Hivi ni kweli wanaume hawapendi kuombwa hela?

Hivi ni kweli wanaume hawapendi kuombwa hela?

Hawa bwana waache kama walivyo, unamuoa akiwa hana mishe hata moja, mbele wala nyuma. Baada ya muda kidogo, siwezi kuwa mama wa nyumbani, nipe mtaji....

Mimi nilipata ninachofanya kwenye ndoa? Usitafute cha kufanya tangu uko kwenu, uje unisumbue mimi ukiwa na meno yako 32? Kweli? Kisha uje uniambie PESA YA MWANAMKE ni ya mwanamke. Kulea hulei tena kisa uko busy, kuchangia gharama za maisha nyumbani hutaki...

Achana nao hao kaka. We fata misaafu inavyozungumza kuhusu wao, ukitaka kuendesha gari kwa kutunga MANUALS zako utaiua gari, fuata ya manufacturer ili gari yako idumu.....soma manuals alizotoa mtengenezaji wa hii dunia, ameelezea kila kifaa na kazi yake mule

Kuna wale wa kwenye ndoa na hawa wengine wa kuibaiba mkuu,

Tofauti yao umeijua,
 
Kuombwa Pesa sio dhambi.

Ila Kupiga mzinga ndio dhambi.

Binafsi nilikua nachukia sana mwanamke anayeomba omba hela , ila nilikuja kugundua Wanawake na Pesa wameunganishwa na uzi mmoja .


Usisubiri Kuombwa
 
Suala sio kuombwa pesa bali timing.
Haiwezekani tu mara tu mkipeana namba masaa machache unaaikia baby nikuambie kitu?

Kuna demu nilionana naye kwa marq ya kwanza aaivyokuwa na aibu akaanza;

Birthday yangu kwasho kutwa naomba pesa ya;
1. Kusuka
2. Viatu
3. Halafu utaandaa chakula hotel flani.
4. Sina ngio nzuri

Pili December nasafiri kwwnda... niandalie ticket ya ndege

Haraka haraka hapa ni zaidi ya 1ml
Hapa hamjafikiana kuwa mtakuwa wapenzi au wachumbq.
Huu ni ufala, kikosa hwkima na aibu.

Kama angeenda hatua kwa hatua angepata zaidivya hizi
Alitisha kwa kweli

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hawa viumbe wanependa hela...we toa tu mzee la sivyo kuna wazeya huwa hawaangalii kesho wenyewe wanatoa tu watakubandulia daily
 
Kuomba omba ni aibu,kunaondoa thamani na utu,kunakinaisha sana pia. Mwanaume kama anakupenda atakuhudumia tu kama anacho, ila sio kuomba omba kama umekatika mikono

Hata kwa urafiki wa kawaida ukiwa mtu wa kuomba omba kadri siku zinavyokwenda utaona watu wanakuescape taratibu taratibu
 
Hapa ndo pagumuu.... Kuna mtu nilimuacha sababu alikuwa hajiongezi na mimi kumuomba hapana.... Basi siku moja nikamwambia it's ova.... Akauliza sababu nini, nikamwambia sitoitaja sababu hata unikate miguu... Alilalama weeee nkamwacha aende.


Ajawai kukupa hata Mia?
 
Hapa ndo pagumuu.... Kuna mtu nilimuacha sababu alikuwa hajiongezi na mimi kumuomba hapana.... Basi siku moja nikamwambia it's ova.... Akauliza sababu nini, nikamwambia sitoitaja sababu hata unikate miguu... Alilalama weeee nkamwacha aende.
Mlikuwa wachumba tu lakini? Wengine usipowaambia wanauchuna tu nawao
 
Back
Top Bottom