Hivi Padri mtuhumiwa wa ubakaji na yeye ana Wakili?

Wakili anayemtetea hana Watoto wala mke.​

Atakuja kuelewa hilo somo siku mtoto / mke wake atakutana na Padre.​

 
Kwani kwenye hii kesi, zaidi ya tuhuma kwa padre je kuna ushahidi dhahiri wowote unaoujua?
Padri anajulikana anafanya hivyo vitendo hata mapdri wenzie wanajua. Awajibishwe aache kutuchafulia watoto na kanisa
 
Sawa ila kama ushahidi upo wanapima nini
Kuwa na subira. Mtuhumiwa ameshafikishwa mahakamani. Ana haki yake pia ya msingi, ya kujitetea. Hata Babu Seya na watoto wake walitetewa!
Mahakama ndiyo itakayo amua iwapo mtuhumiwa ana hatia, au la.

Siungi mkono vitendo vya kikatili dhidi ya watoto, lakini pia mimi ni mmoja ya watu wanao amini katika rule of law. So mahakama pekee ndiyo ina haki ya kuhukumu kwa mujibu wa sheria zetu tulizo jiwekea.
 
The court is a court of proof (beyond reasonable doubt) ,and not a court of truth. Mahakama ni mahakama ya vithibitisho (Pasipo na shaka ), na si mahakama ya ukweli.
 
Aiseee basi sawa. Ila huyu kwa watu wanaomfahamu na,wamesoma,nae wanamjua vizuri. Ww utaona ngoja kesi iendelee ila nahofia kukatizwa njiani
 
Ni mara ngapi sheria inapindishwa hata kama ushahidi ni wa ukweli? Mimi nasema kama ushahidi upo basi sheria ichukue mkondo wake yani pasiwe na kuchelewesha hukumu.
Mkuu, Nenda polepole. Ushahidi haujathibitika - subiri. Zingatia kwamba Mtuhumiwa naye ana haki zake.
 
Elimu
Elimu
Elimu
Hata nilichoandika ni elimu. Sheria na uwakili ni batili. Unaweza kupeleka ushahidi kabisa pasi na shaka na ni ukweli mtupu,ila kw sbb wakili ana knowledge na ni mbobevu wa kupindua meza akapindua. Wabakaji wengi na walawiti wapo mitaani wanakula bata .
 
Wazazi nawashauri mtoto wako akifanyiwa huo ukatiri, usimpeleke polisi, we muwinde aliyetenda huo ukatiri afe
 
Mkuu, Nenda polepole. Ushahidi haujathibitika - subiri. Zingatia kwamba Mtuhumiwa naye ana haki zake.
Sawa. Ila kesi za hivi zinauma ni kwa sbb watu tunaowaamini ndo wanaoharibu kizazi chetu
 
Kuna mahali nilisikia kazi ya wakili sio kutetea bali ni kuisaidia mahakama kufikia haki. Inatakiwa hata jamaa akikutwa na hatia basi aadhibiwe kwa yale makosa aliyo tenda beyond reasonable doubt.
 
Aiseee basi sawa. Ila huyu kwa watu wanaomfahamu na,wamesoma,nae wanamjua vizuri. Ww utaona ngoja kesi iendelee ila nahofia kukatizwa njiani
A'-aaa. Usiwe na hofu. Kuwa mpole, Kuna rufaa n.k. Halafu, vigezo vya kumfahamu mtu kwa kusoma naye havina mashiko kwa sababu ni muda mrefu umepita na mtu huweza kubadilika tabia.
 
A'-aaa. Usiwe na hofu. Kuwa mpole, Kuna rufaa n.k. Halafu, vigezo vya kumfahamu mtu kwa kusoma naye havina mashiko kwa sababu ni muda mrefu umepita na mtu huweza kubadilika tabia.
Noted
 
OSEFUKANY ameniomba hapo juu nirudie kwa sauti.

Lakini mimi nakuelimisha kidogo. Kuwa na wakili ama kuwakilishwa kwenye shauri LOLOTE Mahakamani au mahekalu ya Haki ni takwa la Kikatiba.

Mtuhumiwa yeyote hawezi kutendewa kama mkosaji hadi pale Mahakama itakapomhukumu kuwa ametenda kosa hilo.

Hivyo pamoja na ushahidi kuwepo, inapaswa mahakama ithibitishe pasina shaka kuwa mtuhumiwa ametenda makosa hayo na anastahili adhabu kwa mujibu wa sheria.

Subira yako itakuwa inawatendea haki wahanga ama waathirika wa tukio ambapo Mahakama katika UHURU wake itatimiza wajibu wake muhimu wa kutoa haki. Ukiendekeza upayupayu unaoufanya hapa ni wazi unakuwa unaishinikiza Mahakama tofauti na utaratibu wa kisheria ulivyo.

Kumbuka hukumu ya kesi ya Zombe na wenzake....
 
Sawa. Ila mara nyingi haki hupindishwa huko mnakoita mahakamani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…