reymage
JF-Expert Member
- Aug 5, 2021
- 12,203
- 28,789
Bora umesema kakaKwa taarifa yako mwanafunzi anayejielewa, hawezi kumtegemea mwalimu kwa 100% ili afaulu! Isipokuwa 25% tu.
Umeshajiuliza ni kwa nini kuna wanafunzi wawili waliopata ufaulu wa division two!! Wazazi wa hao wanafunzi wana mchango gani kwenye malezi ya watoto wao?
Mzazi unatoka nyumbani saa 11 alfajiri, halafu unarudi saa 5 usiku! Unategemea nani atakulelea mtoto wako mtukutu? Mwalimu ambaye aliongezewa mshahara wa kueleweka enzi Rais ni JK! Hilo haliwezekani. Na walimu nao ni binadamu. Hivyo wana njia nyingi za kufikisha ujumbe kwa wahusika.
Serikali nayo kujaza darasa la wanafunzi 500 kwenye shule moja nayo ni akili, au ni matope? Na hapo unaweza kukuta hiyo shule hata uzio haina!! Bado unategemea maajabu!! Mbona watoto wanaosoma shule za boarding, wengi wanafanya vizuri?