Hivi ni mimi tu naona kama miaka inakimbia sana(nyakati zinapita haraka sana)

Hivi ni mimi tu naona kama miaka inakimbia sana(nyakati zinapita haraka sana)

Mtoa mada ulichoandika ni sahihi na watu wote wanaiona hii hali, mimi katika maoni yangu nadhani tech katika mawasiliano imechangia hii hali kwa maana maisha yamekuwa na speed sababu too much info zina flow na hizi simu zimechangia unaweza kujikuta unatumia sana simu kwa siku ni ujumla wa tech ya mawasiliano inafanya na maisha yetu kuwa ya haraka huko zamani miaka ya 80-90 life ilikuwa slow sana sababu hatukuwa na tech hii ya kupata habari kwenye kiganja na hii hali hali toka 2000 ndio tunahisi siku zinakimbia sana na tech ya mawasiliano imeanza kukua miaka hiyo ndio maana nasema inawezekana hivi vitu viwili vinafanya hii hali.
You're spot on.
 
Time is slow when you wait
Time is fast when you're late
Time is deadly when you're sad
Time is short when you're happy
Time is endless when you're in pain
Time is long when you feel bored
Time is beautiful when you're in love
Everytime,Time is determined by your feelings and your physiological conditions and not by clocks.
 
Miaka inaenda resi sio uongo, kuna vidogo vya mtaani kwetu juzi tu hapa vilikuwa vinanipa shikamoo nashangaa sasa ghafla bin vuu vimekuwa vikubwa mpaka vingine shetani anataka aingilie kati aniforce nijipakulie minyama

Dah shetani apishilie mbali
 
Kuona miaka inakimbia sana ni dalili ya uzee.

Ukiwa na miaka miwili, mwaka mmoja ni nusu ya maisha yako, 50% ya maisha yako, hivyo utauona mwaka mmoja ni mrefu sana.

Ukiwa na miaka 100, mwaka mmoja ni 1/100 ya maisha yako, 1% tu.

Jinsi unavyozidi kuzeeka ndivyo miaka inavyoonekana kwenda kwa kasi zaidi.

Hakuna mtoto anayesema mwaka huu umepita kwa kasi sana. Hizi ni tabia za watu wanaoelekea au walio kwenye uzee.
Mkuu, natofautiana na wewe kidogo. Siyo dalili ya uzee wala kuzeeka bali ni dalili ya binadamu kujitambua, kukomaa na kumudu zaidi mazingira yake. This is Psychology 101.

Kwa mtoto, almost everything ni new, mysterious and darkly. Ndiyo maana mtoto mdogo anaweza ^kupotelea^ sebuleni nyumbani, lakini mtu mzima kimawazo yuko virtually kila mahali duniani, and relatively safe.
 
Ukiwa una tabia ya kuugawanya mwaka kulingana na jukumu fulani lazima iwe hivyo ,mfano mwez fulani mpka mwez fulani nitafanya jambo fulani, lazma tu uje kushtuka mda umekimbia ,zaman ulikua mtoto huna majukumu au ulikuwa hauna tabia ya kugawanya majukumu ndani ya mda ,mda mwingi ulikua unapoteza kwenye michezo ,ndio maana ulikua hauoni sku zinakimbia.
 
Salamu wakuu, niende moja kwa moja kwenye maada.

Hii kitu huwa najiuliza sana. Hivi kwa nini nyakati zinakimbia sana, kwa mfano kutoka mwaka mmoja kwenda mwingine naona unaisha haraka sana, mwezi mmoja kwenda mwingine, vile vile wiki moja kwenda nyingine.

Hebu just imagine mtu kama Magufuli 2015 aligombea urais akashinda then akaongoza miaka mitano, then akagombea 2020 akashinda na akaongoza miaka miwili then akafariki. Sasa kinachonishangaza mimi toka hiyo 2015 mpaka leo it sounds like juzi tu. Ile moment ya uchaguzi wa CCM na ukawa kisaikolojia kwangu hainijii kichwani kama ni moment ya miaka nane iliyopita but inasound kama ni mwaka juzi flani hivi.

Halafu Kuna moment zingine huwa zinanifikirisha personally na kuona kama nyakati zinakimbia sana tofauti na fikra zangu, kwa mfano nikiwa nasoma Sekondari msimu wa 2003/2004 timu ya Arsenal ilibeba kombe la ligi kuu Uingereza. Hii moment naikumbuka sana kwa sababu Arsenal ni timu yangu pendwa. Kitu cha ajabu kwangu kichwa changu kinashindwa ku make sense kama ile 2003/2004 mpaka leo ni miaka ishirini imepita. Sometime huwa naona kama hii dunia ina short spani, imekuwaje miaka ishirini inasound muda mfupi kiasi hicho wakati miaka ishirini iliyopita kumbe ni kama juzi tu.

Hii sijajua kwa wengine lakini mimi binafsi nikilala usiku let say masaa 7 au 8. Nikishalala usingizi na kuamka asubuhi na feel kama nimelala masaa mawili, in short usiku pia naona kama unakua mfupi sana. Halafu pia hata mchana nikienda kazini, nikipiga mishe mishe na kufika jioni kurudi nyumbani na feel kama huko job sijakaa muda mrefu sana, in short nahisi kama siku pia inakua fupi sana....... Pia kutoka jumatatu mpaka ijumaa siku zinaenda kwa spidi, yaani jumatatu inaikamata ijumaa haraka sana. Halafu pia weekend (jumamos na jumapili) inaisha haraka pia. Hata weekend inaisha then kuikamata jumatatu kwenda ijumaa nayo inaisha haraka sana.

Wakuu hivi hili jambo ni kwa nini? Hivi ni mimi tu huwa nali observe hili jambo?
Majukumu yakiongezeka Hali hiyo lazima itokee
 
Mimi kinachofanya nione miaka inakimbia sana ni umri wa mwanangu. Ni juzi tu hapo, nakumbuka kila kitu, I feel him akiwa kachanga kabisa.

Leo ana miaka 16, huwa nashangaa sana. I can tell, naona kama ndiyo kwanza ana miaka mitatu. Lakini sasa ni kijana Mkubwa.
Hongera sana
 
2010 nilimzika baba yangu,kila nikilala usiku naota nafanya mitihani,mpaka sasa kila siku naona 2010 ni kama juzi
 
Salamu wakuu, niende moja kwa moja kwenye maada.

Hii kitu huwa najiuliza sana. Hivi kwa nini nyakati zinakimbia sana, kwa mfano kutoka mwaka mmoja kwenda mwingine naona unaisha haraka sana, mwezi mmoja kwenda mwingine, vile vile wiki moja kwenda nyingine.

Hebu just imagine mtu kama Magufuli 2015 aligombea urais akashinda then akaongoza miaka mitano, then akagombea 2020 akashinda na akaongoza miaka miwili then akafariki. Sasa kinachonishangaza mimi toka hiyo 2015 mpaka leo it sounds like juzi tu. Ile moment ya uchaguzi wa CCM na ukawa kisaikolojia kwangu hainijii kichwani kama ni moment ya miaka nane iliyopita but inasound kama ni mwaka juzi flani hivi.

Halafu Kuna moment zingine huwa zinanifikirisha personally na kuona kama nyakati zinakimbia sana tofauti na fikra zangu, kwa mfano nikiwa nasoma Sekondari msimu wa 2003/2004 timu ya Arsenal ilibeba kombe la ligi kuu Uingereza. Hii moment naikumbuka sana kwa sababu Arsenal ni timu yangu pendwa. Kitu cha ajabu kwangu kichwa changu kinashindwa ku make sense kama ile 2003/2004 mpaka leo ni miaka ishirini imepita. Sometime huwa naona kama hii dunia ina short spani, imekuwaje miaka ishirini inasound muda mfupi kiasi hicho wakati miaka ishirini iliyopita kumbe ni kama juzi tu.

Hii sijajua kwa wengine lakini mimi binafsi nikilala usiku let say masaa 7 au 8. Nikishalala usingizi na kuamka asubuhi na feel kama nimelala masaa mawili, in short usiku pia naona kama unakua mfupi sana. Halafu pia hata mchana nikienda kazini, nikipiga mishe mishe na kufika jioni kurudi nyumbani na feel kama huko job sijakaa muda mrefu sana, in short nahisi kama siku pia inakua fupi sana....... Pia kutoka jumatatu mpaka ijumaa siku zinaenda kwa spidi, yaani jumatatu inaikamata ijumaa haraka sana. Halafu pia weekend (jumamos na jumapili) inaisha haraka pia. Hata weekend inaisha then kuikamata jumatatu kwenda ijumaa nayo inaisha haraka sana.

Wakuu hivi hili jambo ni kwa nini? Hivi ni mimi tu huwa nali observe hili jambo?
Mimi sasa ndo naiona miaka ni kama inakimbizwa. Ipo kasi sana
 
Ni kawaida ukianza kulipa bills zako mwenyew lazma uone muda unakimbia jarbu kumuulza mtoto wa darasa la 7 huu mwaka anauonaje asipokwambia n kama miaka miwil mana hata moko hawajafanya
 
Katika suala la uaminifu kamili, muda ndio unashika namba moja katika asili. Muda haukawii wala hauchelewi.

Pili, suala la kupita kwa muda ni psychological. Mtu mwenye jambo la maana la kufanya au kitu anachopenda sana, ama hata kitu fulani cha hatari kinachoshughulisha mawazo, hapo ubongo huwa katika hali ya umakini ama fokasi almost 100% na hapo mtu husika kwa nadra hutambua kupita kwa wakati.

Siyo mara chache, katika nyakati kama hizo, wengi wamejikuta wakisema, ^Heee! Kumbe giza limeingia?^ au ^Kumbe kumekucha?^ nk.

Kwa ufupi, mtu anapokosa kitu chochote cha kushughulisha ubongo wake na mwili wake, muda (ambao kimsingi ni definition ya uhai hasa), huonekana kujivuta sanaaa kama mipira ya Malaysia.

Critical application: Kuna baadhi ya watu wanaosema, ^Aseee! Hata kama mbinguni ni halisi, baada ya mrefu kupita hivi hatutafikia hatua ya kupachoka (kuwa bored)?^

I'm happy kwamba majibu ya maswali yote muhimiu yanayomshughulisha na kumtaabisha mwanadamu, tunaweza kuyapata hapa hapa duniani.

Mbinguni (au, more accurately, katika Nchi Mpya), watu hawatakuwa na usumbufu wa kisaikolojia unaosababishwa na shinikizo la kupita ama kuchelewa kwa muda. Muda hauta-define tena uhai wetu wala maisha yetu.

Bandiko hili limfundishe mwanadamu yeyote kwamba hakika kama ilivyo asubuhi, muda ni mchache sana na mambo ni mengi mno, chagua yale tu yenye mwelekeo wa moja kwa moja katika kutimiza lengo kuu la maisha hapa duniani na maisha yajayo. Na hii ni sababu kuu ya pili kwa nini muda huonekani kutoweka haraka.

As they rightly say, BEFORE YOU KNOW IT, IT WOULD BE ALREADY TOO LATE!

^siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja^ ~ 2 Petro 3:8

NB: An important point to note: wale wanaosema, ^Mbona tukio fulani na fulani la miaka 5, 10 au 20 iliyopita ni kama tu limetokea jana,^ wakumbuke kwamba hilo linahusiana na namna ubongo unavyotunza kumbukumbu.

Our brain does not recon or store memories in terms of hours or kilometers that it can physically perceive the elapsed time. They are all images coded and compacted and mostly dormant within our being. These images once awakened, years of corresponding events seem as though just moments or few days.
Kwa kuongezea,time perception inatofautiana kulingana na umri.Kadri umri unavyosonga kelekea utu uzima ndivyo unavyoona muda unakimbia.Ukiwa na umri Mdogo unaona kuwa you have all the time.
 
Ni kwa sbb ya teknolojia..kila kitu kipo kiganjani..habari ya uchaguzi ya 2015 inaongelewa mpk leo kwenye mitandao ya kijamii unaweza google habari za zamani na kuhisi ni za jana tuu...hivyo kwny hisia kumbukumbuku zinaendelea kuwepo na ubongo unakua updated..vivyo hivyo taarifa ya mechi zipo na zipo reviewed kila mara sehemu mbalimbali...hivyo kupelekea ubongo kutofuta memory hizo kwa haraka na kuhisi ni jana tuu..n.k n.k n.k
 
Back
Top Bottom