Hivi shule kama hii ina walimu kabisa watakaoweza kuidai Serikali iwaongezee mshahara bila aibu?

Hivi shule kama hii ina walimu kabisa watakaoweza kuidai Serikali iwaongezee mshahara bila aibu?

kyagata

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2016
Posts
10,406
Reaction score
19,892
Kwa msioifahamu Mburahati, ni shule ya secondari ya kata, iko wilaya ya Kinondoni na mkoa wa Dar es Salaam.

Ni shule iliyopo mjini kabisa nikiwa na maana ina access ya nyenzo zote kuanzia walimu na mpaka vitendea kazi.

Sasa haya ndio matokeo yao ya form 2 kwa mwaka jana.

Je, walimu wa hii shule wanastahili kweli kulilia nyongeza yoyote ya mshahara kutoka Serikalini?

Screenshot_20230108-201415_Opera Mini.jpg
 
Kwa msioifahamu mburahati,ni shule ya secondary ya kata ,iko wilaya ya kinondoni na mkoa wa Dar es Salaam.

Ni shule iliyopo mjini kabisa nikiwa na maana ina access ya nyenzo zote kuanzia walimu na mpaka vitendea kazi.

Sasa haya ndio matokeo yao ya form 2 kwa mwaka jana.

Je, walimu wa hii shule wanastahili kweli kulilia nyongeza yoyote ya mshahara kutoka serikalini?

View attachment 2474008
Ufanisi utatoka wapi shule watoto mia tano mzee mwalimu atalaumiwa bure hapo
 
Kwa msioifahamu mburahati,ni shule ya secondary ya kata ,iko wilaya ya kinondoni na mkoa wa Dar es Salaam.

Ni shule iliyopo mjini kabisa nikiwa na maana ina access ya nyenzo zote kuanzia walimu na mpaka vitendea kazi.

Sasa haya ndio matokeo yao ya form 2 kwa mwaka jana.

Je, walimu wa hii shule wanastahili kweli kulilia nyongeza yoyote ya mshahara kutoka serikalini?

View attachment 2474008
Shule za uswahilini hizo..
Wanafunzi wanashinda kwenye singeli, betting na hawana hofu ya kufail maana watakuwa bodaboda na madalali.
Sisi huku hatima zetu tulishazijua muda tu.

Walimu wapo bize na vikoba

Hayo ya kusoma tushawaachia nyie wa huko osterbay na masaki..
 
Kwa msioifahamu mburahati,ni shule ya secondary ya kata ,iko wilaya ya kinondoni na mkoa wa Dar es Salaam.

Ni shule iliyopo mjini kabisa nikiwa na maana ina access ya nyenzo zote kuanzia walimu na mpaka vitendea kazi.

Sasa haya ndio matokeo yao ya form 2 kwa mwaka jana.

Je, walimu wa hii shule wanastahili kweli kulilia nyongeza yoyote ya mshahara kutoka serikalini?

View attachment 2474008
Walimu sometimes wanalaumiwa bure. Hebu tazama idadi ya wanafunzi waliopo kwenye hilo darasa na utakuta kila somo lina mwalu 1. Hivi mwalimu atawezaje kusahisha na kufuatilia maendeleo ya kila mwànafunzi. Yaani mwalimu asahishe madftari zaidi ya 500? Hii ni bora elimu si elimi bora.
Na Serikali inalijua hilo ndio maana wanasema hadi div 4 kafaulu
 
Kwanini wasidai wakati ni haki ya??

Tatizo la wazazi wengi wanafikiri mwalimu peke yake anafaulisha.

Kama mzazi mtoto wako Akirudia shule huna muda nae WA kumfuatilia masomo yake unamwacha Kwenye disko na vigodoro unategemea nini??

Mtoto akichapwa kidogo mzazi unaenda kuchamba waalimu matokeo yake ndo haya.

Serikali na yenyewe iwathamini waalimu, madai ya nauli na arrears za mishahara Yao walipwe Kwa wakati na madaraja wapandishwe Kwa wakati badala ya waalimu kusumbuka na bahasha za barua za kuomba kulipwa madai Yao.
Waalimu wapi stressed Kwa mawazo,

Wanafunzi wenyewe wanapaswa wajitambue waache utoto na michezo ya kimapenzi.
Wengi wamenunuliwa Simu na wazazi wao na simu hizo zinatumika kuchezea gemu na kutongozana TU basi. Simu wanyang'anywe ili waache kushindwa kucheza gemu.

Waalimu nanyi fundisheni Kwa kutimiza majukumu yenu ipasavyo
 
Walimu sometimes wanalaumiwa bure. Hebu tazama idadi ya wanafunzi waliopo kwenye hilo darasa na utakuta kila somo lina mwalu 1. Hivi mwalimu atawezaje kusahisha na kufuatilia maendelep ya kila mwànafunzi. Yani mwalimu asahishe madftari zaidi ya 200? Hii ni bora elimu si elimi bora.
Na serikali inalijua hilo ndio maana wanasema hadi div 4 kafaulu
Unaposema darasa moja una maana gani?? Si kuna mikondo bro..mimi pia nimesoma kayumba tulikuwa zaidi ya mia mbili mikondo 3...sema tuu watoto wa siku hizi wana mambo mengii
Labda hapo kama mwalimu wa somo ni mmoja shida ipo aisee..
 
Nadhani kuna haja ya kujiuliza shida iko wapi..watoto wakati wanamaliza std 7 uwezo wao ulikuwaje maana "garbage in..garbage out",walimu wanafanya kazi zao kwa weredi? wazazi wanafuatilia maendeleo ya watoto wao?

Maswali ni mengi sana..natamani ningepewa nafasi kutoa suggestion unfortunately hata nikishauri umuhimu wangu hautaonekana na mawazo yangu yatamzidishia manoti kiongozi tu
 
Unaposema darasa moja una maana gani??.si kuna mikondo bro..mimi pia nimesoma kayumba tulikua zaidi ya mia mbili mikondo 3...sema tuu watoto wa siku hizi wana mambo mengii
Labda hapo kama mwalimu wa somo ni mmoja shida ipo aisee..
Mimi nimesoma sekondari o level ya serikali sema haikuwa shule ya kata bali shule kongwe za kitambo tulikuwa na mikondo minne a mpaka d kwa kila darasa na kila darasa lilikuwa na wanafunzi wasiozidi 35 na hiyo mikondo sio ya kuingia kwa kupokezana, hapana kila kidato kilikuwa na madarasa manne.
Sasa hawa wanafunzi 500 hata wawe na mikondo miwili kila darasa lina wanafunzi zaidi ya 200 ni changamoto kwa walimu ukichanganya na ni kizazi cha internet basi sometimes makosa sio ya walimu bali ni mazingira
 
Back
Top Bottom