Hivi tatizo kubwa la Wakoloni lilikuwa ni nini mpaka tukaamua waondoke?

Kwani leo hii hakuna migrant labor?
Kuwafanyisha kazi waafrika ilikuwa ni mfumo wa kikoloni ili wapate malighafi ,waafrika walikuwa wanalima kwa chakula chao , moja kwa moja ni kuwatoa kweny mazoea yao mpaka uchumi wa kutafuta pesa ndio maisha magumu yalianza hapo .
 
Hii kwangu ni topic/wazo/swali bora zaidi kwa muda wote!

Nimekuwa najiuliza hili suala miaka yote!
 
Kuwafanyisha kazi waafrika ilikuwa ni mfumo wa kikoloni ili wapate malighafi ,waafrika walikuwa wanalima kwa chakula chao , moja kwa moja ni kuwatoa kweny mazoea yao mpaka uchumi wa kutafuta pesa ndio maisha magumu yalianza hapo .
Ni nchi gani ambako watu hawakufanyishwa kazi ngumu? Tuache kujikita kwenye historia ya Africa pekee!

Utumwa umefanyika duniani kote!
 
Ni nchi gani ambako watu hawakufanyishwa kazi ngumu? Tuache kujikita kwenye historia ya Africa pekee!

Utumwa umefanyika duniani kote!
Waafrika hawakuwa na kodi kumbuka , walikuwa wanalima na kuwinda pamoja na ufugaji ili kupata chakula cha kila siku ...Hawawahi kulima mazao ya malighafi pia .
 
Waafrika hawakuwa na kodi kumbuka , walikuwa wanalima na kuwinda pamoja na ufugaji ili kupata chakula cha kila siku ...Hawawahi kulima mazao ya malighafi pia .
Hawakuwa na kodi kivipi wakati kulikuwa na tawala za machifu na majeshi ya makabila? Kulipokuwa na vita vya makabila wanajeshi walikuwa wanahudumiwa vipi ?
 
Wivu tu.

Nyerere aliulizwa swali jepesi tu kwa nini anatafuta uhuru na amejiandaa vipi na huo uhuru akashindwa kujibu zaidi ya blah blah

Pale ndio nikajua akili zetu zilivyo
 
Mkuu unaweza kuwa na umri mkubwa zaidi yetu lakini una mentality mbovu sana (with due respect).

Umesema ni bora kuwa na Kiongozi Mwafrika hata kama ni mbovu? Halafu unatukana vijana! Aisee!

Unaidhihaki South Africa lakini hautabisha kwamba, Waafrika kusini hawaikimbii nchi yao lakini Waafrika wengi ikiwemo Watanzania wanapambana kuingia Africa kusini kutafuta unafuu wa maisha.

Kumbuka yale uliyosoma kuhusu ukatili wa Wakoloni Africa ni mode of life ambayo imepitiwa na kila nchi na kila human race!

Acha ujinga!
 
Waafrika hawakuwa na kodi kumbuka , walikuwa wanalima na kuwinda pamoja na ufugaji ili kupata chakula cha kila siku ...Hawawahi kulima mazao ya malighafi pia .
Hiyo stage kila nchi imepitia, watu walikuwa wachache hapakuwa na uhitaji mkubwa, lakini kumbuka vizazi vilikuwa vinakuwa na ushindani haukuepukika!

Afrika kabla ya ukoloni palikuwa na falme nyingi na ushindani ulikuwepo, hata tungeachwa wenyewe Utumwa ungekomaa, ubaguzi ungekuwepo na vita zingepitiwa sana tu kwani zilishakuwepo!
 
Wangekuwepo tungekuwa mbali sn kimaendeleo, sahivi tunaongozwa na majangili + majambazi ya mali za umma.
 
Kwasasa mimi naona tumebadilisha wakoloni wametoka wazungu wamekuja waafrika wenzetu, tuna washika tonge hawa washika tonge ukiwa na hoja inayo gusa masilahi yao, (,wanyang'anya tonge), watakushughulikia, hata kukupoteza

Unyumbu wa kisiasa, unyumbu wa kisiasa ni tabia ya badhi ya wanaopewa dhamana, (washikatonge), kuahahirisha kufikiri kwa nafsi kwasababu ya kujipendekeza, kulitumikia kundi fulani kwa masilahi binafsi na uoga kwa viongozi wao bila utii, (unafiki), a.k.a kujizima data, tuseme kuahirisha kufikiri kizalendo, (uchawa)

Kuahirisha kufikiri kwa nafsi -suspending an individual reasoning
 
sahihi sn
 
Hizo falme unazijua kweli ? Jamii za kiafrika zilikuwa na tawala zao , mifumo yao ...Wakoloni kwa ujumla nao walikuwa na mifumo yao ...Baadhi ya falme walikuwa wanatoa mazao kama sehemu ya kodi zao za maendeleo .

Mfumo walioanzisha wakoloni ulikuwa ni mpya ambao uko mpaka leo.
 
Bado tuko kwenye ukoloni tena mbaya sana unaotufanya tujisahau , ebu fikiria tuna uhuru gani wakati hata sheria zetu zimeandikwa kingereza ..
 
Hiyo ya kufirwa hadharani ndio mmefundishwa shule za national? Ipo kitabu gani mkuu!
Nenda kapakue vitabu mwenyewe.ila ukimuona mwafrika anautamani ukoloni ujue hana ubongo kichwani.
 
Mbona ni basic history kwenye elimu ya msingi? Unadhani wakoloni walipoingia Africa hawakukuta tawala zilizojiimarisha zenye nguvu na dhaifu?
Hizo tawala zote zilikuwa na mifumo ya kodi, ziliitwa tribute kwenye mamlaka. Suala la kodi halijaletwa na wazungu, lilikuwepo.
 
We jamaa acha ubishi , kodi iliyaoanzishwa na wakoloni unajua? kilifika kipindi kijana akifika umri fulani lazima alipe kodi ya kichwa tena kwa sarafu ndio maana waliacha mashamba yao na kwenda kulima kwa wakoloni .

Umesoma historia ipi ? Wasandawe, wasukuma, wapare , wazigua wachaga , waha walikuwa na kodi ipi kabla ya kuja wakoloni ?
 
Reactions: Tui
Bado tuko kwenye ukoloni tena mbaya sana unaotufanya tujisahau , ebu fikiria tuna uhuru gani wakati hata sheria zetu zimeandikwa kingereza ..
Matumizi ya kingereza siyo tatizo mimi nimejifunza kwamba ili uweze kuelewa, kujifunza na kufundisha vizuri maneno ya kiingera ni rahisi sana hutengeneza ufafanuzi kirahisi sana, kwavike watu hawakijui vizuri kimombo ndiyo maana wanakichukia,
 
Sasa kingereza ni lugha yako ? Yaani unalazimisha lugha ya kigeni kwako , machifu walikuwa wanatumia kingereza kweny tawala zao?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…