Mpigania uhuru wa pili
JF-Expert Member
- Apr 12, 2023
- 3,380
- 6,376
Oscar kambona alikua mkristo ila alikosana na nyerere..sidhani kama ni sahihi kusema Mwalimu Nyerere alikuwa na ugomvi na Abdulwaheed Sykes.
..Mwalimu angekuwa na ugomvi na kina Sykes basi asingemteua Abbas Sykes kuwa Gavana wa kwanza jimbo la Mashariki ambalo lilihusisha jiji la Dar Es Salaam.
..Baada ya hapo Mwalimu alimteua Abbas Sykes ktk nafasi mbalimbali za ubalozi ikiwemo ubalozi wa Canada, France, na Italy.
..Vilevile mdogo wake Dosa Aziz anaitwa Hamza Aziz alipata kuwa Mkuu wa jeshi la Polisi IGP. Kungekuwa na ugomvi kati ya Dosa Aziz na Mwalimu Nyerere, Hamza Aziz angeaminiwa ktk nafasi nzito kama IGP?
..Kuhusu uwepo wa wapigania uhuru waliosahaulika hiyo ni hoja inayosimama na wako wengi ambao hawajapata bahati ya kuwa na vijana wao wa kuwaandikia vitabu.
..Pia kuna watu walioteswa kwelikweli na utawala wa Mwalimu Nyerere, watu kama Christopher Kasanga Tumbo, James Mapalala, Bibi Titi Mohamed, na wengine.
Nyerere ambaye anatuhumiwa ni mdini kamwachia nchi mwinyi mwislamu kuna mambo watu wanashadadia na wana akili timamu kabisa