Hivi ni mimi tu naona kama miaka inakimbia sana(nyakati zinapita haraka sana)

Dalili za kuja Bwana Yesu. Muda unafupishwa ili wengi waingie Mbinguni. Muda ukiwa mrefu wengi watakosa Mbingu
 
Kuona miaka inakimbia sana ni dalili ya uzee.

Ukiwa na miaka miwili, mwaka mmoja ni nusu ya maisha yako, 50% ya maisha yako, hivyo utauona mwaka mmoja ni mrefu sana.

Ukiwa na miaka 100, mwaka mmoja ni 1/100 ya maisha yako, 1% tu.

Jinsi unavyozidi kuzeeka ndivyo miaka inavyoonekana kwenda kwa kasi zaidi.

Hakuna mtoto anayesema mwaka huu umepita kwa kasi sana. Hizi ni tabia za watu wanaoelekea au walio kwenye uzee.
 
Mkuu hii point nimeielewa nakumbuka mimi chuo miaka mitatu nahisi nilikuwa nimekaa muda mrefu chuoni.... Kuna mtoto wa dada yangu niliambiwa kamaliza chuo mwaka jana nilishangaa iweje amemaliza chuo wakati juzi tu alikuwa form four
 
Vitabu vinavyoaminika vya dini!! Vimeandika hivyo

Kuwa siku za mwisho siku zitaenda haraka sana na wameeleza mwaka utakuwa kama mwezi, mwezi kama wiki, wiki kama siku, siku kama saa, saa kama dk, dk kama upepo

Masiku ya mwisho hayaa, juzi tu ulikuwa mwezi wa kwanza et!! Leo tumeugawa mwaka ni hatari kwa Kweli
 

Kweli mkuu mtoto wa mwaka mmoja anaona mwaka juzi ni kitambo sana
 
Uko sahihi Kaka, mimi leo nilikuwa naangalia picha za 2016 ni kama juzi tu na sijaona tofauti yoyote na sasa. Pia mwaka huu 2023 ni kama tumeuanza mwezi jana tu hata nikipita katika records book yangu ya kikazi.
 
Uko sahihi Kaka,mimi leo nilikua naangalia picha za 2016 ni kama juz tu na sijaona tofauti yoyote na sasa. Pia mwaka huu 2023 ni kama tumeuanza mwezi jana tu hata nikipita katika records book yangu ya kikazi.
Mkuu just imagine Magufuli mpaka anafariki ameongoza kama miaka saba, kiti cha urais amekikalia miaka saba. Mi records zangu kichwani zina sense kama aliongoza miaka mitatu then akafariki
 
Mbona vitabu vya dini vimeandika haya

Ni maandiko yanatimia mkuu, haihitaji elimu yeyote ya ziada kujua kwamba miaka inaenda haraka Sana

Zamani ilikuwa kuumaliza mwaka ni shughuli pevu ila sasa Hadi unashangaa

Sad enough haya mabadiliko yanatokea kwa ghafla sana
 
Mtoa mada ulichoandika ni sahihi na watu wote wanaiona hii hali, mimi katika maoni yangu nadhani tech katika mawasiliano imechangia hii hali kwa maana maisha yamekuwa na speed sababu too much info zina flow na hizi simu zimechangia unaweza kujikuta unatumia sana simu kwa siku ni ujumla wa tech ya mawasiliano inafanya na maisha yetu kuwa ya haraka huko zamani miaka ya 80-90 life ilikuwa slow sana sababu hatukuwa na tech hii ya kupata habari kwenye kiganja na hii hali hali toka 2000 ndio tunahisi siku zinakimbia sana na tech ya mawasiliano imeanza kukua miaka hiyo ndio maana nasema inawezekana hivi vitu viwili vinafanya hii hali.
 
Kwahiyo hata stop watch timer nayo inakimbia zaidi?

Kule Tanga kuna wavuta bangi walikuwa wakishapuliza bangi zao kwenye Mwembe jioni basi wanaona sura ya baba wa Taifa, na nchi nzima tukaamishwa hivyo.

Hizi ni illusion zenu tu.
 
Mkuu Acha tu, nina mawili:

1. Juzi kuna katoto ka dada yangu nilikatandika bakora baada ya kukakuta kametoroka darasani (alikuwa darasa la tatu) na kwenda kupopoa maembe kwenye miembe ya kijijini ambayo ilikuwa inakatazwa kufanya hivyo na kjjiji chenyewe. Leo, kamekuja kunitembelea likizo hii eti kako kidato cha tatu (form 3). Mshangao nilioupara sio wa nchi hii.

2. Nina rafiki tulikuwa pamoja chuo ingawa kozi tofauti. Tunahangaika na maisha haya mkoa mmoja wilaya tofauti, tulikutana katika sherehe za mkoa za mei mosi. Wakati wa zawadi nikasikia jina lake kama mkuu bora wa shule.....nikashangaa. Baadae nikamuuliza kwani umeshakuwa mkuu wa shule?!!! Akanijibu ndiyo amekuwa hivyo kwa miaka mitano sasa.....nikaduwaa nikijua ananidanganya maana ni juzi tu tumetoka chuo. Mh, nilipojadiliana nae muda tuliomaliza chuo kumbe ni 2013.....eti imeshapita miaka 10. Serious?!!!! Ile juzi imeshakuwa 10 years?!!!!!!!!! Hapana aisee.?.
 
Mkuu haya maisha we acha tu. Mimi huwa naona sina maisha mazuri lakini bado najipa hope kwamba one day nitatoboa, lakini kuna mshikaji tena close friend ni mbunge. Sasa huwa najiuliza huyu jamaa ni mbunge wakati juzi kati tulikua tunakunywa wote uji secondary
 
Katika suala la uaminifu kamili, muda ndio unashika namba moja katika asili. Muda haukawii wala hauchelewi.

Pili, suala la kupita kwa muda ni psychological. Mtu mwenye jambo la maana la kufanya au kitu anachopenda sana, ama hata kitu fulani cha hatari kinachoshughulisha mawazo, hapo ubongo huwa katika hali ya umakini ama fokasi almost 100% na hapo mtu husika kwa nadra hutambua kupita kwa wakati.

Siyo mara chache, katika nyakati kama hizo, wengi wamejikuta wakisema, ^Heee! Kumbe giza limeingia?^ au ^Kumbe kumekucha?^ nk.

Kwa ufupi, mtu anapokosa kitu chochote cha kushughulisha ubongo wake na mwili wake, muda (ambao kimsingi ni definition ya uhai hasa), huonekana kujivuta sanaaa kama mipira ya Malaysia.

Critical application: Kuna baadhi ya watu wanaosema, ^Aseee! Hata kama mbinguni ni halisi, baada ya mrefu kupita hivi hatutafikia hatua ya kupachoka (kuwa bored)?^

I'm happy kwamba majibu ya maswali yote muhimiu yanayomshughulisha na kumtaabisha mwanadamu, tunaweza kuyapata hapa hapa duniani.

Mbinguni (au, more accurately, katika Nchi Mpya), watu hawatakuwa na usumbufu wa kisaikolojia unaosababishwa na shinikizo la kupita ama kuchelewa kwa muda. Muda hauta-define tena uhai wetu wala maisha yetu.

Bandiko hili limfundishe mwanadamu yeyote kwamba hakika kama ilivyo asubuhi, muda ni mchache sana na mambo ni mengi mno, chagua yale tu yenye mwelekeo wa moja kwa moja katika kutimiza lengo kuu la maisha hapa duniani na maisha yajayo. Na hii ni sababu kuu ya pili kwa nini muda huonekani kutoweka haraka.

As they rightly say, BEFORE YOU KNOW IT, IT WOULD BE ALREADY TOO LATE!

^siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja^ ~ 2 Petro 3:8

NB: An important point to note: wale wanaosema, ^Mbona tukio fulani na fulani la miaka 5, 10 au 20 iliyopita ni kama tu limetokea jana,^ wakumbuke kwamba hilo linahusiana na namna ubongo unavyotunza kumbukumbu.

Our brain does not recon or store memories in terms of hours or kilometers that it can physically perceive the elapsed time. They are all images coded and compacted and mostly dormant within our being. These images once awakened, years of corresponding events seem as though just moments or few days.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…