Hivi Nyerere aliwahi kugombana na Kanisa Katoliki au Protestanti?

Hivi Nyerere aliwahi kugombana na Kanisa Katoliki au Protestanti?

Wakuu kwema
Tunajua historia ya Tanzania, Mwalimu Nyerere aliwahi kuingia katika mgogoro au vita na iliyokuwa jumuiya ya Waislamu (East Afric Muslims Welfare Society) ambayo mgogoro huo ulipelekea jumuiya hiyo kufutwa na BAKWATA kuzaliwa

Napenda kuuliza kuwa kama aliwahi kuwa na mgogoro na Kanisa Katoliki au Waprotestanti hata kama haukuwa mkubwa kama ule wa Waislamu

Tunafahamu Magufuli aliwahi kugombana na Kanisa Katoliki na Lutheran kufuatia makanisa hayo kutoa nyaraka za kulaani watu kutekwa, na pia kuhusu alivyoshughulikia ugonjwa wa Covid

Mohamed Said
Iliwahi kutokea mara moja. Na Nyerere alilisema wazi. Japo haukuwa mgogoro kati ya Serikali na Kanisa, bali mtendaji mmoja wa Kanisa.

Kuna padre mzungu alikamatwa na nyara za Serikali, meno ya tembo, akisafirisha kwenda nje.

Baada ya kumatwa, Kanisa lilimwomba Rais amsamehe. Mwishowe alisamehewa, lakini alinyang'anywa mali hiyo isiyo halali, na alifukuzwa nchini.
 
Hizo propaganda ndio zinawafanya mchapwe fimbo ili msamehewe dhambi, mfunge hadi mfe

Mzungu bepari akusanye fedha aje akujengee wewe shule

hadi umri huu bado hujui kuwa kina nani ni moja ya Mawakala wa wakoloni ? Agent of colonialism ?

inamaana hujui kuwa dini ilikuwa kilainishi ( KY) ya kuingiza ( kupenyeza )Ukoloni Barani Africa?
Wewe acha ubishi wa kijinga Watanzania waliosoma kwenye hizo shule walisoma bure enzi hizo na hata matibabu walipata bure kutokana na michango ya Wazungu.Mwafrika alikuwa bado hajajua umuhimu wa COST SHARING.Na kama ulizaliwa baada ya 1990 huwezi jua kule tulikotoka utabaki tu kubwabwaja na stori zako za kijiweni.
 
Nyerere alitaifisha mali za Kanisa kibao, mashule, hospitali n.k

Punguani hawawezi kuliona hilo. Mashule mengi ya Kanisa yalitaifishwa na Serikali ili watu wa dini nyingine nao wasome katika shule hizo wakiwa na amani ya mioyo yao, lakini punguani wanaojificha kwenye udini hawawezi kuliona hilo.
 
Rasilimali za kujenga hizo shule hazikutokana na michango ya kanisani, zilitokana na rasilimali za Nchi

au unadhani walichukua kodi Vatican kuja kujenga huku ?

Kama hunui kitu ukae kimya. Usipende kuropoka mambo usiyoyajua.

Mashule, hospitali na makanisa, vyote wakati huo vilijengwa kwa pesa zilizochangwa na waumini wa makanisa mbalimbali ya mataifa ya Ulaya. Hailiwa kpdi ya watanzania wala sadaka za waumini maskini wa Tanzania.

Ni siku za karibuni sana, ndiyo vitu hivyo vimeanza kujengwa kwa michango ya waumini.
 
MUNGU ni Muweza wa yote Kwahiyo Hana sababu ya kujaza rundo la Kuni ili apate moto.
Na isitoshe hakuna mtu anayejua kwa usahihi maisha ya mtu aliyekufa huko aliko(peponi) yapoje.
Mawazo yako ni matokeo ya Imani uliyofunzwa. Na Imani hiyo ukiichunguza kwa undani utagundua kuwa Kuna baadhi ya mafundisho Yana maswali mengi kuliko majibu.( Mfano: kusema kuwa Musa aliyekuwepo kabla ya YESU alikuwa muislamu, wakati uislamu ulianzishwa mwaka 622 AD( baada ya YESU) , au peponi utapewa wanawake 72, na wakati mwili wa kulala na wanawake umezikwa ardhini na iliyokwenda peponi ni roho ambayo haina jinsi).
Watu wanapumbazwa, nao wanakubali. Umeeleza vizuri sana. Maisha baada ya kifo, ni ya roho pekee yake. Roho haihitaji chakula kwa kuwa chakula ni kwaajili ya mwili. Roho haihitaji nyumba wala gari. Roho haihitaji mke kwa sababu tenaldo la kukutana, tena linaitwa kukutana kimwili, ni la mwili, na siyo roho. Halafu wewe mtu na akili yako unaambiwa ukifa utapewa mabinti warembo mabikira, na wewe unaitikia!! Una akili wewe kweli? Tangu lini Roho ikawa na bikra!

"Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa", inadhihirika wazi.
 
Julius kuna makosa mengi aliyafanya kipindi cha utawala wake ndio yanayotugharimu mpaka leo
Mwongo. Yataje tuyajadili. Unapokosa hoja unabaki na hizi dhana za kuimbishwa tu kama kasuku.
 
Kwahiyo kumbe DINI ni kilainishi cha kuleta ukoloni Africa? Nasubiri jibu wallah.
Dini ilisaidia sana kuleta ustaarabu Afrika.Bila ukoloni bado tungekuwa na maisha mabaya tena tungekuwa Watumwa wa Waarabu.Tumshukuru mkoloni kwa kutuletea maendeleo.
 
Mali gani za Waislam zilizodhulumiwa na kutaifishwa?
Nilisoma mahali
hospitali kubwa na shule za madhehebu ya Kikristo vilitaifishwa. Lakini hospitali za Agha Khan, Hindul Mandal hazikuguswa. Wenye kuelewa mambo haya je hayo niliyosoma yana ukweli wowote?

Baada ya sera ya ujamaa kuwekwa kando kwa sababu zozote zile madhehebu mangapi yamejitutumua tena kujenga hospitali kubwa na hata taasisi za elimu kiwango cha vyuo.
 
Hilo ni swali la msingi sana.
 
Kama hunui kitu ukae kimya. Usipende kuropoka mambo usiyoyajua.

Mashule, hospitali na makanisa, vyote wakati huo vilijengwa kwa pesa zilizochangwa na waumini wa makanisa mbalimbali ya mataifa ya Ulaya. Hailiwa kpdi ya watanzania wala sadaka za waumini maskini wa Tanzania.

Ni siku za karibuni sana, ndiyo vitu hivyo vimeanza kujengwa kwa michango ya waumini.
siyo kweli, zile fedha zilikuwa zinatoka serikali kuu enzi ya ukoloni. Ilikuwa inafanya allocation ya certain percentage na kuwakabidhi kanisa kujenga mashule na huduma za jamii. Nilishawahi kukumbana na documentary fulani ilikuwa inaongelea hivyo vitu na ilikuwa ni system yao kwa makoloni yao yote ya Uingereza.
 
Watu wanapumbazwa, nao wanakubali. Umeeleza vizuri sana. Maisha baada ya kifo, ni ya roho pekee yake. Roho haihitaji chakula kwa kuwa chakula ni kwaajili ya mwili. Roho haihitaji nyumba wala gari. Roho haihitaji mke kwa sababu tenaldo la kukutana, tena linaitwa kukutana kimwili, ni la mwili, na siyo roho. Halafu wewe mtu na akili yako unaambiwa ukifa utapewa mabinti warembo mabikira, na wewe unaitikia!! Una akili wewe kweli? Tangu lini Roho ikawa na bikra!

"Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa", inadhihirika wazi.
Mambo ya imani yana maswala mengi sana ya kushangaza, kama hayo uliyoeleza hapo.
Na wakati huo huo, inaelezwa Mungu ndiye muweza wa yote. Kwa maana hiyo pia inamfanya mtu aamini kwamba Mungu huyo huyo atayawezesha hata hayo wanayotamani wakiwa huko peponi!
Mungu huyu mwenye uwezo wote; akaona ni vizuri binaadam aliowaumba yeye, wamwabudu kwa njia mbalimbali kupitia dini zao(?)..., wengine wawe wakristo, na wengine wawe mabudha, wahindu, waislam,n.k.,. Na katika dini zote hizo, patokee tena vikundi mbalimbali; waislamia, wasuni, wasabato, baptist, walokole na.k.n.k., na inapolazimika hawa watu wagombane kwa sababu za hizi dini zao za kumcha Mungu yule yule, ambaye anaweza kila kitu, anajuwa kila kitu; kama mtoto, anapotungwa mimba, hata kabla, kwamba mtoto huyo siku moja atakuwa peponi au jehanam...

Kuwa na Imani ni vizuri, na kumtukuza Muumba wako ni jambo zuri sana; kama ilivyo kuishi maisha na binaadam wenzako kwa maelewano mazuri. Mimi naamini, Mungu huyu mwenye huruma nyingi kwa viumbe wake, kamwe hawezi akageuka na kuwa katiri, anayechukizwa kila mara na kutaka kuangamiza binaadam aliowaumba.
Nitaishi maisha mazuri duniani kwa kutenda mema kwa uwezo wangu alionijaalia Mungu mwenyewe, na mwisho wa siku, atanipokea peponi pamoja na madhaifu mengi aliyoniruhusu kuwa nayo.
Nitatumia mafuzo nilikojiunga na dini, lakini 'dogma' za huko zote hazina maana kubwa kama zisivyokuwa na maana za wale wengine katika imani zote zinazodai kufundisha aliyowapa Mungu wayafundishe wao kwa binaadam, na kujiona wao ni bora zaidi ya wengine.
 
Back
Top Bottom