Miwazo ya aina yako haya huwa nawaachia wapumbavu wanaotafuta viongozi kwa kuangalia dini zao na si kwa kuangalia uwezo wao bila kujali dini zao.
Hivi katika akili zako bado unaona uongozi wa nchi hii unahitaji kuingizwa dini?
Ndiyo maana kuchwa nzima mnavimba misuri kutetea upumbavu wa namna hiyo
Hivi hamuwezi kuwatazama waTanzania wote kwa u-Tanzania wao kwanza kabla ya hayo maswala mengie yote?
Umezungumzia wakati wa Magufuli, ulitaka hao wenye dini yao wafanye lipi la ziada? Hukumbuki kitu chochote walichomkatalia Magufuli, au kwa vile akili yako imejifunga ndani ya dini, ambayo hata inawezekana siyo mfuasi wake mzuri?
Haya, tueleze, wewe katika dini yako hiyo, ulifanya jambo gani kumpinga Magufuli, na hao wenye dini nyingine hawakukusikiliza kwa vile tu wewe ni mtu wa dini?.
Ujuha ni huo wa kumteyea kiongozi hata kama hafai, kwa sababu tu ya dini yake.