Hivi tungekodi kampuni ya Uingereza kuchunguza makinikia tungejua tulichojua?

Una akili sana we jamaa.
 
hao wakina Maluma mnaowadhalau ndio walioleta chachu ya kubadilisha sheria za madini,pamoja na kutishwa sana na wapuuzi kama nyie eti tutashitakiwa Miga
Hii nchi wajinga ni wengi, Lissu alisema kama mnakamata makontena mjitoe MIGA na mbadili sheria maana tunaibiwa kupitia sheria sio makontena!!!

Sasa si ndio mlichofanya mkabadili sheria kabla ya negotiation kama alivyoshauri Lissu, sasa toka lini kubadili sheria utashtakiwa MIGA? nlichogundua waTanzania wengi hatufuatilii mambo tunakurupuka tu.
mbona accecia walifutiliwa mbali na hawakwenda mahakamani Kudai fidia,Kama walikuwa halali na hawaibi?
Walifutiliwa mbali wapi si mliingia ubia na kampuni yao mama na mkaanzisha subsidiary ambayo mmepewa 16% hisa huku wao wakipiga 84% zote then mmewafutilia wapi??

Mwanyika mliyemuita msaliti na jizi hadi JPM akasema anawasiliana na Lissu!!....... Ndio mkampa ubunge wa CCM huko Makambako!!

Kweli JPM aliwalaghai wengi sana
 
Kuna msemo unaosema kwenye msafala wa Mamba na kenge wamo, wewe unajua aliyekuwa akiiba tarifa za accecia na kuzileta selikalini?ukiambiwa serikali inamkono mrefu usiulize,Watu wengine wamo humo kwa niaba ya serikali hata Kama watasemwa vibaya, maana wapo kikazi,wakimaliza kazi Ndio wanapewa kazi nyingine za kuwapoza,nyie huku mtaani mnabaki kubishana tu.
 
Hayo makampuni sio ya kigeni, ni yake binafsi na washikaji zake. Yanaitwa ya kigeni ili tuyalipe hela ndefu ya kigeni
 
Acha kuongea vitu usivyovijua wewe...

Uliza TANESCO walitangaza tenda mara ngapi hadi anakuja kupatikana mtu mwenye sifa!! Sijui ni nani aliwadanganya habari za software ya ku-monitor umeme!

Moja ya tenda za huo mradi ni hii hapa chini:-


Ona hapo #4. Tenda ilianza kutangazwa back 2016, ikaja kurudiwa November 2017, na tena 2018 lakini bado haikupatikana kampuni yenye sifa, na ikaja kutangazwa tena June 2020! Je, baada ya kutangazwa tena June 2020, alipatikana mzabuni?

Jibu hili hapa chini :-

Unaona hapo, waka-extend muda from September to October...

What happen next? Jibu tena hili hapa chini:-



Hata baada ya ku-extend muda hadi October bado ngoma ilikuwa mbichi ndipo wakatoa hiyo taarifa mwezi November ya nia yao kuongeza muda!!

Sasa hivi kwa akili yako kama lingekuwa jambo rahisi rahisi tu unadhani lingetokea hilo suala la kila wakati bidders kuomba clarification na hatimae ku-extend deadline lakini bado unashindwa kupata mtu na kuamua kutangaza upya?
na kwa kumbukumbu zangu hata hapo hakuweza kupatikana!!

Btw, muda wote huo JPM si bado alikuwa mzima na bukheri wa afya... kwanini basi utawala wake haukutoa hiyo tenda kwa Watalaamu wenu wa IT?

Narudia kama nilivyokueleza mwanzo na ninavyowaeleza wenzako: TAFUTENI TAARIFA badala ya kuleta porojo kwenye mambo msiyoyajua!
 
Kwahiyo ungekuwa wewe ndo mfanya maamuzi ungechukua kampuni ya Kitanzania hata kama haina sifa na haijawahi kufanya hiyo kazi kisha ikushauri?

Sasa anakushauri nini wakati hata mwenyewe hajawahi kufanya kazi husika?

Hivi nyie watu mnajua mnachokiongea kweli nyinyi?!

Nawe nitakueleza: Hizo habari za mfumo wa kompyuta HAMJUI what's it all about! Huu sio mfumo like just installing softwarre and you're done kama mnavyodanganyana!

Angalia Post #66 hapo juu nimeweka ni mara ngapi TANESCO walitangaza tenda ya hicho mnachodhani ni it's just a electricity monitoring software, na tena ilikuwa wakati wa huyo huyo mnayemuona mzalendo!!

Chachu ya kubadilisha sheria ya madini haikuletwa na akina Mruma, again kama unavyodhani! Angalia Sheria ya Madini ya mwaka 2010, Kifungu cha 12 ambayo ilianza kutumika 2012 inayosema:-
 
Chige
Ona hapo #4. Tenda ilianza kutangazwa back 2016, ikaja kurudiwa November 2017, na tena 2018 lakini bado haikupatikana kampuni yenye sifa, na ikaja kutangazwa tena June 2020! Je, baada ya kutangazwa tena June 2020, alipatikana mzabuni?

Hiyo haina maana kwamba Tenda ilianza kutangwazwa back 2016, etc. - Bali maana yake ni hizo regulations zitakazotumia kumtafuta Bidder ndio za hiyo miaka ya July 2016, revised ....
Hii tenda inaonekana GPN(General Procurement Notice) ilitangazwa 18th Feb. 2020 na Specific Procurement Notice ilitangwazwa 22nd June 2020
 

..tatizo la hawa vijana ni kusikiliza habari za upande mmoja.

..hawajisumbui kutafuta UKWELI kwa kujiridhisha na taarifa toka vyanzo mbalimbali.

..nina hakika wakati mgogoro ule unaendelea hawa vijana hawakujisumbua kutafuta habari toka vyanzo vya acaccia au barrick.

..matokeo yake wamejiaminisha / wamejipotosha kwamba mgogoro ule haukufika mahakamani au miga kama wanavyopenda kusema.

..acaccia walikwenda mahakamani na shauri lao lilisitishwa baada ya barrick kukubali kununua hisa za minority shareholders.

..baada ya acaccia kuwa 100% miliki ya barrick ndipo majadiliano na serikali ya Tz yakaendelea na kufikia conclusion.

..kwa upande mwingine Tz / serikali ndio walalamikaji kwamba tumeibiwa usd 191 billion. Sasa tujiulize kwanini hatukushtaki ktk mahakama yoyote?

..hivi ni mtu gani mwenye akili timamu anaweza kuibiwa usd 191 billion halafu akaridhika na kusitisha madai yake kwa kulipwa usd 300 million?
 
Kwa hicho kipengele cha ku-revise, upo sahihi, nili-overlook! Nimechanganya suala la hiyo the so-called just a software na mradi mzima wa TAZA ambao moja ya implementation zake ilikuwa ndo installation ya hiyo software!

Lakini multiple deadline extension ya hiyo tenda bado inathibitisha kitu kile kile kwamba it's not that simple na ndo maana mara kwa mara Bidders walikuwa wanaomba clarifications!!

On top of that, hiyo tenda ilitangazwa wakati wa uhai wa JPM, kwahiyo kwavile wanaamini ingekuwa wakati wa JPM hilo shavu angepewa Mtanzania basi tenda mzima ingekuwa local. Na kwavile financier ni World Bank, I doubt kama World Bank wangekubali aliyeshinda alipwe 30M wakati hiyo pesa inatoka kwao!!!

Thanks any way!
 

Kasahau na zile Noah zetu [emoji23]
Umeelezea vile vile ninavyojua hata mimi wa la 7!
 
Mkuu, Mwanyika si mtu wa kawaida JPM RIP alishikwa sikio.
 
Yani we bado upo gizani, ile report ya makinikia ilikuwa ni blahblah za awamu danganyifu iliyopita. Hakuna la maana baada ya pale na makinikia yanatoka kama kawaida tangu mwendazake akiwepo ni kiini macho, ni upupu mtupu hakuna cha nini wala nini.
Makinikia sasa yanakwenda kama makinikia sio kama mchanga. Kinacholipwa sasa sio kile cha mchanga. Hii ni mojawapo ya faida za ule uchunguzi.
 
Yaani hili suala la watu kupenda kusikiliza taarifa za upande mmoja, tena upande wa wanasiasa inaniogopesha sana manake tafsiri yake ni kwamba, taifa litaendelea kuburuzwa na wanasiasa kwa sababu wanafahamu watu huwa hatutafuti ukweli!

Halafu umenikumbusha hilo la Barrick kumiliki 100% manake kuna kitu kila nikijiuliza, huwa nashindwa kupata jibu!!

Mwanzoni, out of 100% Share of Acacia, Barrick walikuwa wanamiliki around 64%. Na kama hivi sasa wanamiliki 100% ina maana minority shareholders waliuza around 36% shares of Acacia... kampuni iliyosajiriwa Tanzania!

Kwa mujibu wa Sheria ya Kodi ya Mapato, hawa jamaa walitakiwa kulipa 30% Capital Gains Tax lakini sijawahi kusikia popote kwamba hii kodi ililipwa... what am I missing?!
 
Kipindo hicho watu walikuwa wanogopa kunde kutoa rushwa kwa PPRA na hakika hata hiyo kampuni hana vigezo vyovyote vile zaidi kuhonga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kipindo hicho watu walikuwa wanogopa kunde kutoa rushwa kwa PPRA na hakika hata hiyo kampuni hana vigezo vyovyote vile zaidi kuhonga

Sent using Jamii Forums mobile app
1. Vigezo vilikuwa ni vipi?
2. Hiyo kampuni ilikosa kigezo kipi, kipi, kipi, kipi, kipi, kipi, kipi, na kipi miongoni mwa vigezo ambavyo vilikuwa vinatakiwa?!
 
na kutishwa sana na wapuuzi kama nyie eti tutashitakiwa Miga, mbona accecia walifutiliwa mbali na hawakwenda mahakamani Kudai fidia,Kama walikuwa halali na hawaibi?
ACACIA haikufutwa ilibadili "Letterhead", watu ni walewale na makunikia yanaendelea kubebea, mamlaka ya migogoro bado ni London na siyo Mahakama za Tanzania, smelter bado hakuna, 50/50 economic benefits siyo fedha. Kimoja tu ndiyo akina Kabudi waliweza; kupandisha mrahaba kutoka 6% hadi 16%.
Kasahau na zile Noah zetu [emoji23]
Umeelezea vile vile ninavyojua hata mimi wa la 7!
Wewe ni zaidi ya la Saba kama unaelewa issue ya Noah
 

I was joking
Or in other word Taking a piss
Thanks anyway [emoji120]
 
Tusinge kodi kampuni za nje tungeweza kujua hata tuna Gesi kiasi gani?.
 
Mbona sasa mliishia kupewa kishika uchumba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…