Hivi Rais Samia amewahi kuandika Makala au Paper ya utatuzi wa changamoto za jamii?

Hivi Rais Samia amewahi kuandika Makala au Paper ya utatuzi wa changamoto za jamii?

..aliandika makala kuhusu falsafa yake ya "4R."

..sina uhakika kama alikuwa na uelewa wa alichoandika, au aliamini kwa dhati andiko lake.

..zaidi, aliitupilia mbali falsafa ya 4R muda mchache baada ya kuchapisha makala hiyo.
Naomba ufafanuzi wa 4R
 
Aliona siasa za Afrika zimejaa ujinga na ukizi approach kwa ideals kama mwenyewe alivyokuwa anajaribu mwanzo utaishia kujuta tu
Ndio maana sasa anarudisha na wale mafioso wa Magufuli
Ni kwamba amaembiwa ukweli, kuwa chama chake hakina ushawishi wa kihivyo, kwahiyo akifanya siasa za kistaarabu zitakigharimu chama chake, na wenye chama hicho chama ndio kinga ya wizi waliolifanyia taifa hili. Ni aidha aendelee na siasa chafu za chama chake, au majizi wamchomoe wasije poteza Dola na kuishia jela.
 
20231228_210910.jpg
 
..kama Magufuli aliandika itakuwa ni ktk majaribio ya wakemia wenzake.

..Magufuli hakuwahi kuandika makala yoyote akiwa kiongozi na mwanasiasa ktk masuala ya kijamii, kisiasa, na kiuchumi.

..Hata hotuba alipozokuwa akitoa hazikuwa zikiwekwa ktk tovuti ya Ikulu kama alivyofanya Mkapa na Kikwete.
Mleta hojahakufanya utafiti kabla ya kuja kulalamika
 
Nimelazimika kuuliza hii kitu, ni muhimu sana kujua. Makala nzito iliyojaa critical analysis na ikapatikana kwenye national au International journals. Paper fulani hivi ya kuzungumzia changamoto mtambuka za jamii yetu ya Kitanzania.

Mambo haya yanaakisi sana uwezo wa mtu. Nafikiri ana Degree na Masters, ziko wapo Research reports zake tuzifanyie Literature Review.

Tanzania inakabiliwa na changamoto nyingi chungu mzima. Lakini hatuoni hatuoni hata moja ikipatiwa majibu ya utatuzi. Nchi ni kama mgonjwa anayesubiri muujiza wa Baba wa Mbinguni tu.
Hivi the late Nyerere alifariki akiwa na PhD?..
 
Hivi the late Nyerere alifariki akiwa na PhD?..

..Mwalimu Nyerere hakuwa na PhD, alikuwa MA toka chuo kikuu cha Edinburgh Scotland.

..Lakini alitunukiwa Shahada za Heshima za Falsafa ni vyuo vingi vyenye hadhi kubwa duniani.

..Na mihadhara aliyokuwa akitoa baada ya kutunukiwa Shahada hizo ilikuwa mizito kwelikweli.
 
Hadi sasa hakuna aliyeleta tasnifu ya Samia licha ya kuwa wapambe wake kila siku wanasema mama yuko kazini.

Chuo kikuu Mzumbe najua wapo humu mtuletee tasnifu hiyo la si hivyo tutaamini yale maneno ya mnabariki wanasiasa vilaza na nishani za kitaaluma kama kina Nape .
 
Nimelazimika kuuliza hii kitu, ni muhimu sana kujua. Makala nzito iliyojaa critical analysis na ikapatikana kwenye national au International journals. Paper fulani hivi ya kuzungumzia changamoto mtambuka za jamii yetu ya Kitanzania.

Mambo haya yanaakisi sana uwezo wa mtu. Nafikiri ana Degree na Masters, ziko wapo Research reports zake tuzifanyie Literature Review.

Tanzania inakabiliwa na changamoto nyingi chungu mzima. Lakini hatuoni hatuoni hata moja ikipatiwa majibu ya utatuzi. Nchi ni kama mgonjwa anayesubiri muujiza wa Baba wa Mbinguni tu.
Unataka "paper" nenda chuo kikuu maktaba ya Afrikana" ukasome "paper".

Mama Samia utakuja kusoma memoirs zake zitakapowachiwa.
 
Baada ya Nyerere, hakuna rais aliyewahi kuandika makala yoyote yenye intellectual content. Mwanasiasa mwingine aliyekuwa anaandika intellectually ni Pius Msekwa tu. Wengine wote wakifanikiwa kuandika makala yoyote utakuta ni mlolongo wa maoni au kumbukumbu ya matukio yasiyokuwa na intellectual content yoyote.
 
..Mwalimu Nyerere hakuwa na PhD, alikuwa MA toka chuo kikuu cha Edinburgh Scotland.

..Lakini alitunukiwa Shahada za Heshima za Falsafa ni vyuo vingi vyenye hadhi kubwa duniani.

..Na mihadhara aliyokuwa akitoa baada ya kutunukiwa Shahada hizo ilikuwa mizito kwelikweli.
Lakini hakujiita Dr Nyerere
 
Back
Top Bottom