Hivi Ramadhani ni mwezi wa kula Sana au wa kufunga?

Chuki haileti maendeleo ila kuita mtu kafiri kunaleta. Juha wewe
Kwani maana ya kafiri uijuavyo wewe ni nini?

Nijuavyo mimi ni mpingaji, anampinga hata Mungu.

Sasa mtu anaeuliza kwanini unafunga mchana halafu usiku unakula sana, huyo ni kafiri tu. Anashindana na Mwenyezi Mungu aliyeweka wazi muda wa kufunga na muda wa kula na kufanya mengine yote ambayo umezuiliwa kiyafanya wakati wa kufunga katika Mwezi wa Ramadhani. Mwenyei Mungu hakuweka kipimo cha mtu kula. Soma...

Qur'an 2:

183. Enyi mlio amini! Mmeandikiwa Saumu, kama waliyo andikiwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kuchamngu. 183





184. (Mfunge) siku maalumu za kuhisabika. Na atakaye kuwa miongoni mwenu mgonjwa au yumo safarini basi atimize hisabu katika siku nyengine. Na wale wasio weza, watoe fidiya kwa kumlisha masikini. Na atakaye fanya wema kwa kujitolea, basi ni bora kwake. Na mkifunga ni bora kwenu, kama mnajua. 184





185. Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur'ani kuwa ni uwongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uwongofu na upambanuzi. Basi ataye kuwa mjini katika mwezi huu naafunge. Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi atimize hisabu katika siku nyengine. Mwenyezi Mungu anakutakieni yaliyo mepesi wala hakutakieni yaliyo mazito, na mtimize hiyo hisabu, na mumtukuze Mwenyezi Mungu kwa kuwa amekuongoeni ili mpate kushukuru. 185





186. Na waja wangu watakapo kuuliza khabari zangu, waambie kuwa Mimi nipo karibu. Naitikia maombi ya mwombaji anapo niomba. Basi na waniitikie Mimi, na waniamini Mimi, ili wapate kuongoka. 186
 
Wapi ulipoambiwa mtu anaweza kuugeuza usiku kuwa mchana na mchana kuwa usiku? Au ni fikra zako tu?

Ni ujuha tu kuwa na dhanna hiyo.
Halafu na wewe Bi Mkubwa, muda huu unatakiwa uwe kwenye swala ya Eid, au uwe umetingwa kweli kweli kuandaa maakuli kwa ajili ya familia yako hapo baadaye!

Haya mambo ya kujibizana na Makafir humu, huoni yatasababisha ushindwe kutimiza majukumu yako mengine?
 
Hiyo Eid ipi inayosaliwa saa nne asubuhi? Halafu kwa ufinyu wa fikra zako za upunguani unafikiri watu wote wanaoingia JF wapo jirani yako.

Ujinga ni mzigo.
 
Umechelewa jamvini karamu imeshaliwa.

Naamini kafiri wa leo ndiye Muumini wa kesho.
Wewe Bibi acha uchoyo! Fanya kutualika basi ili tuje tule Eid! Leo ndiyo siku ya kuhitimisha karamu. Ni mwendo wa kula na kusaza siku nzima.
 
Usichokielewa Waislamu asilimia 90, mwezi wa ramadhani wanaupa heshima hivyo wengi hufunga, ndiyo maana mama mtilie jioni huuza sana futari kwa Waislamu amba wako mbali na wenzio wao masingo, na hata kwa baadhi ya Wakristo ambao wanataka kula chakula chepesi usiku.

Kwa wakristo hili huwezi kuliona, Maana wanaofunga kweresma ni asilimia 10 tu, wengi wao wanaungana kwenye Sherehe ya pasaka tu.

Nina rafiki yangu niko nae ofisini, dhehebu mlokole, huyu jamaa kipindi chote cha kwaresma alikua anafunga, ila kuna siku kaja Dada mmoja, akasema uzuri wa sisi wakristo hatuna muda maalumu wa kufunga unaweza ukafunga hata kwa saa moja tu.
 
Hamna mnapofunga, mnabadilisha tu ratiba ya kula.
Usiku unakua mchana na mchana unakua usiku.

Na ramadhani ndio mnakulaga sana kuliko siku za kawaida
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…