Hivi ni nani aliekata mipaka ya nchi hizi?

Mungu ni alfa na omega! Hapangiwi cha kufanya au namna ya kufanya. Wewe unataka kum-contain Mungu kuendana na matakwa yako? Huyo si Mungu.
Hapo ndo wafrika tunapokwama.
Chochote tunachoambiwa na weupe tunakipokea vilevile kilivyoletwa bila kufanya utafiti wowote wa kueleweka.
Lakin story za aina hii wewe mwafrika au mtu mweusi usingeweza kuzipeleka huko Israel, Uingereza, Italy na kwengineko wakazikubali bila kuwaonesha fact wanayoweza kuiona kwa macho.
Wengine wanasema lugha ya Mungu ni moja tu Kiarabu, sasa unajiuliza hizi lugha nyingine zimekujaje kujaje na nani aliewapa watu uwezo wa kuongea lugha tofauti?
Hizi dini zilizoletwa hizi na weupe katika ukoloni.... 😷😷😷
 
Hizo sio story kaka. Mungu wa Yakobo ndiye Mungu.
 
Kurahisisha utawala wakoloni walizingatia pia mila na desturi mahalia. Walijua waki-group chiefdoms walizozikuta katika makundi fulani (Kenya vs Uganda; Zambia vs Malawi vs Zimbabwe vs Botswana) utawala kwao ungekuwa rahisi among other key factors.

Kutawala kutokea London na bado order ikaweza kufika makoloni yote duniani hadi India na Pakistan ilihitaji akili kubwa!

Ukipewa umonitor wa darasa unaweza kukushinda sembuse kutawala ma-bushmen yasiyo na akili!
Ki ukweli ukiitizama Jiografia ya nchi ya Uingereza kutawala nusu na robo ya dunia yote ikiwemo USA, Canada, Australia, New Zealand nk. Hii ilikuwa ni akili kubwa kuliko ukubwa wenyewe.
 
Nashukuru umeelewa. Wewe ni kati ya waungwana sana humu jf.
 
Mkuu hili swali lako linatokana na mada hii au umechomekea tu upate majibu ya huku na kule?
Ukilitazama swali na maelezo yake kwamba ni kupanua wigo wa mada yako ungeelewa.Nilitaka ulitumie swali uifikiria sababu za kutokea kwa utofauti wa mipaka(kama ilivyo sasa).
Mbinu hii ktk ufundishaji huitwa 'bungua bongo',kimtaa huitwa 'chemsha bongo'.Mbinu ya kuuliza swali kwa swali ni nzuri kwa kiasi chake kwani humwezesha muiliza swali kuushughulisha ubongo wake ili hata akipewa majibu ya swali lake basi anaweza kuelewa haraka.(sorry kama nimekuchanganya)
 
Serikali moja na lugha moja kidogo linaweza kuwa suluhisho la huu mtengano japo wafia dini mnapinga.
 
Mungu ni alfa na omega! Hapangiwi cha kufanya au namna ya kufanya. Wewe unataka kum-contain Mungu kuendana na matakwa yako? Huyo si Mungu.
Acha kuamini stori za kijinga na wewe unaamini mipaka ya israeli ipo mbinguni?
 
... Israel ni special case; mipaka yake iko kwenye makabati ya Mbinguni.

Hizo nyingine ilitokana na survival for the fittest. Tawala zilizokuwa na nguvu ziliweza kutwaa ardhi kubwa na zile nyonge ndio hivyo tena. Mfano ni wewe mwenyewe; una eka ngapi za ardhi? Inawezekana hata kiwanja huna ila kuna watu wana eka kwa eka za ardhi.
Kwaiyo mipaka mingine ipo kwenye mikabati ya Shetani akili yako haiko sawa mkuu anyway Israel nchi yao imekuja juzi tena kwa ushawishi wa Marekani
 
Sorry kama umekereka Mkuu ila ndio hivyo.
 
Ukilitazama swali na maelezo yake kwamba ni kupanua wigo wa mada yako ungeelewa.Nilitaka ulitumie swali uifikiria sababu za kutokea kwa utofauti wa mipaka(kama ilivyo sasa).
Mbinu hii ktk ufundishaji huitwa 'bungua bongo',kimtaa huitwa 'chemsha bongo'.Mbinu ya kuuliza swali kwa swali ni nzuri kwa kiasi chake kwani humwezesha muiliza swali kuushughulisha ubongo wake ili hata akipewa majibu ya swali lake basi anaweza kuelewa haraka.(sorry kama nimekuchanganya)
Oh hapa nimekuelewa mkuu wangu
 
Hizo sio story kaka. Mungu wa Yakobo ndiye Mungu.
Mungu ni wa kila kiumbe mkuu sio wa Yakobo peke yake. Acha kuamini mambo yaliotengenezwa na watu fulan ili ije kuonekana kama wao ndio walikuwa na hakimiliki ya Mungu na wengine eti hawana.

Kama Mungu ni wa Yakobo vipi kuhusu wewe, mimi, babu zako na zangu waliumbwa na Mungu gani? Pia Mungu kama ni wa Yakobo vipi kuhusu binadam wa kwanza kuumbwa kabla ya Yakobo yeye aliumbwa na Mungu gani?
Ni kwanini Mungu awe wa Yakobo na sio wa Adamu, wewe au mimi?
 
Nashukuru umeelewa. Wewe ni kati ya waungwana sana humu jf.
Mkuu nashukuru sana kwa comment zako zinazoelewesha na kuelimisha.
Ulichoandika kiliendana na uhalisia wa mada husika, kwahiyo ni ngumu sana kwa mtu mwenye uelewa ashindwe kuelewa kile ulichoandika.
 
Serikali moja na lugha moja kidogo linaweza kuwa suluhisho la huu mtengano japo wafia dini mnapinga.
Mkuu unamaanisha serikali moja na lugha moja kwa afrika nzima au kwa nchi moja?
 
Mkuu nashukuru sana kwa comment zako zinazoelewesha na kuelimisha.
Ulichoandika kiliendana na uhalisia wa mada husika, kwahiyo ni ngumu sana kwa mtu mwenye uelewa ashindwe kuelewa kile ulichoandika.
Pamoja sana Kiongozi. Tulipokwazana tusameheane. Ndio ubinadamu huo.
 
Mjerumani alijimegea bongo, rwanda na burundi. Sasa kwanini bongo ikawa kubwa ki mipaka na zingine zikawa finyu? Kwanini zisingekuwa mikoa yetu tuwatawale? Kwanini zipewe hadhi ya kuwa nchi kisha kigoma inayofanana nazo inyimwe hadhi hiyo?
 
Pamoja sana Kiongozi. Tulipokwazana tusameheane. Ndio ubinadamu huo.
Ya ni kweli mkuu, sisi wote ni ndugu kuanzia kwenye utamaduni, mila na utaifa wetu. Kwahiyo kukwaza kimtazamo wa kiimani au kwa itikadi ya mambo ya kitaifa haiwezi kuwa sababu ya kutoheshimu misingi yetu ya undugu na umoja wetu kama watanzania.
Ubarikiwe sana mkuu.
 
Back
Top Bottom