huko kuandikwa siilikuwa Ku favor malengo ya kijamii ya wakati ule? Jiongezeni aisee
Mkuu,, wapo pia wanaume waliosahau uanaume wao na majukumu yao hao nao unawaongeleaje??Uzi huu nimesoma natoka kuamka akili haijaweza ku digest mambo ila ngoja niweke neno.
Kinacho peleka yote ni mwanamke kusahau wanamke wake na majukumu yake.
sijakataa usemacho, nauliza wewe unamwabudu Mungu humuabudu?
Umesahau wanaume wanakufa vitani, kwenye mashimo ya migodi. Sisi ndio wanaume. Mtuache tu jamani.
Mkuu huyu aliongea tu kutetea chama lakini siyo kweli wanawake wanawazidi wanaume kwenye nyanja hizo...Napenda watu wa Data. Mkuu naomba hizo Data.
Tena hata ulete za Ulaya nitashukuru zaidi. Data zinazoonyesha kuwa Wanawake wamewazidi wanaume kwa mambo mengi.
Nikurahisishie dondoo utakazojikita.
●Kiuchumi
●Kijamii
● Kisiasa
● Kiulinzi na usalama
● Kiutamaduni.
Nakuruhusu hata nchi za Ulaya utumie kama Case Study.
Nakusubiri.
Nilijipa muda kidogo, I am happy you are back madam.
I personally missed you.