Hivi ni mimi tu naona kama miaka inakimbia sana(nyakati zinapita haraka sana)

Hivi ni mimi tu naona kama miaka inakimbia sana(nyakati zinapita haraka sana)

DUBULIHASA

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2016
Posts
4,446
Reaction score
8,215
Salamu wakuu, niende moja kwa moja kwenye maada.

Hii kitu huwa najiuliza sana. Hivi kwa nini nyakati zinakimbia sana, kwa mfano kutoka mwaka mmoja kwenda mwingine naona unaisha haraka sana, mwezi mmoja kwenda mwingine, vile vile wiki moja kwenda nyingine.

Hebu just imagine mtu kama Magufuli 2015 aligombea urais akashinda then akaongoza miaka mitano, then akagombea 2020 akashinda na akaongoza miaka miwili then akafariki. Sasa kinachonishangaza mimi toka hiyo 2015 mpaka leo it sounds like juzi tu. Ile moment ya uchaguzi wa CCM na ukawa kisaikolojia kwangu hainijii kichwani kama ni moment ya miaka nane iliyopita but inasound kama ni mwaka juzi flani hivi.

Halafu Kuna moment zingine huwa zinanifikirisha personally na kuona kama nyakati zinakimbia sana tofauti na fikra zangu, kwa mfano nikiwa nasoma Sekondari msimu wa 2003/2004 timu ya Arsenal ilibeba kombe la ligi kuu Uingereza. Hii moment naikumbuka sana kwa sababu Arsenal ni timu yangu pendwa. Kitu cha ajabu kwangu kichwa changu kinashindwa ku make sense kama ile 2003/2004 mpaka leo ni miaka ishirini imepita. Sometime huwa naona kama hii dunia ina short spani, imekuwaje miaka ishirini inasound muda mfupi kiasi hicho wakati miaka ishirini iliyopita kumbe ni kama juzi tu.

Hii sijajua kwa wengine lakini mimi binafsi nikilala usiku let say masaa 7 au 8. Nikishalala usingizi na kuamka asubuhi na feel kama nimelala masaa mawili, in short usiku pia naona kama unakua mfupi sana. Halafu pia hata mchana nikienda kazini, nikipiga mishe mishe na kufika jioni kurudi nyumbani na feel kama huko job sijakaa muda mrefu sana, in short nahisi kama siku pia inakua fupi sana....... Pia kutoka jumatatu mpaka ijumaa siku zinaenda kwa spidi, yaani jumatatu inaikamata ijumaa haraka sana. Halafu pia weekend (jumamos na jumapili) inaisha haraka pia. Hata weekend inaisha then kuikamata jumatatu kwenda ijumaa nayo inaisha haraka sana.

Wakuu hivi hili jambo ni kwa nini? Hivi ni mimi tu huwa nali observe hili jambo?
 
Salamu wakuu, niende moja kwa moja kwenye maada.


Hii kitu huwa najiuliza sana. Hivi kwa nini nyakati zinakimbia sana, kwa mfano kutoka mwaka mmoja kwenda mwingine naona unaisha haraka sana, mwezi mmoja kwenda mwingine, vile vile wiki moja kwenda nyingine...
Hii hali nilidhani naiona mimi tu kumbe tupo wengi, kuna muda mpka naogopa nahisi labda nipo ndotoni au nakimbilia kifo😂😂😂😂
 
Mkuu kumbe na ww hiyo kitu una observe!!!!! Mi huwa nahisi maybe ni mm kisaikolojia cko vzur
Nakumbuka vizuri Kikwete ndio ameingia madarakani alikuja kwenye mji nilokuepo nasoma shule na kwenye moja na mbili akatupa mikono tulokuwepo front, huwa naona kama week ilopita tu na ile arsenal inapigwa mbili moja na Barca 2006! Daamn mpaka leo nakumbuka hayo maumivu ajabu sai ni miaka mingapi sijui ya kwenye calendar. Vitu ni vingi!
 
nakumbuka vizuri Kikwete ndo ameingia madarakani alikuja kwenye mji nilokuepo nasoma shule na kwenye moja na mbili akatupa mikono tulokuepo front, hua naona kama week ilopita tu na ile arsenal inapigwa mbili moja na barca 2006! daamn mpk leo nakumbuka hayo maumivu ajabu sai ni miaka mingapi sijui ya kwenye calendar. vitu ni vingi!
Mkuu kumbe ww ni shabiki wa Arsenal... 2004 Arsenal alichukua ubingwa so ni miaka ishirini imepita. Aisee it makes me crazy
 
Mimi kinachofanya nione miaka inakimbia sana ni umri wa mwanangu. Ni juzi tu hapo, nakumbuka kila kitu, I feel him akiwa kachanga kabisa.

Leo ana miaka 16, huwa nashangaa sana. I can tell, naona kama ndiyo kwanza ana miaka mitatu. Lakini sasa ni kijana Mkubwa.
Halafu huyo mtoto unatamani hata akienda shule umsindikize ukihisi bado ni mdogo kumbe ni wewe unamwoma mdogo but yeye anajiona mkubwa
 
Siamini juzi tu 2013 nilipanga ifikapo 2020 ntakuwa nmetimiza malengo yangu na kula kuku kwa mrija, miaka ilivyokimbia hao kuku nawala kwa macho tu haloo.

Hiki kizazi cha.com kuna namna kimefanya dunia imeanza mbio kujibust kwenda nacho sawa
 
Siamini juzi tu 2013 nilipanga ifikapo 2020 ntakuwa nmetimiza malengo yangu na kula kuku kwa mlija,miaka ilivyokimbia hao kuku nawala kwa macho tu haloo.
Hiki kizazi cha.com kuna namna kimefanya dunia imeanza mbio kujibust kwenda nacho sawa
Sasa mkuu shangaa kidogo

2013 ndo nimeajiriwa rasmi baada ya kumaliza chuo 2012. Mpaka leo nashindwa kuamini kama nimefanya kazi miaka 10
 
Asilimia kubwa ya wanao experience hichi miaka kwenda taratibu ni wale ambao wapo under pressure na muda. Kwa mfano, wanafunzi, wanavyuo, wafungwa, n.k.

Ukiwa under pressure na muda lazima tu kuna tafsiri zitapelekwa kwenye ubongo, (wataalam wanafahamu) na kupelekea hiyo hali. Kwa mfano, ukiwa una safari unayoipenda sana, may be ndio mara ya kwanza kupanda ndege, utatamani pakuche lakini kila ukiamka utaona muda bado.

Kwa ufupi tu naona muda wa kueleza nakosa.
 
Back
Top Bottom