Nyerere hakufilisi uchumi wa nchi. Nyerere alianzisha mashirika na viwanda vingi tu lakini hakujua watanzania ni wezi na wavivu wa kutupwa. Enzi za Nyerere watu waliokuwa wanasoma bure. Hospital bure. Kulikuwa mpaka na kupewa warrant wa kusafiri kwa wanafunzi na watu wengine kama wanamuziki. Kwa kifupi watu wa kawaida ndiyo walikuwa wana-enjoy keki ya Taifa. Hebu nionyeshe katika hizi nchi za sub-Sahara African countries ni nchi ipi wananchi wake walikuwa wanaishi vizuri kama Tanzania kipindi cha Nyerere! Nyerere mpaka raslimali aliziacha kwa matumizi ya baadae. Sasa hizi wanashindana kuzipiga bei.
..Nchi ilifilisika wakati wa awamu ya kwanza.
..baadhi ya matatizo yalisababishwa na sera za kijamaa alizoziamini Mwalimu Nyerere.
..kibaya zaidi Mwalimu alikataa ushauri wa kuchukua hatua za kurekebisha uchumi mapema.
..nashauri msome vitabu vilivyoandikwa na Edwin Mtei, na Andy Chande, mtapata picha ya nini ilisababisha uchumi wetu kuanguka miaka ya 1980.
..Kwenye kitabu cha Andy Chande anaelezea jinsi Mwalimu alivyotaifisha mali za kina Chande na kuanzisha shirika la National Milling.
..tatizo ni kwamba waliopewa kuendesha hizo mali za kina Chande / National Milling hawakuwa na uzoefu wa uendeshaji wa biashara hiyo.
..Matokeo yake shirika la umma kukawa likiendeshwa kwa hasara. Serikali ya Mwalimu iliendelea kutupa fedha ktk mashirika mengi ya aina hiyo.
..Mwalimu pia alitaifisha mashamba ya mkonge. Mkonge ilikuwa moja ya mazao yanayoingiza fedha nyingi za kigeni. Matokeo ya hatua za utaifishaji za Mwalimu Nyerere ni kuanguka kwa sekta ya mkonge.
..kulikuwa na harakati nyingi za kuyasimamisha mashirika yaliyokuwa yametaifishwa, pamoja na kuanzisha mengine mengi mapya ambayo hayakuweza kusimama yenyewe.
..Mwalimu alishauriwa atafute wabia kwa mashirika na makampuni yaliyokuwa wakifanya vibaya, lakini ushauri huo haukutekelezwa.
..Watanzania waliokuwa wakitoa ushauri, au kuunga mkono mabadiliko ya sera za uchumi waliitwa WASALITI / VIBARAKA ndani ya Ccm, na walishindwa ktk chaguzi za ndani ya chama.
..Mfumo wa uendeshaji uchumi wa Mwalimu uliwakera nchi wafadhili na taasisi zilizokuwa zikitukopesha. Matokeo yake ni wafadhili na wakopeshaji kugoma kutupa fedha mpaka pale tutakapobadili sera zetu, na namna tunavyoendesha uchumi.
..Hali hiyo ndio chanzo cha mgogoro kati ya Mwalimu Nyerere na taasisi za fedha kama IMF na WB. Mwisho wa yote Mwalimu aliamua kung'atuka na kupisha wengine waje waendesha nchi.
..Tofauti ya Mwalimu Nyerere na waliomfuatia ni kwamba yeye hakuwa fisadi aliyenufaiki ktk lindi la matatizo ya kiuchumi tuliyokuwa tukikabiliana nayo. Mwalimu aliachia madaraka akiwa hana hata pensheni ya Uraisi.