Hivi ni nani anawadanganya watanzania kuwa lockdown haifanyi kazi? Hata kama tumeigomea, tuache kupotoshana!

Hivi ni nani anawadanganya watanzania kuwa lockdown haifanyi kazi? Hata kama tumeigomea, tuache kupotoshana!

Ajabu sana, wenye akili zao wamepiga lockdown, wametoa elimu na watu wameelimika na sasa wanaanza kufungua hizo lockdown kwa tahadhari kubwa sana, tunawaona hata kwenye supermarkets zao na maeneo mbalimbali walivyo na nidhamu ya hali ya juu (tunajipa moyo kwamba wanatuiga), upuuzi mtupu, sisi hakuna elimu iliyotolewa hata theluthi kulinganisha na kwao, zaidi tunaambiana tusitishane na huku watu wakiendelea kuteketea na kimdudu kikiendelea kusambaa, usipinge kwa kuwa halijakufika, na ukipinga likaja kukufika uje uunge mkono hoja usikae kimya kwa aibu, Lockdown ilitakiwa sana tu na siyo ya milele bali ya muda tu na elimu itolewe kwa kila njia, wale waliokuwa wakizika usiku wasambaze vipeperushi kutoa elimu namna ya kujikinga tukitoka, watu wangeogopa na wangeishi kwa tahadhari ya hali ya juu na ingesaidia sana kupunguza hofu iliyoko mtaani kwa sasa, kila mtu anamuogopa mwenzie, na wala kusingekuwa na mazishi ya usiku. Shule zimepigwa lockdown hakuna mishahara kwa walimu na wafanyakazi wengine wa shule, kwao tunaona ni sawa lokdaun ila kwenu nyinyi siyo sawa kwa sababu gani? Hakuna nchi hata jirani zetu aliyekufa kwa njaa, sisi tunakula sana ama vipi? Nimeagiza popcorns nyingine.
Kadiri muda unavyozidi kwenda, wanaotetea haya watapunguwa maana yatawafika tu.
 
Ukishashiba unadhani kila mtu ni fisadi tajiri kama wewe!?

Kuna tunaobangaiza kutoka nje kila siku kwenda kutafuta huku na kule ili tusife njaa!

Wewe uko bize unaleta mifano ya ulaya! Bongo na ulaya wapi na wapi?

Hizo shule zenu za kata hazikuwafunza majedwali ya kuoanisha vinavyofanana?

Halafu, umezuiwa kujifungia? Kwanini usijifungie? Unataka kusindikizwa na kila mtu una ajenda gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
Nani amesema kila mtu alitakiwa kufungiwa?wacha kukwepa majukumu.
 
Hahahahaha hujui Wuhan pamewaka Moto au hufatilii vyombo vya habar

Sent using Jamii Forums mobile app
Na bado anadhani walifanya au wanafanya mchezo. Tungekuwa serious, tungewashirikisha viongozi wa ngazi za chini huko kama mabalozi na makatibu tarafa kwenye janga hili! Ni suala la kuwa serious na siyo kama ilivyo sasa...
China’s residents live under a grid-style social management system: All residential areas are divided into geographical blocks, and street-level authorities assign individual workers to manage each of them.

The system enforces “social stability” in regular times, with these workers monitoring their assigned residents and reporting them for undesirable activities such as gambling or religious gatherings. During the pandemic, they’ve become responsible for enforcing restrictions on movement, registering people for tests, and caring for the vulnerable under lockdown.


Wuhan reopened last month. Now, new coronavirus infections spark mass testing and renewed fears
 
Mkuu hoja apa ni njaa

Serikali haina uwezo wa kuwapa at nusu kibaba cha dona wananchi wake kwa mwez mzima

Na ww unatakiwa utuambia hyo partial lockdown waliwafanyia nn wananchi wao!?


Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani ugonjwa ulianza nchi nzima kwa pamoja? Tambuwa kwamba mlisema tutakufa njaa tukiwazuia wachina wakati kila Taifa tayari walishaifungia!
 
Yani unavyo shupaa utadhani hauijui Tanzania...in Tanzania lockdown won't work bro and will never work
Mliacha kufunga mipaka, na AirPorts wachina na wageni wengine kumiminika kwa kigezo cha njaa!

Mulikataa kufunga baadhi ya maneneo huku mnawatafuta ama ku trace contacts! Kwa kigezo cha njaa! Wakati Rwanda imeweza na wakati tuna chakula kushinda wao!

Sasa mnakurupuka na kusema eti lockdown ni kufungia wananchi ili wafe na njaa!

Mumeenda hadi vijijini kudanganya wazee kuwa wanaosapoti lockdown, wanataka wawafungie ndani huko vijijini kwao nk. Huo ni upotoshaji na propaganda mbaya! Tambua kwamba ugonjwa ukifika kijijini hata hapo Dar mtalia njaa maana wakulima watakuwa busy na corona!
 
Hili swala nadhani tulifanye kuwa sisi Mkuu wetu ameamua tusitumie ile njia ya kujifungia, na ukiangalia nchi zetu hizi wananchi wake wana usugu fulani kwenye mafua.

Tatizo upande wa mkuu hakuna suluhu upande wa upinzani ni kubezwa na kuzarauliwa. Nao wanajitahidi kusisitiza kuna maana katika kujitenga.

Mashindano haya hayafai lolote, wapinzani kubezwa huku kunaweza kukitokea kweli hali ikabadilika na vifo vikajaa mitaani. Mkuu ataaibika sana,

Lakini pia kama hakutakuwa na vifo vingi na ugonjwa kupotea upinzani watabezwa na kuaibishwa sana.

Haya yote yanatija yeyote?

Ni upuuzi usio na maana yeyote kwa Mkuu na Upinzani pia, huu ni ugonjwa na janga linalo gharimu maisha ya watu. Basi upande mmoja unyamaze hasa upinzani wamesema sana basi wanyamaze.

Serikali nao wasilazimishe maana huu ugonjwa upo na unaendelea kuua watu. Wasilazimishe
mpka kuficha vifo na hali ya ugonjwa iliyopo kwa uhalisia wake. Siasa hizi zinapindukia kwenye chuki sasa na hasa vyombo vya usalama kuanza kuwakamata na kuwatesa wanao wakosoa, au kuwaambia mbadala wasioupenda wanasiasa wao, baada ya haya kuna maisha pia.

Mkuu asikimbie ofisi na majukumu yake na kwenda kujificha akiogopa ugonjwa na huku akiwahimiza wengine waendelee kufa na ugonjwa huku yeye akiwa mafichoni. Ni usaliti. Lakini wapinzani umefika wakati wa kunyamaza.

Kuna ofisi moja ingeweza kumaliza malumbano haya kama ingekuwa na watu makini na wenye ufahamu, bali hii ofisi imegeuka na kuwa haina manufaa kwa nchi na wananchi walio wachagua GENGE HILI ndiyo ofisi pekee yenye uamzi wa kumaliza shida hii. Lkn sasa ndiyo haina maana kabisa watu wake ni zero wamejazana humo kuwafirisi waTZ. Uongozi wake ni zero + zero ukiwasikiliza ni genge litakalo kumbukwa miaka mingi ijayo. Wana hira mashetani wasio na haya wamekalia kukomoana hasa kiongozi wao. Ni AJABU
SIJUI HUWA ANAVUTA BANGE KITUKO. NIWA KUOMBEA KWELI

Basi najua MUNGU ATATUOKOA na hawa watu bali walioandikiwa watakwenda wasioandikiwa watabaki.

Tuendelee kujikinga Corona ipo.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo linked article haikuongelea hayo mkuu.
Ameongelea reality ya sasa bila kutaja makosa ya Trump
Hayo ni matatizo yao yaliyosababishwa na uongozi mbovu wa Trump kwenye janga hili! Uzuri wa wenzetu, kuna accountability in one way or another. Kwahiyo wananchi lazima wapime kama alionyesha uongozi makini wakati wa janga hili linalotafuna maelfu ya wamarekani, wengi kwasababu ya uzembe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mliacha kufunga mipaka, na AirPorts wachina na wageni wengine kumiminika kwa kigezo cha njaa!

Mulikataa kufunga baadhi ya maneneo huku mnawatafuta ama ku trace contacts! Kwa kigezo cha njaa! Wakati Rwanda imeweza na wakati tuna chakula kushinda wao!

Sasa mnakurupuka na kusema eti lockdown ni kufungia wananchi ili wafe na njaa!

Mumeenda hadi vijijini kudanganya wazee kuwa wanaosapoti lockdown, wanataka wawafungie ndani huko vijijini kwao nk. Huo ni upotoshaji na propaganda mbaya! Tambua kwamba ugonjwa ukifika kijijini hata hapo Dar mtalia njaa maana wakulima watakuwa busy na corona!
Mkuu sijui umetumia creteria gani kuifananisha Rwanda yenye 12.3m populationa na eneo la 26,338 km2 wakati population na TZ ina yenye 56+m na eneo la 947,303 km2 zaidi ya mara 35 kuilinganisha na Rwanda.... Kiuchumi kwa maana ya mtu mmoja mmoja wanakipato kizuri kuliko Tanzania ambao mlo wao mpaka mtu atoke aonane na mtu ili ale. Serikali imechukuq hatua na inaendelea kuhamasisha sana kupitia media... Mwitikio upo na tutafanikiwa
 
Back
Top Bottom