Mkuu
jmushi1 kuna mifano mingi sana inayothibitisha kuwa lockdown infanya kazi.
1. Wengi hawafahamu nchi ya kwanza kuweka lockdown ilikuwa New Zealand chini ya Waziri mkuu Jacinda Arden. Nchi hiyo ina maambukizi machache sana vifo na ni moja ya ''success story'' duniani.
2. Visiwa vya Caribbean ikiwemo Cuba vina maambukizi machache na vifo 84 kutokana na hatua za lockdown
Cuba ina kifo kimoja kama sitakosea kwa taarifa za karibuni.
3. Italy ilifanikiwa kupunguza mazishi kwa kutumia Jeshi baada ya lockdown.
Kumbuka Italy ndiko Biblia ilikoandikwa na kama leo 'Masiah akifanya ziara ya kushtukiza duniani' atapokelewa na Pope kule Vatican. Pamoja na hayo, Vatican ilikuwa katika lockdown na Pasaka ilikuwa ya Pope na wapambe 4.
4. Mecca , mji mtakatifu na sehemu ya Mahujaji, wamefunga sughuli zote kwa maana ya lockdown
5. South Africa, inasifiwa kwanza, kwa uwazi katika kutoa takwimu.
Pili kwa hatua kali za lockdown zilizopunguza maambukizi.
6. Brazil na Rais wao Bosara aliyesema ni mafua ya kawaida na hataki lockdown, leo amezika na sasa ni nchi inayoongoza katika top 5 zenye vifo vingi na bado watu wanakufa huenda ikashindana na Marekani
7. UK walikataa lockdown kwanza, well, kilichofuata ni misiba hadi wakaweka bila shurti. Johnson anajua
8. Nchi za EAC zilichukua hatua mapema tukiwa hatuna mgonjwa hata mmoja.
Leo idadi kubwa kuliko wao, hatujui namba kamili. Wanatufungia mipaka! sisi tukiwaonea huruma wanatutegemea
Swali ninalojiuliza, hivi huyu Mungu wetu tunayemtegemea ni tofauti na wa duniani?
Kwanini Mungu aliyepelekea Italy na Vatican kuzika kwa kutumia jeshi atusikilize tofauti na wenzetu?