Hivi ni sawa hili la kuhubiri ndani ya mabasi ya umma?

Hivi ni sawa hili la kuhubiri ndani ya mabasi ya umma?

kiukweli hapo hata akiwa wa dini yoyote yule sio ustaarabu.

binafsi huwa nna waza sana......
kabla ya hawa wenzetu kutuletea hizi dini ,tulikua na dini (Imani) zetu za kimila na mambo yalikua yanaenda.......

wakaja hawa wenzetu kutuletea za kwao ,tukaacha za mababu zetu huko japo hawa wenzetu ni wajanja wajanja sana....waarabu Kwa wamisionari
walikua na mambo yao waloyaficha nyuma ya pazia sio hivi hivi ...

Tukaacha dini za mababu zetu na saivi tumekua "wakereketwa" kuliko hata walotuletea hiyo dini yenyewe.....tupo radhi kuuwana kisa dini za mapokezi ..

Ukereketwa huu umefikia hatua ya kupelekeshana , kutishiana ooh usipofanya hiki cjui mara kile utafikwa cjui na nn , mara toa hiki upate kile .......kufokeana, kuogopeshana nikae natetemeka, sadaka mda mwingine Ka lazima, unaenda nyumba ya ibada ukitaka kutoka linapigwa biti Ka cjui nn .....aisee sipendi
Ni tatizo halafu wanalazimisha uamini wanachoamini wao, usipoamini wanakasirika.
 
Ndio maana yakajengwa makanisa.ina maana huko akuwatoshi.isitoshe kwenye gari kila mtu ana imani yake.inakua sio ustaharabu mzur.
na nyie pigeni adhana hakuna aliyewazuia
 
Wadau naomba kuzungumzia kuna hili jambo kwa sasa limezidi kushika kasi kuhubiri ndani ya daladala imekuwa sehemu nyingi hasa mabasi ya Tegeta toka mjini yaaani mnakosa utulivu kwenye mabasi na mwisho wa siku wanachangisha sadaka sasa najiuliza hii hali vipi wadau
Hili ni kosa la jinai...huwezi ingia ndani ya dala dala na kuanza kurap kwani si kila mtu anafuata hizi dini za kikoloni (Uislam na Ukristu)....watu lazima tuheshimiane. Serikali naomba ituruhusu raia kuua ama kupiga mawe hawa wahubiri wa hizi dini za kikoloni. Hii ni dharau na matusi kwa sie tunaojitambua.
 
Ndio hatutaki sasa.huko ni kulazimishana imani.kama me ni mpagani je.wasitusumbue asee.tukimiss tutawafata huko kwa maeneo yao maalum ya hzo mambo zao.
Hizi dini zimekuwa chaka la matapeli.

Hawa wezi wameshabaini kwamba watu wamelewa dini wamekuwa misukule wa imani. Ni rahisi sana kuwalaghai.

Ukithubutu kuwakemea hawa matapeli utashambuliwa mpaka ukimbie gari.

Watakuita mchawi.
 
hao wahubiri labda wanagawana sadaka na hao madereva wanaowapakia
 
Wewe una matatizo. Unalazimisha kwamba habari za Mungu ndio njema, Nani kakwambia? Halafu kwani ni lazima kuamini? Tutazifata huko kwenye makanisa tuondoleeni usumbufu kwenye mabasi. Msilazimishe unaloamini wewe kila mtu aamini. Hata mchawi ana haki zake..
Mbona wachawi hawaji kanisani kuhubiri sera zao?
Kwakuwa Sheria haijamkataza utapata tabu Sana na uchawi
 
Hizi dini zimekuwa chaka la matapeli.

Hawa wezi wameshabaini kwamba watu wamelewa dini wamekuwa misukule wa imani. Ni rahisi sana kuwalaghai.

Ukithubutu kuwakemea hawa matapeli utashambuliwa mpaka ukimbie gari.

Watakuita mchawi.
Sure mkuu...

baadhi kama c asilimia kubwa ,sisi waafrika tuna changamoto sana vichwani mwetu. Unakuta Jambo optional , linalazimishwa kua lazima.

Mababu zetu walikua wanaamini kwenye mila cjui na mizimu huko ...na wakienda kuomba iwe mvua, njaa , ugonjwa .....majawabu wanayapata na mambo yanakwenda fresh tu.

nafikiri malengo ya dini huenda yalikua mazuri ila baada ya kupokewa na wakereketwa/wafia dini/wajanja wajanja hapo katikati wameingiza vitu havieleweki kazi kupigana mabiti, kutishana, kuogopeshana na ndo hapo utakuta watu tumejengewa uoga zaidi na utii ...unakubali kila kitu bila hata kufanya Reasoning.
 
Uwe unanipitia kuanzia leo nitakwenda church

Plan ya kwenda kanisani inaanzia Jumamosi, unahakikisha unalala bila kutia vyombo.

Maana ukilala umeshapiga vyombo likelihood ya kuchelewa kuamka ni kubwa.
 
Kwakuwa Sheria haijamkataza utapata tabu Sana na uchawi
Actually, sheria imekataza.

This is nuisance and emotional disturbance!

Sio kila mtu anataka kubwatukiwa hizo injili za kitapeli.

Kama una hamu sana ya kubwatuka injili kwanini usijenge banda lako la maturabai ubwatuke humo usiku kucha?

Na hili jua kali watu wana misongo ya mawazo wewe unafika tu unaanza kuwabwatukia!

Mtakuja kutandikwa makofi siku moja!
 
Mbona huwa tunahubiri bure bila kudai sadaka? Tunawapa neno popote ili siku ya mwisho msisingizie kuwa hooo hatukusikia
 
Back
Top Bottom