Hivi siku hizi hakuna majambazi?

Sijaelewa
 
Hela ya sadaka hamna mwenye uhalali nayo acha hao majambazi waichukue
 
Tukio kama hilo ni ngumu kufanyika bila kuwa na taarifa za ndani (inside job)....
 
Siku hizi ujambazi umerahisishwa,shamba la bibi ,bibi hayupo tena japo awachukulie bakora wajukuu wakora,hivyo wanajichukulia tu,hawahitaji tena japo kuchukua manati ili kumtisha bibi!
 
Tanzania sasa hivi ufanye ujambazi au ugaidi utakuwa kwanza akili huna na hujipendi wewe binafsi kama wewe
 
Umewamiss mkuu?
 
Kisa kasema hivyo? Hebu jaribu kuwa jambazi kuprove alichosema
No. siwezi kuwa jambazi, Mungu anakataza.

ushwari huwa hausababishwi na uwepo na uimara wa mabunduki na askari (Jeshi). ushwari unaletwa na Mungu mwenyewe baada ya sisi watu wake kumuomba. Ushwari huanzia katika ulimwengu wa roho
 
Sema mwendo ni kuchota tu.
Vyombo vya usalama vya Tanzania sasa hivi wana zero tolerance kwenye ugaidi na ujambazi iwe kwenye planning stage ,au implementation

Ni zero tolerance

Kaa mbali mwananchi na ujambazi na ugaidi kataa kuwa sehemu yake at any stage utaumia tena mno kaa mbali na schemes za ujambazi au ugaidi
 
Kuna wale walikuwa wahaishi mapangoni kule mwanza, siku wanapelekewa moto ilikuwa ni zaidi ya vita. Zilirindima risasi z kutosha hadi wakawa neutralized.
Aisee umenikumbusha ule mtiti wa wale washenzi , ilikuwa ni balaa 2004 kama sikosei hiyo mzee , actually Mimi nilikuwa mhanga wa hao wapuuzi , nilikuwa nakaa na wazazi wangu mtaa wa Kiloleli - Mwanza , Tulivamiwa usiku mmoja wale wapuuzi walikuwa wanavunja milango kwa mawe flani yanaitwa Fatuma .
Na walikuwa wanafunga mtaa ,njemba thelathini , na wana magobole na silaha nyingine kali ,panya road wakasome .
Aisee nakumbuka siku hiyo ile nyumba niliyokuwa nakaa walipiga sana na kujeruhi watu na wengine wanawake walibakwa kabisa .
Yale majamaa sitasahau kabisa ,na sehemu au pango walilokuwa wanajificha ni hapo juu ya kilima cha wakatoliki karibia na PΓ rokia ya Kiloleli na shule ya Montessori .
Yalikuwa yanajificha hapo halafu usiku yanaingia mtaani kukinukisha ,halafu wengi walikuwa wakurya ,
Siku wanaenda kufurushwa mle aisee zilipigwa risasi zaidi ya masaa sita na polisi ila walifanikiwa kuyaua mwishoni ,ila naamini kuna mengine yalitoroka .
2004 -2005 ilikuwa miaka hatari sana Mwanza kwa ujambazi wa kutumia silaha
 
Kwani hao uliowataja walikuwa majambazi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…