GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Barua ya wazi kwa Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Sanaa Utamaduni na Michezo
Kwako Dkt. Hassan Abbas
Hatuna shaka kwamba wewe nikiongozi makini na unayefuatilia nakusimamia mambo kwa weledi mkubwa.
Hatuna shaka na Utendaji wako na msimamo wako katika kutetea aki na Maslahi ya vilabu vya soka nchini. Tunakupongeza Sana kwa hilo.
Mh.Katibu Mkuu, DktA.bbas tumelazimika kuandika barua hii ya wazi ikufikie ili walau upate kuangalia kwa ukaribu pia suala hili tutakalo lieleza katika barua hii.
Tunaamini kwa nafasi yako umepata kusikia malalamiko mengi ya Klabu ya Yanga kwenye Shirikisho la Soka Tanzania(TFF). Kwa kipindi kirefu Yanga tumekuwa tukilalamikia masuala mbalimbali lakini TFF imekuwa ikiyapuuza na kunyima haki ya Klabu yetu kwa sababu ambazo haziwekwi wazi.
Hatuna sababu ya kukuandikia mlolongo wa kesi tangu msimu uliopita, lakini lengo la barua hii ya Wazi kwako ni kuomba ulitupie macho Sakata la Mkataba wa Mchezaji Raia wa Ghana Bernard Morrison na Simba SC ambao sisi kama klabu tumeuona una mapungufu makubwa ya kuufanya kuwa sio halali.
Oktoba1,2020,tukiwa kama wadau kwenye soka la Tanzania, tulipeleka malalamiko yetu TFF juu ya usajili uliokiuka kanuni za Mchezaji MORRISON katika Klabu ya Simba.
Kwani Mkataba uliopo haukuwa na saini za upande wa Klabu jambo ambalo nikinyume na kanuni za usajili za TFF. Lakini tangu wakati huo, hadi sasa TFF imekaa kimya na zaidi wanawatishia viongozi wetu kuwafungia juu ya Suala hilo.
Kwa barua hii, tunaomba mkono wa Serikali katika hili na tunaamini ofisi yako kupitia watendaji wako au wewe mwenyewe unaweza kulifuatilia na kutoa majibu kwa wadau kama Serikali kwakuwa Serikali yetu haipendi kuona uonevu na imejipambanua katika kusimamia haki.
Ahsante Sana
Wako watiifu
Wanachama wa Yanga SC
Chanzo: yangawhatssap_makao makuu
========
Hivi Yanga SC kupitia Wasemaji wenu wa hovyo hovyo, wanaogombana na wasiopendana kila Siku Hassan Bumbuli na Antony Nugaz bila kumsahau Makamu Mwenyekiti wenu Tumbo Tumbo Fredrick Mwakalebela si mlituaminisha kuwa mmeshaishtaki Simba SC huko CAS na kwamba Kibano kinaenda Kutuangukia na Morisson hatocheza? Sasa mbona leo mnakimbilia tena Serikalini ambapo hata Kisheria tena zile za FIFA hazitaki mambo ya Mpira kupelekwa Serikalini? Mkiambiwa hamna Akili mnanuna.
Na kama hamna matokeo hadi hivi sasa ya huko Arusha ni kwamba Simba SC tunaongoza kwa Goli 7 kwa 0 dhidi ya Coastal Union. Watakoma leo!