Hivi ni nani aliekata mipaka ya nchi hizi?

Hivi ni nani aliekata mipaka ya nchi hizi?

6 Pack

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2022
Posts
2,819
Reaction score
5,996
Salam wana jamii,

Wakuu naomba mwenye ujuzi wa mambo ya mipaka ya nchi mbalimbali aje anipe muongozo wa vigezo vilivyotumika kuzipendelea baadhi ya nchi kwa kuzipa ardhi kubwa, na kuzikomoa zingine kwa kuzipa ardhi ndogo.

Ukiangalia namna nchi ya China ilivyopendelewa huku majirani zake Cambodia, Vietnam, Nepal nk wakipewa viji ardhi vidogo mno ambavyo vingine vinaonekana kama ni vichochoro tu vya kutokea Thailand kwenda China, hii inatafakarisha sana, na hapo bado China itadai baadhi ya nchi zingine hapo bembeni yake ni ardhi yake.

Nashindwa kujua ilikuaje kuaje nchi moja iwe na eneo kubwa hivyo huku majiran zake wakikosa hata sehem ya kulimia.

Hii ipo hata kwa nchi za mashariki ya kati. Ukiiangalia Saudia ukubwa wake unaweza kufikiri kuwa Israel ni moja ya kata yake maana hata wilaya au mkoa wa Saudia unaonekana ni mkubwa kwa ardhi ya Israel.
Tukija kwetu naziangalia Burundi na Rwanda ni kawa wilaya tu zilizopo ktk mikoa ya Kigoma na Kagera.
Ni nani aliegawa mipaka hii na kwanini alibagua hivi?

Kwa wale wasioona vizuri Map nawashauri wa zoom.
 
Attachments

  • f39f3ec1ff4ca0ea0fb22a59fa2ded25.jpg
    f39f3ec1ff4ca0ea0fb22a59fa2ded25.jpg
    24 KB · Views: 4
  • images (24).jpeg
    images (24).jpeg
    39.3 KB · Views: 7
... Israel ni special case; mipaka yake iko kwenye makabati ya Mbinguni.

Hizo nyingine ilitokana na survival for the fittest. Tawala zilizokuwa na nguvu ziliweza kutwaa ardhi kubwa na zile nyonge ndio hivyo tena. Mfano ni wewe mwenyewe; una eka ngapi za ardhi? Inawezekana hata kiwanja huna ila kuna watu wana eka kwa eka za ardhi.
 
... Israel ni special case; mipaka yake iko kwenye makabati ya Mbinguni.

Hizo nyingine ilitokana na survival for the fittest. Tawala zilizokuwa na nguvu ziliweza kutwaa ardhi kubwa na zile nyonge ndio hivyo tena. Mfano ni wewe mwenyewe; una eka ngapi za ardhi? Inawezekana hata kiwanja huna ila una watu eka kwa eka za ardhi.
Muone huyu

Mungu yupi? Yuda
... Israel ni special case; mipaka yake iko kwenye makabati ya Mbinguni.

Hizo nyingine ilitokana na survival for the fittest. Tawala zilizokuwa na nguvu ziliweza kutwaa ardhi kubwa na zile nyonge ndio hivyo tena. Mfano ni wewe mwenyewe; una eka ngapi za ardhi? Inawezekana hata kiwanja huna ila kuna watu wana eka kwa eka za ardhi.
Mbinguni kwa wanywa pombe? Au kwa mbinguni kwa lesbian? Mshamba we
 
mi naona imetokea tuu ikawa hivyo... au viongozi wa hizo nchi kubwa walikuwa na nguvu wakachukua ardhi zaid
Kwahiyo zile story kwamba wazungu ndio waliozigawa nchi zetu, na kuleta mipaka baina ya nchi na nchi ni story tu zisizokuwa ukweli wowote?
 
... Israel ni special case; mipaka yake iko kwenye makabati ya Mbinguni.

Hizo nyingine ilitokana na survival for the fittest. Tawala zilizokuwa na nguvu ziliweza kutwaa ardhi kubwa na zile nyonge ndio hivyo tena. Mfano ni wewe mwenyewe; una eka ngapi za ardhi? Inawezekana hata kiwanja huna ila kuna watu wana eka kwa eka za ardhi.
Ni Mungu gani huyo anaebagua ardhi aliyoiumba mwenyewe? Kwamba kipande kimoja mipaka yake iwe mbinguni na eneo lililobaki mipaka yake ibaki duniani?
Kwa vile ana nguvu na uwezo wa kila kitu ni kwanini hakuamua dunia nzima iwe na mipaka yake huko mbinguni kama alivyofanya kwa hiyo Israel?

Hawa walioleta dini hawa..... 😷😷😷
 
Kwahiyo zile story kwamba wazungu ndio waliozigawa nchi zetu, na kuleta mipaka baina ya nchi na nchi ni story tu zisizokuwa ukweli wowote?
.... Struggle for power amongst African chiefdoms sio kwamba haikuwepo; ilikuwepo na wababe walitwaa ardhi kubwa kwa himaya zao. Tumejifunza tawala kama Monamutapa Empire na nyinginezo ni mmatokeo ya ubabe.

Bahati mbaya (nzuri?) wakaja wababe zaidi (Europeans) tawala za kichifu zikafia kusikojulikana.
 
That's the fact! Tawala zenye nguvu ziliweza kupanua mipaka ya himaya zao.
Kumbe ni watawala wenyewe ndio waliotengeneza kitu kinachoitwa nchi na mipaka yake. So mabeberu waliotugawa kama tulivyoaminishwa?
 
Ni Mungu gani huyo anaebagua ardhi aliyoiumba mwenyewe? Kwamba kipande kimoja mipaka yake iwe mbinguni na eneo lililobaki mipaka yake ibaki duniani?
Kwa vile ana nguvu na uwezo wa kila kitu ni kwanini hakuamua dunia nzima iwe na mipaka yake huko mbinguni kama ulivyofanya kwa hiyo Israel?

Hawa walioleta dini hawa..... 😷😷😷
Mungu ni alfa na omega! Hapangiwi cha kufanya au namna ya kufanya. Wewe unataka kum-contain Mungu kuendana na matakwa yako? Huyo si Mungu.
 
Tupanue mada,kwanini ukoo A uwe na wanukoo 29 na ukoo B unawanaukoo 229?

Kuna mambo yalizingatiwa,hata hivyo hayo mambo siyajui vizuri,wajuzi njooni mtusaidie.
Mkuu hili swali lako linatokana na mada hii au umechomekea tu upate majibu ya huku na kule?
 
... of course mipaka ya Afrika ni matokeo ya struggle for power amongst European nations. Mbabe alitwaa maeneo ya kibabe. Pamoja na Berlin Conference, haikuwa lelemama.
Cha kushangaza Uganda na Kenya zilikuwa chini ya Muingereza, lkn ardhi ya Kenya ni kubwa kuliko ya Uganda.

Zambia, Zimbabwe na Malawi pia zilikuwa chini ya Muingereza, lkn ardhi zao pia zinatofautiana ukubwa. Sasa unajiuliza kama mtawala wa eneo alikuwa mmoja ilikuaje ukataji wa mipaka ya ardhi uwe tofauti?
 
Kurahisisha utawala wakoloni walizingatia pia mila na desturi mahalia. Walijua waki-group chiefdoms walizozikuta katika makundi fulani (Kenya vs Uganda; Zambia vs Malawi vs Zimbabwe vs Botswana) utawala kwao ungekuwa rahisi among other key factors.

Kutawala kutokea London na bado order ikaweza kufika makoloni yote duniani hadi India na Pakistan ilihitaji akili kubwa!

Ukipewa umonitor wa darasa unaweza kukushinda sembuse kutawala ma-bushmen yasiyo na akili!
 
.... Struggle for power amongst African chiefdoms sio kwamba haikuwepo; ilikuwepo na wababe walitwaa ardhi kubwa kwa himaya zao. Tumejifunza tawala kama Monamutapa Empire na nyinginezo ni mmatokeo ya ubabe.

Bahati mbaya (nzuri?) wakaja wababe zaidi (Europeans) tawala za kichifu zikafia kusikojulikana.
Hapa nimekuelewa vizuli mkuu
 
Back
Top Bottom