Hivi Russia anasubiri nini kuivamia Ukraine, Kwanini amebaki mpakani tu?

Hao usa na nato hawana cha kumfanya zaid ya mikwara tu
 
hiyo ukraine unayoiongelea usifikiri ni mtoto mdogo, hata kama russia ni super power lakini naye hawezi kufa kwa kipigo cha siku moja, atasumbua sana, pia NATO wana pua yao pale. ila kati ya mataifa maoga na ambayo sio ya kutegemea, la kwanza duniani ni urusi. urusi alijifanya yupo upande wa Gadafi, mwisho wa siku akakaa pembeni anaangalia tu akila za uso. urusi akajifanya yupo upande wa Asad akapeleka hadi silaha kule, mwisho wa siku Damascus imebaki magofu tu na watu wamekimbia nchi, russia hajafanya chochote. ujinga mtupu. angekuwa marekani akisema anatia mguu jua kuwa tayari ameshafika chumbani.
 
miaka 20 tangu aombe uwanachana lakini nato wanaiyogopa urusi mbona poland na hangury walipewa uwanachama chap chap dogo putin ni next level waulize georgia
 
UKRAINE kama akijiunga na NATO halaf RUSSIA asimpe kichapo naachana na kutumia JF inyeshe mvua liwake jua UKRAINE haruhusiwi kujiunga na NATO itaibuka hata vita yatatu ya dunia ila UKRAINE hataruhusiwa kujiunga na NATO hata kwa sekunde
 
Tusishabikie vita wakuu,
Vita isikie kwa mwenzako.

Kikiumana,
nyie nmmnaoshabikia Vita ndo mtakua wa kulaumu na kulaani kwa waliochochea Vita ile.

TULIKUEPO ENZI ZA VITA YA IDD AMIN,

Msoto tulopitia kabla,wakati na baada ya ile Vita hauelezeki kabisa.

Hizi sio Mambo za kushabikia kabisa[emoji3525]
 
Kiduku yeye anakwambia wee peleka jeshi lako mpakani,
Mi ntapiga bomu Moja tu kutoka nilipo watageuka majivu.

Ukiwa na teknolojia Raha sana.[emoji4]
 
Unapenda sana watu wavamiwe wauawe? Wewe ukivamiwa utafurahi?
 
Russia ilishakua zilipendwa kwenye anga za kivita.

Ujamaa kitu kibaya Sana, anaishi Kama Yuko kisiwani[emoji4]
 
Tukuondoa ubishi tunatakiwa kujua kwamba vita ni uchumi namanisha kwamba mwenye uchumi mkubwa ndiyo Huwa anashunda vita .Sasa angalieni kati ya NATO na Russia nani mwenye uchumi mkubwa.Vita inahitaji hela kuighalamia na inaweza chukua hata miaka 10 kuisha Sasa hapo kama una uchumi legevu lazima utashindwa tu.USA ndiyo super power wa DUNIA na pia Kumbukeni kapona na nchi mbili kwa wakati mmoja kwa zaidi ya miaka 20 lakini Bado yupo vizuri kiuchumi,Iraq na Afghanistan wamepigwa na USA kwa pamoja lakini Bado jamaa wako vizuri kiuchumi.
Kwa huu Mgogoro uliopo utaisha kwa mazungumzo tu Wala hakuna vita hapo maana wanaogopa hasara za vita.
 
Anaogopa moto
Rais wa Urusi Vladimir Putin ameishutumu Marekani kwa kujaribu kuisukimiza nchi yake kwenye vita na Ukraine.

Amesema lengo la Marekani lilikuwa kutumia mvutano huu kama kigezo cha kuweka vikwazo zaidi kwa Urusia.

Putin pia amesema Marekani imekuwa ikipuuzia wasiwasi uliyotolewa na Urusi kuhusu kuongezeka kwa vikosi vya NATO barani Ulaya.

Marekani na Muungano wa NATO unaishutumu Urusi kupanga kuivamia Ukraine huku Urusi ikikana mara zote.

Wakati huo huo Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ametoa onyo kwa Urusi akisema uvamizi wowote wa nchi hiyo hautaishia kuwa vita kati ya Ukraine na Urusi bali vita kubwa na kamili ndani ya bara lote la Ulaya.
 
Binafsi naona ugunduzi wa silaha za nyuklia ndio umesaidia kwa kiasi kikubwa kuzuia vita kuu ya tatu ya Dunia. Hii ni kwa sababu, kila nchi kubwa ina silaha za nyuklia, hivyo kila nchi kubwa inaogopa kuanzisha vita, kwani madhara yake yanaweza kuwa makubwa pale silaha za nyuklia zitakapotumika.

Lakini, kama silaha za nyuklia zisingekuwepo Duniani, inawezekana tayari vita ya tatu ya Dunia ingekuwa imeishatokea
 
Afghanistan ipi unayoizungumzia weee hii inayoongozwa na taleban ambayo US nashost zake wameikimbia
Vita sio uchumi imara tuu ingekua ni uchumi tu US asingekimbia SOMALIA asingekimbia VIETNAM asingelikimbia AFGHANISTAN
pia SAUDIA wangelikua washamalizana na HOUTH ila mpaka sasa mambo magumu
ukiachana nakua na chumi imara kuna zaidi yakua na chumi imara ili kushinda vita yeyote ile
nb:-hapo hamna vita ila vita itaibuka endapo UKRAINE itajiunga na NATO nanijambo ambalo halipo halijatokea ba halitatokea ama labda litokee baada ya kuiba vita kali sana na RUSSIA kuchapwa
 
Alitakiwa kujitathmini kabla, Gesi yake atamuuzia nani?
Marekani sio ya kuishtukizia kwenye mapambano, marekani alijaribu na kufanikiwa kwa kiwango kikubwa kuitawala dunia kiuchumi muda mrefu sana
 
LENGO LA PUTIN LIMEANGUKIA PUA.

Putin alijua akitishia kuivamia kijeshi Ukraine Basi NATO wataogopa na kukubali matakwa ya Urusi ili asiivamie Ukraine. Malengo ya Urusi yalikuwa Kama ifuatavyo;

1.Marekani na Washirika wake wa NATO wasaini mkataba na URUS ambao utaipiga Marufuku nchi ya Ukraine kujiunga na NATO mazima.
NATO wamekataa takwa Hilo la URUS wakisema Uanachama wa Ukraine kujiunga NATO ni jukumu la uamuzi wa Mataifa 30 wanachama wa NATO. NATO imeongeza kwa kusema,URUS Haina mamlaka ya kuzuia Sera ya NATO ya OPEN DOOR POLICY hata Kidogo. Ukraine ikikidhi vigezo itajiunga na NATO.

2.Marekani na Washirika wake wa NATO waondoe Siraha zao ambazo wameipa nchi ya Ukraine tangu mwaka 2014. URUS imedai kuwa Ukraine ametumia Siraha hizo kuwapiga Washirika wa Urusi kwenye majimbo ya CRIMEA,DONBASS,LUHANSK na DONETSK.
Marekani na Washirika wake wa NATO inaonekana kabisa wamepuuza matakwa hayo badala yake Marekani na Uingereza wameongeza msaada wa Siraha kwa Ukraine hivi Karibuni.

3.Marekani na Washirika wake wa NATO wasijitanue kwa kuweka Majeshi yake na Siraha kwenye nchi za Ulaya Mashariki ambazo zilijiunga na NATO Kabla ya mwaka 1997. Hapa Urusi ilimaanisha nchi za ROMANIA,HUNGARY,LITHUANIA na LATVIA.
Marekani na Washirika wake wa NATO wamepuuza matakwa hayo. Hivi Karibuni rais wa Marekani JOE BIDEN ameiamuru wizara ya Ulinzi ya Pentagon kuwaweka Wanajeshi 8,500 tayari kupelekwa Ulaya Mashariki mda wowote ule. Tunavyoongea hivi Sasa,Wizara ya Ulinzi PENTAGON imeanza kuwapelekwa Wanajeshi 2,000 nchini Poland kutoka Marekani na Wengine 1,000 walioko Ujeruman imeanza kuwapeleka nchini ROMANIA.

Nchi za POLAND na ROMANIA zote Zina mpaka wa moja kwa moja na nchi ya Ukraine. Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg amesema wazi kwamba NATO haitapeleka Wanajeshi wake nchini Ukraine ambayo sio wanachama lakini itatoa usaidizi wa vifaa vya kijeshi vya kujilinda kwa Ukraine.
 
Urusi naona alkua anataka apewe assurances kuwa Ukraine hatakuwa NATO member, kitu ambayo USA hataweza kumpa hilo jibu,mbaya zaid kaonyesha kapeleka majesh yake mpakan na Ukraine ili awe kwenye position nzur ya kunegotiate na USA,ndio kaharibu, USA naye anapeleka wanajesh wake kwa allied nations na ana supply silaha kwa Ukraine in a broad daylight,kama Russia akikomaa kwa Ukraine hii vita itakua tofaut na zle za mwanzo.

Ukraine hatakuwa yule wa kipindi kile, wala haitakua kama ile ya Georgia.USA naona this time hatoi gepu kwa Russia.undava undava tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…