Hivi shule kama hii ina walimu kabisa watakaoweza kuidai Serikali iwaongezee mshahara bila aibu?

Kwa msioifahamu mburahati,ni shule ya secondary ya kata ,iko wilaya ya kinondoni na mkoa wa Dar es Salaam.

Ni shule iliyopo mjini kabisa nikiwa na maana ina access ya nyenzo zote kuanzia walimu na mpaka vitendea kazi.

Sasa haya ndio matokeo yao ya form 2 kwa mwaka jana.

Je, walimu wa hii shule wanastahili kweli kulilia nyongeza yoyote ya mshahara kutoka serikalini?

View attachment 2474008
Ungetafuta sababu za matokeo kuwa hivi ungekuwa umefanya la maana sana. Huku kuangalia outcome badala ya source, kumesababisha hukumu kuwa tofauti na uhalisia
 
  • Thanks
Reactions: K11
Kwa msioifahamu mburahati,ni shule ya secondary ya kata ,iko wilaya ya kinondoni na mkoa wa Dar es Salaam.

Ni shule iliyopo mjini kabisa nikiwa na maana ina access ya nyenzo zote kuanzia walimu na mpaka vitendea kazi.

Sasa haya ndio matokeo yao ya form 2 kwa mwaka jana.

Je, walimu wa hii shule wanastahili kweli kulilia nyongeza yoyote ya mshahara kutoka serikalini?

View attachment 2474008
Kosa la elimu yetu ni moja tu ...kushindwa kuhusisha ufanisi wa wanafunzi na mishahara ya walimu ....inatakiwa shule inayo fanya vizuri ndiyo walimu walipwe vizuri na kupanda vyeo na madaraja kwa kuangalia ufanisi wa masomo kwa wanafunzi
 
Sasa kama walifaulu hesabu iliyoandikwa kwa KISWAHILI kwa ku-shade au kuchagua kuanzia swali la kwanza hadi la mwisho....watafaulu vipi kwa kuambiwa habari za ‘factorize’ au numerator na denominator?

MAE 😂😂
 
Kwa msioifahamu mburahati,ni shule ya secondary ya kata ,iko wilaya ya kinondoni na mkoa wa Dar es Salaam.

Ni shule iliyopo mjini kabisa nikiwa na maana ina access ya nyenzo zote kuanzia walimu na mpaka vitendea kazi.

Sasa haya ndio matokeo yao ya form 2 kwa mwaka jana.

Je, walimu wa hii shule wanastahili kweli kulilia nyongeza yoyote ya mshahara kutoka serikalini?

View attachment 2474008
Singeli + Vigodolo + Betting + Ukabaji + Ngono + uswahili wa mitaa yao + hali ngumu ya maisha ya ile mitaa + ku’shade hesabu (shule ya msingi) + elimu bure (elimu ya huruma) ARE DIRECTLY PROPORTIONAL na hayo matokeo.....
 
Kosa la elimu yetu ni moja tu ...kushindwa kuhusisha ufanisi wa wanafunzi na mishahara ya walimu ....inatakiwa shule inayo fanya vizuri ndiyo walimu walipwe vizuri na kupanda vyeo na madaraja kwa kuangalia ufanisi wa masomo kwa wanafunzi
Walimu wa ilboru, kibaha, mzumbe ,tabora boys , hao ndio watajikuta wanalipwa mishahara mikubwa maana wanapelekewa cream.
Kuna shule watoto wanajua asee, ukiangalia watoto wa ilboru ni A tuu kama utitiri

Hizi za uswazi huko watoto wanaenda kwa kulazimushwa hata wapelekewe maprofesa ni zero tuu
 
Kwa msioifahamu mburahati,ni shule ya secondary ya kata ,iko wilaya ya kinondoni na mkoa wa Dar es Salaam.

Ni shule iliyopo mjini kabisa nikiwa na maana ina access ya nyenzo zote kuanzia walimu na mpaka vitendea kazi.

Sasa haya ndio matokeo yao ya form 2 kwa mwaka jana.

Je, walimu wa hii shule wanastahili kweli kulilia nyongeza yoyote ya mshahara kutoka serikalini?

View attachment 2474008
mpwayungu village
 
Inashangaza na kufikirisha sana.Kesho ya hawa watoto sijui itakuwaje.
 
Matokeo ya form two mwaka juzi haya..ubaya unavuma sana kuliko uzuri
IMG_1371.jpg
 
Kwa msioifahamu mburahati,ni shule ya secondary ya kata ,iko wilaya ya kinondoni na mkoa wa Dar es Salaam.

Ni shule iliyopo mjini kabisa nikiwa na maana ina access ya nyenzo zote kuanzia walimu na mpaka vitendea kazi.

Sasa haya ndio matokeo yao ya form 2 kwa mwaka jana.

Je, walimu wa hii shule wanastahili kweli kulilia nyongeza yoyote ya mshahara kutoka serikalini?

View attachment 2474008
Hapa waalimu, wanafunzi, wazazi pamoja na serikali wote, hawajitambui!
 
Mie nimesoma gov enzi hizooo kuanzia la kwanza had form 6...

Niseme ukweli hata kipind hiko walimu walikua hawafundishi wakati tupo form 4 masomo matano kati ya tisa hayakua na walimu na hayo yenye walimu ticha anazama mara mbili kwa wiki sa ingine mwez mzima hamumuoni...

Ikaja A LEVEL pia hvo hvo walimu hawaingii...

Licha ya yote hayo watu tulikua tunazama mapindi mtaani tuna connect na watoto wa shule bora kusaka matirio na tunagonga one kama kama kawa shule tulikua tunaita kituo cha mitihan tu...

Kwa hyo shule ka hyo watoto kufeli ni watoto wenyewe siku hz mambo mengi mara singeli, mara tik tok, mtu anaenda shule na kidaftari kimoja atapata ngapi,

Wazaz wenyewe ndio sie wa 1980's tunawaza kula tunda kimasihara[emoji28] kuna nn hapo...
 
Bado swala la elimu ya ngazi za chini Tanzania hii ni ukungu mzito haswa🌫🌫🌫
 
Wanafunzi mia tano darasa Moja walikua wengi sana yaani ni idadi ya shule nyingine kabisa. Kwahiyo hapo waligawanywa katika mikondo 6 au Saba. Kutokana na idadi ya walimu waliopo Kama ni wachache kufelisha ni jambo la kawaida.
Duh! aisee? Hata kama walimu ni wachache na wanafunzi ni wengi bado kuna kitu (sintofahamu) upande wa wanafunzi na wazazi wao.
1. Wazazi hawafuatilii maendeleo ya watoto wao (Ripoti za masomo)
2. Wanafunzi hawajali, hawazingatii, wanapuuzia, hawaoni umuhimu wa masomo wanayofundishwa
NB: Inawezekana hakuna ushirikiano wa dhati kati ya walimu, wazazi na Bodi ya shule.
Wanafunzi ni watu wa kusimamiwa na kuelekezwa. Mwalimu mkuu(Headmaster) ndiye Katibu wa Bodi na anatoa Taarifa kila robo mwaka ya hali halisi (mafanikio na changamoto) na mwenendo mzima wa shule mbele ya Bodi. Je, Bodi ya shule imesemaje kuhusu matokeo hayo? Kama Bodi imeridhika; ndo basi tena tuseme "Yajayo yanahuzunisha zaidi"
Hizo shule zingine zimewezaje kufaulisha wanafunzi wao? (walau kwa kiwango cha kuridhisha)au Hiyo shule ndo tuseme iko Dar zaidi?
 
Back
Top Bottom