Nchi inaangamia kwa kukosa watu walio na maarifa na fikra dhabiti. Nchi imejaa rushwa, ufisadi, wizi, hongo na uongozi ulio na watawala wabovu. Nchi haina clear vision, umasikini umetamalaki, mfumuko wa bei, biashala kusuasua, ukosefu wa ajira, matumizi mabovu ya fursa na rasilimali, hivyo vyote hujaviona?. Unakuja na hoja mbovu za migogoro ya mwaka 1970 huko?. Unaanzisha mada za EAMWS ambazo hata taarifa zake huna bali kwa kusoma kwene site za mitandao tena zikilikuza jambo Kana kwamba ni kubwa. Zilitaifishwa hospitali na mamia ya shule za taasisi za Dini ya kikristo pamoja na mamia ya mali kama mashamba na viwanja je hayo hujayaona? EAMWS ilikua na nini cha Ziada? Haikufikia hata 5% ya mali za waprotestant achilia mbali Roman Catholic. Jumuiya mbovu iliyokuwa inafadhiriwa na yule mturuki agakhan ndio iwe mjadala. Stupid. Ashukuliwe baba wa taifa Mwalimu Julius kambarage Nyerere kwa kujenga jamii iliyo na Amani, Umoja na Mshikamano.