Hivi ni sawa kuzaa watoto kwa matarajio ya watakuja kukusaidia baadaye?

Kweli, suala la kusaid
 
Mimi kuzaa au kutozaa ina umuhimu gani katika hoja dhahania?

Hili si suala la mimi binafsi, ni suala la facts.

What is your point?
Point yangu ni kujua mtazamo wako binafsi kuhusu kuzaa kwa sasa na kama umebadilika au ndio ulivyokuwa tangia mwanzo, je ni kitu kizuri?
 
Waafrika wengi tunazaliana ilimradi tu bila hata kujiuliza. Sababu tunazitafuta baada ya kuzaa.
 
Hii nayo nimechelewa kuiona Lakini bado ni mupya.
Napenda sana fikra zako ShesRise_1

Kuhusu hii maada Mimi Nina mitazamo miwili.

1. PRIMITIVE AGE

Kile kipindi ambacho wazee wetu walikua wanaoa wake wengi na kuzaa watoto wengi ili wapate nguvu kazi ya kulima mashamba na kuchunga mifugo.

Kwa nyakati hizo watoto walikua ni utajiri kwasababu watoto pamoja na mama zao walitumika kama nguvu kazi katika shughuli za uzalishaji.

Pia kutokana na ndoa za mitala pia wanawake walikua wanazaa watoto wengi ili kushindana😂 na kujaribu kumshawishi mwanaume ampende mwanamke aliemzalia watoto wengi. Mfano ni ndoa ya Yakobo.

2. UJINGA, UPUMBAVU NA KUKOSA AKILI

Hii nimeshindwa kuipa jina moja lakini katika maelezo tutaelewana.

Kuna mzazi au wazazi wanazaa watoto wengi pasipo kuwa na mipango/mikakati yoyote ya maisha ya sasa au ya baadae ya hao watoto.

Hawa wazazi wanazaa watoto wengi huku wakitegemea kudra za mwenyezi Mungu juu ya hao watoto. Kuna kauli moja hupenda kuitumia wanasema " Kila mtoto amebeba baraka zake"

Binafsi huwa natamani sana kuwauliza kwani wao walizaliwa wakubwa? Yaani wao hawakuwa watoto? Je! wao wakati wanazaliwa hawakubeba hizo baraka wanazozitarajia kutoka kwa watoto wao?

Ukienda mbele zaidi na kusoma maandiko ya biblia inasema mtoto hurithi Mali kutoka kwa babaye (mithali 19:14). Sasa inakuaje mzazi amtegemee mtoto? Unaona ni kama Kuna ujinga/upumbavu au kukosa akili kwa hawa watu maana hata Mungu mwenyewe amekataa hayo mawazo yao.

Pia biblia inatufundisha kwamba Mungu ndiye Baba yetu na YESU Kristo ni mwanawe. Tunaona kwamba Mungu amempa urithi wa Mali zote YESU Kristo ambaye ni mwanaye. Hagai 2:8 Warumi 8:17

Kwahiyo hawa ndugu zetu wanaozaa watoto wakitegemea watakuja kuwasaidia ni kwamba akili zao zinakasoro kidogo.
 
Point yangu ni kujua mtazamo wako binafsi kuhusu kuzaa kwa sasa na kama umebadilika au ndio ulivyokuwa tangia mwanzo, je ni kitu kizuri?
Kuzaa inatakiwa anayezaliwa aulizwe kabla hajazaliwa, aamue anataka au hataki kuzaliwa. Kitu ambacho hakiwezekani.

Zamani nilikuwa naona kuzaa ni jambo la kawaida, tena kama wajibu.

Sasa hivi naona it is a moral problem kumleta mtoto kwenye dunia hii yenye matatizo mengi, bila ya mtoto huyo kukubali.
 
Mi nafikiri kama unamudu vizuri kumpa mtoto mahitaji ya muhimu na upendo na msingi mzuri wa kujitegemea kuzaa sio kitu kibaya.... asilimia kubwa ya watu hawajutii kuzaliwa pia, wanaona maisha yana maana, japo changamoto lazima ziwepo
 
Mi nafikiri kama unamudu vizuri kumpa mtoto mahitaji ya muhimu na upendo na msingi mzuri wa kujitegemea kuzaa sio kitu kibaya.... asilimia kubwa ya watu hawajutii kuzaliwa pia, wanaona maisha yana maana, japo changamoto lazima ziwepo
Tatizo si kumpa mtoto mahitaji.

Tatizo ni kwamba unamleta mtu duniani bila ridhaa yake.

Ni jambo fulani gumu sana kulielezea ukishazaliwa, kwa sababu tayari unakuwa na bias ya kuzaliwa.

Ila, ukiliangalia kutika upande neutral, kumleta mtu duniani bila ya yeye kukubali, kuna tatizo.

Ukimsoma mwanafalsafa David Benatar katika "The Human Predicament: A Candid Guide to Life's Biggest Questions" kaandika vizuri sana suala hili.

Naweka attachment hapa ya pdf.
 

Attachments

Kuletwa duniani bila hiyari ndio asili ya viumbe hai vyote ilivyo.
Kiumbe yoyote anakuwa na msukumo mkubwa wa asili kuzaa alishapevuka, na binadamu ndivyo ilivyo.
Swala mwenyewe anazaliwa bila hiyari yake ili aje kuwa chakula cha Simba au chui, kama ni kulaumu basi tulaumu asili, viumbe wote ni watumwa wa asili au Mungu sijui
 
Hoja ya "asili" ni logical fallacy.

Inaitwa "Argument from nature" logical fallacy.
 
Kivip? Maelfu ya miaka watu wamekuwa wanazaa na kuzaa
Hapa umeongeza argument from tradition logical fallacy.

Kitu kuwa cha asili, au kuwa kinafanyika kwa maelfu ya miaka, haifanyi kuwa kiwe sawa.

Ndiyo maana hata magonjwa ya asili yaliyokuwapo kwa maelfu ya miaka, watu wameyapatia dawa na kuyaondoa.
 
Baba si useme tu wasukuma kwani unawaogopa?
 
Sasa kama nimemsomesha,nimemlea vizuri na kumwandalia maisha mazuri kwa nini asinisaidie pale ambapo mimi nimekosa nguvu(nimezeeka)?Unataka anitelekeze wakati yeye nilimpa kila kitu?
Ni wajibu wako kama mzazi! Wakati unafyatua watoto unatakiwa uandae na mpango wako wa uzeeni na huwezi kufanya hivyo kama unazaa watoto wengi kuzidi uwezo wa kuwasomesha
 
Ni wajibu wako kama mzazi! Wakati unafyatua watoto unatakiwa uandae na mpango wako wa uzeeni na huwezi kufanya hivyo kama unazaa watoto wengi kuzidi uwezo wa kuwasomesha
Naunga mkono hoja
 
Ulikua wapi mpaka mada imepoa
japo umesema bado mpyaa🔥

Asante kwa maoni yako mjarabu🙏🙏
 
Hii comment yako nilichelewa kuiona
Kwanza ni kuweke sawa mkuu

Ukisoma mada yangu hakuna mahali nimeandika watoto wasisaidie wazazi la hasha usinilishe maneno

Nimesema sio sahihi mzazi kuzaa watoto weengi ambao hana uwezo wa kuwatengenezea msingi mzuri wa maisha kwa matarajio asaidiwe baadae

Huo ni ujinga yaani uzae kwa kutegemea kusaidiwa halafu hapo hapo hujatengeneza future ya watoto ?

Mzazi na azae watoto anao wa mudu awalelee vizuri awapatie elimu bora na hii ni wajibu wake sio fadhila kwa sababu ukumbuke mtoto hajakuomba umzae kwa hiyo ni wajibu wako kumtimizia mahitaji


Na pia sio sawa kutaka kulipwa fadhila huko baadae kama kweli umewapa watoto elimu umewapa mahitaji yote ya msingi wanaachaje kukusaidia ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…